Kama unasafirisha mzigo haramu kwa gari; make sure gari yako haina tatizo lolote; kuanzia la kiufundi hadi kiutawala kv insurance n.k! Unapokuwa kwenye usukani, make sure unakuwa dereva mtiifu kuliko madereva wote duniani... yote hayo, unayafanya kukwepa kukutana na mkono wa dola kwa sababu yoyote ile! Kosa la kumpiga pasi tu mwenzako, litapelekea kukaguliwa kwa leseni yako! Kukaguliwa kwa leseni yako tu kutasababisha kupitiwa kwa nyaraka zako zingine na kuwafanya wengine watake kuchungulia hadi ndani kuna nini! Kitakachoonekana ndani ya gari ndich kitakachowafanya wao wapate hamu ya kwenda kukupekua nyumbani kwako... hebu ona sasa... kosa ni la kumpiga pasi dereva mshenzi na mtukutu wa bajaji lakini kosa hilo hilo limesababisha kwenda kupekuliwa nyumbani kwako! Itoshe tu kuseama kwamba, one event generate another... na kama alivyosema mshana jr, haya mambo sometime watu wanakuwa wanakulia mingle uingie kwenye 18 zao! Ni kama mwanaume aliyepata taarifa za mkewe kumegwa... si kwamba hawezi kwenda kumteka mbaya wake na kumfanyia kitu mbaya, la hasha; bali atakausha kama hafahamu lolote kumbe ankulia mingle uingie kwenye 18 zake!Wanasheria watusaidie katika hili ni halali kwa polisi kudai nyaraka zote hizo kwa kosa analoshitakiwa nalo, maana tunaambiwa ni mwananchi mmoja ndo amemshitaki Gwajima kwa kuwa kakerwa na maneno aliyotumia dhidi ya Askofu Pengo.
But all in all, probably even much better than above all, huwezi kumwambia polisi "hey, kosa langu nimekojoa barabarani, how come unataka ukanipekue nyumbani...!" "Geshi" limeona umuhimu huo... inawezekana una ugonjwa wa akili kwahiyo inabidi wakakupekue wapate ushahidi wa vyeti au angalau dawa za magonjwa ya akili ili wakipata ushahidi, wakurudishe Mirembe usije ukahatarisha usalama wa raia, otherwise kwanini mtu mzima akojoe barabarani!!!!
Polisi hakosi genuine cause! Na asikudanganye mtu kwamba eti polisi wanapenda kubambikia watu makosa! Polisi anakubambikia kosa ukiingia kwenye 18 zake... na wakiamua "kubambikia" watu makosa, wote sisi tutalala central tena kwa makosa tuliyofanya kabisa!!!