EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,347
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mb) akizungumza katika kipindi cha Nipashe cha Radio One Stereo, amesema anawaeleza Watanzania kuwa, uchumi wa Dunia wa sasa ni wa ushindaji, hivyo "sisi" Watanzania tumetaka tuifanye Bandari ya Mtwara kituo kikuu cha utafiti na uendeshaji wa shughuli zote za gesi. Kwa hivyo, wawekezaji waliotaka kuwekeza wakiondoka, bandari ya Mtwara kutokana na sababu zozote za kushindwa utulivu wa kufanya kazi zao, watahamishia shughuli zao bandari za Beira au Mombasa.
Mwandishi: Tatizo la wakazi wa Mtwara ni lipi?
Waziri: Mimi sielewi, inabidi wao waulizwe. Watu wa Mtwara kitu walicho nacho haki ni Korosho... Hizo korosho ni mali zao kabisa, mbona hizo korosho zinasafirishwa? Watanzania tuwaulize kwa nini korosho zao zinasafirishwa kutoka Mtwara.
Mwandishi: Huoni vyema nyie Serikali mkakaa na wananchi kutoa elimu kuhusiana na suala la gesi?
Waziri: Serikali na TPDC tumefanya vikao vingi sana na viongozi wa Mtwara na Lindi... wakiwemo Wabunge wao hadi wale wa Halmashauri wamepelekwa nje ya nchi kujifunza umuhimu unaotokana na hiyo gesi asilia.
Isitoshe, wananchi wa Lindi na Mtwara wamepunguziwa bei ya umeme... Je, wanavyounganishiwa huo umeme kwa bei nafuu kuliko wananchi wengine, hawajiulizi? Pili, vijana wao tumewachukua wanakwenda kusoma VETA...
Mwandishi: Upi ni wito wako kuhusiana na vurugu, migororo?
Waziri: Kwanza naomba kuwaambia wananchi wa Mtwara, kuwa wasicheze ngoma wasiyoijua. Wasiimbe nyimbo wasizozijua wala hawajui wanaotunga tenzi za nyimbo hizo.
Pili, Watanzania wote kwa miaka mingi tumepata matatizo ya umeme, suluhisho la umeme linapatikana sasa.
Shukrani za dhati ziende kwa wavuti.com kwa kuyaweka hayo mahojiano kwenye maandishi. Unaweza kumskiliza Mh. Muhongo mwenywe hapa: audio:-Kauli ya Waziri wa Nishati na Madini & Taarifa za habari Januari 27, 2013 - wavuti.com