Sakata la Corona limetuonyesha Rais tuliye naye watanzania ni wa aina gani

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Na Emmanuel J. Shilatu

Wakati mgumu wa janga la ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya Corona vimetuonyesha aina ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tuliyenae Watanzania aitwaye Dkt. John Pombe Magufuli (JPM).

Tumemshuhudia JPM akisitisha sherehe zote za kuwasha Mwenge, sherehe ya Muungano na sherehe ya Wafanyakazi na kuelekeza fedha hizo ziende kupambana na janga la Corona. Hapa JPM aliweka pembeni anasa na mazoea yote na kuelekeza fedha ziende kupambana kulinda uhai wa Watanzania kama alivyoapa kiapo cha kulinda uhai na usalama wa Raia wake, JPM ametimiza hili.

Tumemuona JPM akiwa na msimamo mkali wa kutokufungia Raia wake ndani hali iliyopelekea mataifa mengine kumbeza. Leo hii wale wale waliombeza ndio hao hao wanaiga msimamo wa JPM na kuanza kuwafungulia Raia wao. JPM ameifanya Tanzania kuwa nchi ya mfano Duniani kiuongozi.

Mwamba JPM akaendelea kuwaonyesha Mabeberu juu ya msimamo na ujasiri wake kwa kukataa mikopo kipindi hiki na badala yake watusamehe madeni tofauti na nchi nyingine ambazo wamekopa mikopo hiyo. Huu ni msimamo, ujasiri na uzalendo wa Rais Magufuli kwa nchi yake.

Ni JPM huyu huyu shujaa aliwasihi Watanzania kutokubali misaada ya kukabiliana na Corona toka nchi nyingine kipindi hiki kwani mingine inawezekana isiwe salama; JPM hakubweteka na vipimo vya Corona akavifanyia utafiti na kubaini vina kasoro, jambo lililozua gumzo Duniani. Huu ni ushahidi wa uchapa kazi usiku na mchana alionao JPM na Serikali yake kwa maslahi mapana ya Watanzania.

Ni Rais Magufuli amefanikiwa kuwaunganisha Watanzania kumtegemea Mwenyezi Mungu pekee kutuokoa na janga la ugonjwa wa Covid 19 ambapo alitenga siku 3 za maombezi. Huyo ndio JPM Mcha Mungu na Mzalendo kwa Taifa lake.

Sakata la Corona limetuonyesha Dkt. Magufuli sio tu Rais wa nchi bali ni Baba anayeipenda familia yake (Tanzania) kupitia Uzalendo, ujasiri, ucha Mungu, uadilifu, ufuatiliaji na uchapa kazi.

*Shilatu E.J*

FB_IMG_1589198198223.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NAMBO POYU KEZA MBOCHI TOCHA?? YEYE SI RIDAMEJE?

#Nataka kuvunja KIJIKO ili nijue NGUVU YA UMA.
 
Hapo ninamuona mwimba mapambio tuu huku taifa laenda kombo.

Anaemsifu 'Jemedari' aliyejificha UVUNGUNI ili asiwaone raia wake wanaopigana vita kali na wala asijue kama waweza kuwa wameanza kuelemewa.

'Jemedari' ambae,anakimbilia kujikosha kwa kuokoteza vijisababu ili kutukana vifaa na wataalamu wake wanaohatarisha maisha yao mstari wa mbele ili kuokoa nchi yao.

'Jemedari' aliyejaa visingizio na kuamini anajua kuliko hata wenye utaalamu.

Kama kwako na wa aina yenu, huo ndio ujasiri, uzalendo na ucha Mungu, basi ni dhahiri kuwa vita ya corona tumeshashindwa tusubiri kuokolewa TU na hao hao ambao sasa tunawaita mabeberu Amen
 
Makala nzuri sana ila haina wachangiaji ,wengi waliomo humu ni mercenaries,wanapenda za kumdhihaki ,kukejeri na kumponda,ingekua hiyo saa hizi replies zingekuwa mia mbili na kuendelea,wakigonga cheers
 
Na Emmanuel J. Shilatu

Wakati mgumu wa janga la ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya Corona vimetuonyesha aina ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tuliyenae Watanzania aitwaye Dkt. John Pombe Magufuli (JPM).

