Sakata la CAG: Tafakuri ya Askofu Bagonza

Sakata la CAG: Tafakuri ya Askofu Bagonza

Akili kubwa,inayo utendea umma haki katika utumishi wa kiroho.Naam!namuombea utumishi mwema na Mungu aendelee kumuongoza na kumpa ujasiri wa kiroho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa namn hii ccm wanatumbukiza nchi shimoni.Baba Bagonza tunamba maombi yako kwa taifa hili.Kila nikiangalia naona giza.Nchi hii Mungu ashailaani.Mali zote zinaliwa na wajanja raia wanajifanya wajanja kumbe ni umbumbumbu.Wameamua kukaa kimya na kucheka ndio kufuta machozi yao.wametupa maarifa na kuona kama takataka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani hawataki kufanya Kazi na Assad,ila watafanya kazi na ofisi ya sieiji
 
Nafikiri watamtisha ili atangaze kujiuzuru. Akiiiuzuru nia zao ovu zitatimia kwa mchakato mfupi sana

Akibisha wanaua. Ccm siyo ya mchezo
 
The weakest Parliament.
The weakest Leader of Parliament.
The weakest Members of Parliament from CCM Party.

The strongest CAG.

May Almight God bless our Archbishop Dr. Bagonza .

Sent using Jamii Forums mobile app

Bishop -Askofu
Archbishop -Askofu mkuu

Askofu ni mtumishi na kiongozi wa kanisa katika level ya jimbo katika makanisa ya roma au makanisa yanayoendana kiutawala na RC
Archbishop ni mtumishi na kiongozi wa kanisa katika level ya jimbo lakini akiwa muangalizi wa majimbo mengine yaliyochini ya utawala wa jimbo kuu. Mfano Askofu pengo ni Archbishop lakini Askofu Mkude wa Morogoro ni bishop.
 
Ameandika Askofu Benson Bagonza (PhD)

YAMETOKEA, Itakuwaje sasa?

Kuna maswali magumu mbele yetu baada ya Bunge kupitisha uamuzi wa kihistoria tarehe 2 Aprili 2019.

1. Je, Bunge limepitisha azimio la kutofanya kazi na Prof. Assad au na CAG?

2. Kama ni Prof Assad, basi Bunge bado linaweza kufanya kazi na CAG Assad.

3. Kama Bunge halitafanya kazi na CAG, linamuingiza Rais ktk mgogoro mkubwa wa Kikatiba, kwa sababu:

- Ndani ya siku 7 tangu kupokea Ripoti ya CAG, Rais anatakiwa kuipeleka Ripoti Bungeni iliyofanywa Kazi na CAG ambaye ni Prof. Assad.

4. