ntogwisangu
JF-Expert Member
- Nov 25, 2011
- 524
- 164
Kwa mjanja yeyote wewe ni dokta!Najaribu kuangalia uwiano wa malipo ya 'wateule wetu' na wafanyakazi wengine wa umma...
Daktari katika hospitali zetu za umma analipwa call allowance ya shilingi 10,000/= kwa masaa 12 au 24 anayofanya (masaa yanategemea na utaratibu wa hospitali) na tena basi, sehemu nyingine wanaikata kodi!
Nimeambiwa barua ya kuongeza hiyo 'posho' kutoka 10 hadi 30 ilipigwa danadana hadi wakasahau! Kwa sasa haijulikani ilipo,so now hakuna mwongozo wa hayo malipo kwa sababu hakuna basis, kama kawaida mwajiri anafurahia hali kama hii, so wengi wanapewa 10 kwa sasa!
Nadhani, ndiyo maana nasikia madokta wamekuwa wengi bungeni kwa sasa.
Na unachokifanya na wewe unapigania uongezewe mapato, kuwa muwazi na jenga hoja nzito! Ukishindwa nenda kachukue CCD kwa gonjwa, piga kimya, lisongeshe!!!