Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,348
- 26,144
Ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari umesitishwa/umefutwa katika kile kinachotajwa kuwa hakuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ruhusa ya Spika wa Bunge. Katika kutekeleza hilo, Ofisi ya Spika imeijenga hoja yake kwa kutumia Ibara ya 71(1)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kwa mara)ambayo nainakili hapa chini:
71.-(1) Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo-
(a).……………………………….(haihusiki)
(b).……………………………….(haihusiki)
(c) ikiwa Mbunge atakosa kuhudhuria vikao vya Mikutano ya Bunge Mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika;
Ni dhahiri kuwa Ibara niliyoinakili hapo juu inazungumzia sababu mojawapo ya kukoma kwa Ubunge wa Mbunge yeyote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.ababu hiyo ni kukosa kuhudhuria vikao vya Mikutano ya Bunge Mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika. Kulingana na Ibara hiyo, kuna mambo muhimu.
Mosi, Mbunge husika anakosa kuhudhuria vikao vya Mikutano ya Bunge mitatu mfululizo. Kulingana na sakata la Nassari, Nassari hakuhudhuria vikao vya Mikutano ya Bunge mitatu mfululizo. Ni jukumu lake Nassari nje au ndani ya Mahakama kuthibitisha kuwa alihudhuria vikao vya mikutano hiyo ya Bunge ambayo anadaiwa kuwa hakuihudhuria. Katika hilo, hakutakiwi porojo wala siasa, ushahidi unatosha.
Pili, Ibara tajwa inazungumzia ruhusa ya Spika. Ruhusa ni kibali cha kufanya au kutofanya au kusema au kutosema jambo. Katika uga wa kiutumishi, ruhusa huombwa kwa fomu au barua maalum. Mwombaji wa ruhusa huhakikisha kuwa fomu au barua yake imemfikia ipasavyo mtoa ruhusa na hatimaye amepata ruhusa hiyo kupitia fomu hiyo au barua ya mtoa-ruhusa. Hapo ndipo ruhusa ya kufanya au kutofanya au kusema au kutosema huanza.
Tatu, kwa mujibu wa Ibara niliyoinakili hapo juu na sakata zima la Joshua Nassari, mtoa-ruhusa ni Spika wa Bunge. Ni ruhusa ya kutohudhuria vikao vya mikutano ya Bunge ima chini ya mitatu au mitatu. Joshua Nassari, kwa mujibu wa jambo lake, alipaswa kuomba na kupata ruhusa ya Spika wa Bunge ili kutohudhuria vikao vya Mikutano mitatu mfululizo ya Bunge. Kama aliipata ruhusa hiyo, ni wakati wake nje au ndani ya mahakama kuianika ruhusa hiyo. Kulialia na kuomba huruma kutafuata baadaye.
Kwa uelewa wangu, neno 'mfululizo' limetumika kuonyesha ukubwa wa jambo hilo la kukosa kuhudhuria vikao vya mikutano ya Bunge kwakuwa Miukutano ya Bunge hufanyika kila baada ya miezi kadhaa. Kimsingi, mikutano mitatu mfululizo hubeba kipindi kirefu cha kutosha na ndiyo maana Mbunge anapokosa bila ruhusa ya Spika anapaswa kukoma kuwa Mbunge. Joshua Nassari, pamoja na kuiweka mbele hoja ya kumuuguza mkewe, anapaswa kuuambia umma, wapigakura wake na hata Mahakama (kama atakwenda) kuhusu ruhusa yake kutoka kwa Spika.
Kwakuwa suala la Joshua Nassari ni suala nyeti na linaloweza kujengewa nadharia mbalimbali sahihi na potofu, ni wajibu wake kuweka mambo sawa kwa kuanika ruhusa yake kutoka kwa Spika au ushahidi wake kuwa si kweli kuwa hakuhudhuria vikao vya mikutano mitatu mfululizo ya Bunge.Amasivyo, Katiba, Sheria, Kanuni na Taratibu za Bunge zitampiga kumbo kirahisi sana.