Wapinzani wamekuwa wakilalamika na kuona wanaonewa katika kila jambo linalotokea kwao. Inawezekana ni kweli mke wake alikuwa na changamoto, je ni mwanamke huyo tu mwenye changamoto za uzazi? Hivi kama kila mwanaume ataamua kukaa nyumbani kulea mimba ya mke wake kwa miezi tisa kazi zitafanyika kweli? Wakati mwingine tuwe serious bhana, Joshua hapa amechemka.
Japo naona baadhi ya viongozi wake wamejaribu kukubeba na kukutetea, lakini kiuhalisia kukutetea kwenye hili inabidi uwe umekunywa gongo kidogo. Lissu nae ameamua hadi kutoa ujumbe wa uongo kwamba Nassari alimpigia kuomba ushauri na akamwambia vikao vya Novemba alikuwepo lakini kwenye press umesema Novemba ni kweli hakuwepo. JE,
1. Ni kwa nini alikataa kuulizwa maswali na waandishi wa habari ambao amewaita yeye mwenyewe?
2. Ni kwamba viongozi wake wanakurupuka hasa Lissu?
3. Ameona ni njia bora ya kuhama chama bila kuzomewa na kuitwa msaliti?
4. Viongozi wake wamewahi kumuonya juu ya utoro wake Bungeni?
5. Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni kupitia kwa mnadhimu hawakuwa na taarifa juu ya dharura alizokuwa nazo Mbunge wao?
6. Barua anayodai ametuma kwa Spika, kwa nini haikupita kwenye ofisi ya Kambi rasmi ya Upinzani?