Tumemshuhudia JPM akisitisha sherehe zote za kuwasha Mwenge, sherehe ya Muungano na sherehe ya Wafanyakazi na kuelekeza fedha hizo ziende kupambana na janga la Corona. Hapa JPM aliweka pembeni anasa na mazoea yote na kuelekeza fedha ziende kupambana kulinda uhai wa Watanzania kama alivyoapa kiapo cha kulinda uhai na usalama wa Raia wake, JPM ametimiza hili.

Tumemuona JPM akiwa na msimamo mkali wa kutokufungia Raia wake ndani hali iliyopelekea mataifa mengine kumbeza. Leo hii wale wale waliombeza ndio hao hao wanaiga msimamo wa JPM na kuanza kuwafungulia Raia wao. JPM ameifanya Tanzania kuwa nchi ya mfano Duniani kiuongozi.

Mwamba JPM akaendelea kuwaonyesha Mabeberu juu ya msimamo na ujasiri wake kwa kukataa mikopo kipindi hiki na badala yake watusamehe madeni tofauti na nchi nyingine ambazo wamekopa mikopo hiyo. Huu ni msimamo, ujasiri na uzalendo wa Rais Magufuli kwa nchi yake.

Ni JPM huyu huyu shujaa aliwasihi Watanzania kutokubali misaada ya kukabiliana na Corona toka nchi nyingine kipindi hiki kwani mingine inawezekana isiwe salama; JPM hakubweteka na vipimo vya Corona akavifanyia utafiti na kubaini vina kasoro, jambo lililozua gumzo Duniani. Huu ni ushahidi wa uchapa kazi usiku na mchana alionao JPM na Serikali yake kwa maslahi mapana ya Watanzania.

Ni Rais Magufuli amefanikiwa kuwaunganisha Watanzania kumtegemea Mwenyezi Mungu pekee kutuokoa na janga la ugonjwa wa Covid 19 ambapo alitenga siku 3 za maombezi. Huyo ndio JPM Mcha Mungu na Mzalendo kwa Taifa lake.

Sakata la Corona limetuonyesha Dkt. Magufuli sio tu Rais wa nchi bali ni Baba anayeipenda familia yake (Tanzania) kupitia Uzalendo, ujasiri, ucha Mungu, uadilifu, ufuatiliaji na uchapa kazi.

*Shilatu E.J*

View attachment 1447059

Sent using Jamii Forums mobile app
IMG_20200511_162755.jpg
 
Hili tukio la mkuu wa nchi kukimbizwa kwenda kijijini ni kutangaza kuwa kuna gonjwa la hatari sana.

Tukio la kukimbia toka mjini kutokana na gonjwa ni marudio katika historia ya binadamu katika harakati ya kujiokoa.

Katika muhadhara wa public health katika chuo Kikuu maarufu cha Yale, Prof. Snowden anasimulia.

Hivyo tulioachwa mijini tukio hili tusilichukulie kwa urahisi bali ni ujumbe tosha tuchukue tahadhari kwani mkuu wa nchi ameshauriwa ahame kwa muda toka Dar es Salaam na Dodoma ktk mawe kwani kuna hatari kubwa ya gonjwa hili hatari.

00:00 - Chapter 1. Responses to the Plague and Miasmatism 09:05 - Chapter 2. Individual Measures of Self-Protection and Scape-Goating 18:52 - Chapter 3. Religiosity 25:51 - Chapter 4. Organized Public Health Measures 37:25 - Chapter 5. Did the Public Health Measures Succeed?
Source: Yalecourse
 
Ndo hapo sasa kuna watu humu naona wana bwabwaja tu maneno hawana lolote jipya,Madhara ya korona hapa jamii forum ni makubwa saba kuliko huku mitaani tulipo.

Kabisa mkuu kama hayajakukuta. Ila kwa ambao tayari wameshapoteza wapendwa wao kwa haka kaupepo sidhani kama watakubaliana na wewe.

Tusisubirie kuumia hadi pale mkuki wa nguruwe inapokuwa tumetelekezewa sisi?

Au wewe waonaje mkuu?
 
Back
Top Bottom