Sakata la Makonda na Utapeli wa Gari: Kamwelwe(Mwenye gari) anadaiwa ni mkimbizi, tapeli na katimuliwa Burundi

Nipo Tanzania ila magari bado nafata huko nipo kwenye Utalii kwa hiyo Cruiser natoa kule unataka gari gani?
20221020_124654.jpg
20221020_124700.jpg

Unyama kama huo wa 2013 naupata kwa kiasi gani mpaka kuusajili
 
Two wrongs don't make a right.

Kama Kamwele sio mtz haiondoi haki yake ya kuporwa Range yake na DAB.
 
Muuwe kabisaa mkuu🤣🤣🤣, vipi mkuu bado uko bondeni au ulishatoka nataka ndinga
Nipo Tanzania ila magari bado nafata huko nipo kwenye Utalii kwa hiyo Cruiser natoa kule unataka gari gani?
View attachment 2392672View attachment 2392673
Unyama kama huo wa 2013 naupata kwa kiasi gani mpaka kuusajili
Kodi pekee ni 23m kwa miaka hiyo kununua inacheza rand 180,000 mpaka 250,000 na zidisha na 150 tsh upate shilingi..disco sio ghali sana na zipo nyingi..
 
Kamwele kagushi nyaraka inawezekana hata gari nyaraka za gari kaghushi pia.
 
View attachment 2391363
SAKATA LA MAKONDA! WAKO WAPI WAANDISHI WA HABARI ZA KIUCHUNGUZI?

Jamaa anaedai Kumdai Alokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu, Paul Makonda kumbe ni Tapeli na Kashatapeli wengi tu Hapa Nchini Tanzania.

Cha Ajabu ni Waandishi wetu kuandika Habari Nyepesi nyepesi na Kuacha Mambo ya Msingi sana yanayo Muhusu Bwana Kamwelwe.

Taarifa zinaonesha kuwa Kamwelwe ni Tapeli wa Kimataifa na Kwao ni Burundi, Watu waliotapeliwa na Mrundi huyo ni wengi sana. Lakini mshangao ni Kwanini tapeli aonekane Malaika wakati taarifa zake zinajulikana huko Mtaani?

Sio Wema tu aliewahi kulalamika wala siyo wafanya biashara wa Madini, Muhuni Kamwelwe kashawaliza Wengi sana Hapa Nchini mpaka akakimbia Tanzania baada ya Kujua anakaribia Kukamatwa kwa Utapeli wake.

Yani kila kona anatapeli huku akisafishwa ma magazeti wakati kumbe hata nchini kwake ni BURUDI.

Na Inasemekana huko Burundi kwao haruhusiwi kukanyaga Sababu Serikali ina Taarifa za Utapeli wake na Imemtimua.

Sasa Ajabu ni Mkimbizi anasumbua Raia wa Nchi yao na Taariza za Uchafu wake watu hawazichimbui.

Tizama hizi Nyaraka Muhuni alivyo Gushi.

Sauti kutoka Nyikani
View attachment 2391364
Mtoa mada nami nikuulize swali maana naona kama hukutafakari kabla ya kuleta hili pizza, je raia mwenye kosa la jinai anawezaje kufukuzwa nchini kwake? Jibu nikuulize tena
 
Wakati unanijibu ambatanisha na ushahidi zikiwemo sheria na kanuni za uraia wa Burundi kuhusu raia wa kuzaliwa mwenye hati ya bandia
 
Salaam Mkuu,

Nakuheshimu sana. Kipi kimekufanya uamini ni tapeli wa kimataifa?(Ushahidi). Je, Ushahidi gani mleta mada kaleta kuonyesha alifukuzwa Burundi?. Je, hizo picha zilizowekwa ni feki au sio feki? Kama alifukuzwa Burundi basi ni Mtanzania, hakuna nchi inafukuza raia wake kwa Utapeli, hata kama angekuwa mwizi wa kutumia Silaha. Angenyongwa au kufungwa maisha ila sio kufukuzwa.

