Sakata la Makinikia: Kuna aibu inatunyemelea

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,147
2,000
Hawa jamaa kweli watakuwa wametuibia lakini findings za kamati hizi kuhusu viwango vya madini na hasara tuliyopata, mimi binafsi zinanipa mashaka sana na ninaona tunaweza kuja kuumbuka hapo baadae.

Ni hivi,kama mchanga tu unaweza kuwa na madini ya thamani ya trilioni mpaka 380.9 kwa kiwango cha juu kwa miaka hiyo 19,ni wazi nchi zenye rasilimali madini duniani na zenye mikataba mizuri zingekuwa ni nchi tajiri sana katika huu ulimwngu.

Cha kujiuliza, kama hiyo ni thamani ya makinikia tu,madini yenyewe(matofali ya dhahabu) yatakuwa na thamani kiasi gani kwa miaka yote hiyo?

Alafu kingine cha kujiuliza ni kwanini findings za kamati hizi mbili za sasa na ile ya Jaji Bomani zitofautiane katika data za viwango vya madini tu lakini zifanane katika matokeo mengine ikiwemo na mapendekezo?Tukumbuke hata hadidu za rejea zimeonekana kufanana kwa maelezo ya Lissu aliyoyatoa Bungeni jana huku akiwa na ripoti ya Jaji Bomani mkononi.

Kubiwa ni kweli tumeibiwa lakini hivyo viwango vya madini vilivyotajwa katika hizo ripoti inabidi tujiulize mara mbili mbili kama kweli vina uhalisia na hali ya nchi zingine zenye migodi tena kutuzidi.

Hizi ripoti hawa mabwana wanaweza kuzitafsiri kama ni defamatory kwao na hivyo tunaweza kuwa sued for defamation japo wametubia unless tuthibitishe usahihi wa hivyo viwango vya madini.

Tutafakari na hii:
millard ayo on Twitter
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
34,860
2,000
Unajua tunaweza kujaa kiburi kwa kujion washindi lakini kama taarifa hizi zina utata,tunaweza kushitakiwa kwa kuchafua jina la hiyo kampuni.

Alafu unamtuhumu mtu hata ripoti yenyewe humpi sasa sijui tunaelewekaje!!
Na kinachofanyika sasa ni ccm kuwalaghai wananchi eti waandamane nchi nzima kumpongeza. Nashukuru Lissu katika hoja yake Bungeni ambayo mimi naiita "WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA" ameweka wazi sana kuwa hakuna jipya hapo.
Wenye akili na watambue.
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,147
2,000
Na kinachofanyika sasa ni ccm kuwalaghai wananchi eti waandamane nchi nzima kumpongeza. Nashukuru Lissu katika hoja yake Bungeni ambayo mimi naiita "WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA" ameweka wazi sana kuwa hakuna jipya hapo.
Wenye akili na watambue.
Kinachotafutwa hapa ni sifa za kisiasa na ndio maana wameanza kugeuza maneno kuwa wapinzani wanatetea wawekezaji.

Mbowe na Katibu Mkuu wa chama walipaswa walichukue hili jambo na chama kilitolee tamko kupitia mkutano wa waandishi wa habari na pia watoe press release kwenye vyombo vya habari kuelezea historia nzima ya wapinzani katika hii vita.
 
chinembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
5,541
2,000
Takwimu zimepikwa

Sasa wewe umeangalia makontena mwaka 2017,

Unaweka majumuisho ya jumla eti kwa kuwa 2017 tumekuta hasara hii,basi tuweke assumption kwamba ulikuwa unafanya hivyo kila Siku

Yaani kama umeiba ngombe mmoja mwaka 2017,basi tunasema kila mwaka ulikuwa unaiba ngombe mmoja,

Ushahidi wa kwamba makinikia ya mwaka 2016,2015,2014,2013,2012,2011,2010 mpaka 1998 jamaa walikuwa wanafanya kosa lilelile na kwa kiwango kilekile bila kukosea wala kuzidi wala kupungua,je tuna evidence za makontena ya mwaka 1998,1999,2000,2001,2002......mpaka 2016?

Nani alichukua sample za mwaka 1998?1999?2000?

Unatumia sample ya 2017 kutoa hukumu kwa suala la 1998,2010.....

Exchange rate zilikwaje?thamani ya Dhahabu ilikuwaje?

Tunafanyiwa usanii
 
chinembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
5,541
2,000
Kuna wakati kontena la makinikia lilizama bandarini, hao jamaa walitumia zaidi ya dollar milioni kumi kuliopoa.
Swali langu, kulikua na zahabu kiwango gani humo?
Sasa unadhani mamlaka ya bandari wangekubali uache kontena lako kwenye bandari likaharibu propela za meli?

