isale lo njofu
Member
- Jun 13, 2017
- 87
- 30
Ni kweli kuwa wananchi wengi wanapotoshwa kuhusu dhana nzima ya vyama vya upinzani. Wanalishwa imani potofu na chuki dhidi ya vyama vya upinzani. Ukweli no kuwa vyama vya upinzani vina majukumu ya kutoa mawazo mbadala kwenye masuala nyeti na upinzani wamekuwa wakifanya hayo kwa ueledi mkubwa. Kwa hiyo upinzani ujipange kuzima hizi propaganda chafu dhidi ya vyama vya upinzani.Kinachotafutwa hapa ni sifa za kisiasa na ndio maana wameanza kugeuza maneno kuwa wapinzani wanatetea wawekezaji.
Mbowe na Katibu Mkuu wa chama walipaswa walichukue hili jambo na chama kilitolee tamko kupitia mkutano wa waandishi wa habari na pia watoe press release kwenye vyombo vya habari kuelezea historia nzima ya wapinzani katika hii vita.