Sikatai inawezekana alikuwa anamiliki passport feki ya Burundi ndo maana akafukuzwa. Katika utafutaji hiyo ipo.

Basi tuseme sio Mtanzani basi mpeni gari aondoke nalo.

Gari lake lilichukuliwa kama Malipo ya kukaa Tamzania bila Uraia ili Asisumbuliwe?
Asante kwa heshima yako kwangu ila nasema hivi hakuna sehemu nimesema jamaa ni tapeli but nafahamu uelewa wetu mdogo kwenye kufafanua maneno inasumbua watanzania wengi ukiwemo.

Ukisoma reply yangu kuna maneno mawili nimeyabold nikisema hivi; 'KAMA KWELI'
 
Umenena jambo la maana. Unajua inawezekana huyo jamaa anatumika na watu fulani fulani tu na yeye bila kujua kaingia choo cha aina aina yake. Hata mi naweza amka tu nikasema RC Gambo alinipora gari ni ngumu mno kujua ukweli kwa sababu inakuwaje ulikaa kimya muda wote huo??
Rc Gambo nae inabidi atubu. Aliumiza watu sana akihudumu kwenye nafasi hiyo
 
Kwa hiyo Warundi hawaruhusiwi kufanya biashara Tanzania, au wakifanya tunapaswa kuwanyang'anya magari yao?

Mbona unatoa mbofu mbofu sana>? Gari imeenda kwa Makonda bila kulipiwa, unasema huyu tapeli. Kama Makonda amekutuma mwambie hata kama Kamwele ni mrundi, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

Unatia kichefuchefu na ubaguzi wako. Hovyo kabisa wewe mtu. Utapeli wa Kamwele na ukoseshaji wa Makonda wa haki za kuishi za watu, upi mbaya zaidi? Na mwambie Makonda ashukuru urafiki wake na Samia ndio umemuokoa hadi sasa - lakini hata Samia anaogopa kumgusa, anavyonuka damu za Watanzania, na wala si Warundi..
Makonda kagunduanudhaifu wake wa uraia naye anataka atapeli. Ampe kwanza gari alaf utapeli wa kamwele uje baadae
 
Jiandae kuchafuliwa na Makonda & the gang.

Wamejipanga kila atakayedai haki lazima wamchafue
Hawezi kunipata kwani alijaribu kumtumia mkuu wa wilaya ya Kigamboni kutushumu wauza madawa ya kulevya ikashindikana na akahakikisha tunafufukuzwa Tanzania na sasa tuko ulaya tumeshitaki serikali ya Tanzania mahakama ya kimataifa
 
Kwa hiyo makonda na lemutuz walimnyang'anya Mali yake sababu hakuwa na proper documents za kuishi hapa nchini?? Walimnyang'anya Kwa niaba yetu watanzania wote? Unafikiri Kuna watu wangapi walimnyang'anywa mali zao na Hawa wakiwa na madaraka?? Unakumbuka sakata la tajiri wa Yanga na nyumba yake aliyonyang'anywa na makonda?? Yule pia sio mtanzania???

Kwa taarifa yako watu wengi wamenyang'anywa mali zao na watu kibabe sababu tu walikuwa na madaraka, Yani hata diwani, alikuwa na uwezo wa kutamani mali ya mtu na kuichukua. Na ni watanzania wamenyang'anywa mali zao wala sio warundi.

Mh. Rais tunakuomba fatilia hai za watu, watu wapewe na kurudishiwa Mali zao. Watu wameshindwa kuendesha maisha na kuchangia Pato la Taifa Kwa sababu ya unyang'anyi ambao ulifanywa na baadhi ya viongozi waandamizi wa chama na serikali
Kama unataka kujua dhulma ya Makonda na kundi lote la watu waliokuwa wanajifanya ni wapwa wa Magufuli Kigamboni ndio ilikuwa sehemu yao ya kudhulumu watu na kufukuza wawekezaji ambao hawakuwa Watanzania Mkuu wa Wilaya Sara Msafiri Kigamboni alifanya kazi kumbwa kudhulumu wawekezaji mbona yeye hajashughulikiwa
 
Back
Top Bottom