Unajua gharama za kuharibu propela ya meli ? Au unadhani mamlaka ya bandari wangekubali uache kontena karibu na mahali meli zinapaki? Ili ziligonge zianguke?
 
Gatekalii

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
249
500

Unachotafuta utakipata
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,147
2,000
Takwimu zimepikwa

Sasa wewe umeangalia makontena mwaka 2017,

Unaweka majumuisho ya jumla eti kwa kuwa 2017 tumekuta hasara hii,basi tuweke assumption kwamba ulikuwa unafanya hivyo kila Siku

Yaani kama umeiba ngombe mmoja mwaka 2017,basi tunasema kila mwaka ulikuwa unaiba ngombe mmoja,

Ushahidi wa kwamba makinikia ya mwaka 2016,2015,2014,2013,2012,2011,2010 mpaka 1998 jamaa walikuwa wanafanya kosa lilelile na kwa kiwango kilekile bila kukosea wala kuzidi wala kupungua,je tuna evidence za makontena ya mwaka 1998,1999,2000,2001,2002......mpaka 2016?

Nani alichukua sample za mwaka 1998?1999?2000?

Unatumia sample ya 2017 kutoa hukumu kwa suala la 1998,2010.....

Exchange rate zilikwaje?thamani ya Dhahabu ilikuwaje?

Tunafanyiwa usanii
Mkuu,wacha tuone mwisho wa hili sakata.
 
MTENDAHAKI

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
4,009
2,000
Hawa jamaa kweli watakuwa wametuibia lakini findings za kamati hizi kuhusu viwango vya madini na hasara tuliyopata, mimi binafsi zinanipa mashaka sana na ninaona tunaweza kuja kuumbuka hapo baadae.

Ni hivi,kama mchanga tu unaweza kuwa na madini ya thamani ya trilioni mpaka 380.9 kwa kiwango cha juu kwa miaka hiyo 19,ni wazi nchi zenye rasilimali madini duniani na zenye mikataba mizuri zingekuwa ni nchi tajiri sana katika huu ulimwngu.

Cha kujiuliza, kama hiyo ni thamani ya makinikia tu,madini yenyewe(matofali ya dhahabu) yatakuwa na thamani kiasi gani kwa miaka yote hiyo?

Alafu kingine cha kujiuliza ni kwanini findings za kamati hizi mbili za sasa na ile ya Jaji Bomani zitofautiane katika data za viwango vya madini tu lakini zifanane katika matokeo mengine ikiwemo na mapendekezo?Tukumbuke hata hadidu za rejea zimeonekana kufanana kwa maelezo ya Lissu aliyoyatoa Bungeni jana huku akiwa na ripoti ya Jaji Bomani mkononi.

Kubiwa ni kweli tumeibiwa lakini hivyo viwango vya madini vilivyotajwa katika hizo ripoti inabidi tujiulize mara mbili mbili kama kweli vina uhalisia na hali ya nchi zingine zenye migodi tena kutuzidi.

Hizi ripoti hawa mabwana wanaweza kuzitafsiri kuwa ni defamatory na hivyo tunaweza kuwa suted for defamation japo wametubia unless tuthibitishe usahihi wa hivyo viwango vya madini.
Acha uzuzu wa kiwango cha standard gauge! Nani hajui kwamba hiyo siyo halisi!?Tunajua kwamba hicho sio kiwango halisi, lakini matokeo ya kamati kutoka kwny makontena 40 kati ya 270 yaliyofunguliwa hayana shaka! Na katika utafiti majibu ya sampuli uliyochagua ndio kila kitu!Kifupi ni kwamba hata ikirudiwa mara 10 sampuli hiyo itatoa majibu hayohayo! ACACIA wanajua wameshikwa, ila wanajua huu mchezo hawakuwa wanaufanya kwenye kila makontena so, watajaribu kufurukuta hata wapewe nafasi ya kwenda kupima makontena yaliyoko mgodini (they will never get it)!cheating is cheating na msemo wa kikwetu za mwizi 40!Hivi unadhani wezi wote huiba mara 40?
 
Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,212
2,000
Naona wapuuzi mnajipa moyo kwa ujinga wenu wa kutofikiria, sasa kama mna mashaka kwa nini msiunde tume yenu ifanye uchunguzi?

Yaan Tume idanganye? ili iweje labda? au mnadhani akina Prof. Mruma na Prof. Ossoro ni wendawazimu? kwamba washushe reputation zao na vyuo vyao wanavyofundisha?
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
186,748
2,000
Hawa jamaa kweli watakuwa wametuibia lakini findings za kamati hizi kuhusu viwango vya madini na hasara tuliyopata, mimi binafsi zinanipa mashaka sana na ninaona tunaweza kuja kuumbuka hapo baadae.

Ni hivi,kama mchanga tu unaweza kuwa na madini ya thamani ya trilioni mpaka 380.9 kwa kiwango cha juu kwa miaka hiyo 19,ni wazi nchi zenye rasilimali madini duniani na zenye mikataba mizuri zingekuwa ni nchi tajiri sana katika huu ulimwngu.

Cha kujiuliza, kama hiyo ni thamani ya makinikia tu,madini yenyewe(matofali ya dhahabu) yatakuwa na thamani kiasi gani kwa miaka yote hiyo?

Alafu kingine cha kujiuliza ni kwanini findings za kamati hizi mbili za sasa na ile ya Jaji Bomani zitofautiane katika data za viwango vya madini tu lakini zifanane katika matokeo mengine ikiwemo na mapendekezo?Tukumbuke hata hadidu za rejea zimeonekana kufanana kwa maelezo ya Lissu aliyoyatoa Bungeni jana huku akiwa na ripoti ya Jaji Bomani mkononi.

Kubiwa ni kweli tumeibiwa lakini hivyo viwango vya madini vilivyotajwa katika hizo ripoti inabidi tujiulize mara mbili mbili kama kweli vina uhalisia na hali ya nchi zingine zenye migodi tena kutuzidi.

Hizi ripoti hawa mabwana wanaweza kuzitafsiri kama ni defamatory kwao na hivyo tunaweza kuwa sued for defamation japo wametubia unless tuthibitishe usahihi wa hivyo viwango vya madini.
Kwa hesabu za Acacia, ili tuwadai matrilioni hayo inabidi wao wamechuma mazilioni na kuwa wachimbaji wakubwa dunian
 
morenja

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
4,340
2,000
Kuna wakati kontena la makinikia lilizama bandarini, hao jamaa walitumia zaidi ya dollar milioni kumi kuliopoa.
Swali langu, kulikua na zahabu kiwango gani humo?
Weee nae dollar milioni kumi walikuwa wanajenga bandari au crane ya kunyanyulia hilo container
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
30,759
2,000
Hawa jamaa kweli watakuwa wametuibia lakini findings za kamati hizi kuhusu viwango vya madini na hasara tuliyopata, mimi binafsi zinanipa mashaka sana na ninaona tunaweza kuja kuumbuka hapo baadae.

Ni hivi,kama mchanga tu unaweza kuwa na madini ya thamani ya trilioni mpaka 380.9 kwa kiwango cha juu kwa miaka hiyo 19,ni wazi nchi zenye rasilimali madini duniani na zenye mikataba mizuri zingekuwa ni nchi tajiri sana katika huu ulimwngu.

Cha kujiuliza, kama hiyo ni thamani ya makinikia tu,madini yenyewe(matofali ya dhahabu) yatakuwa na thamani kiasi gani kwa miaka yote hiyo?

Alafu kingine cha kujiuliza ni kwanini findings za kamati hizi mbili za sasa na ile ya Jaji Bomani zitofautiane katika data za viwango vya madini tu lakini zifanane katika matokeo mengine ikiwemo na mapendekezo?Tukumbuke hata hadidu za rejea zimeonekana kufanana kwa maelezo ya Lissu aliyoyatoa Bungeni jana huku akiwa na ripoti ya Jaji Bomani mkononi.

Kubiwa ni kweli tumeibiwa lakini hivyo viwango vya madini vilivyotajwa katika hizo ripoti inabidi tujiulize mara mbili mbili kama kweli vina uhalisia na hali ya nchi zingine zenye migodi tena kutuzidi.

Hizi ripoti hawa mabwana wanaweza kuzitafsiri kama ni defamatory kwao na hivyo tunaweza kuwa sued for defamation japo wametubia unless tuthibitishe usahihi wa hivyo viwango vya madini.
Unalinganisha kamati ya Bomani iliochukua data kutoka kwenye makaratasi yaliyoandaliwa na GST halafu unalinganisha na kamati iliyofanya sampling katika Makontena yaliyodakwa?

Nadhani utakuwa ni muhitimu wa Chuo cha kata.

Pili unaongeleaje uwepo wa Bi kejo ndosi ndani ya kamati ile?

Tatu Kamati ya Bomani iliongelea madini nyeti kama Rhadium??

Wasaliti wakubwa mnaohangaika na simu usiku wa manane kwa kuhongwa na Acacia
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom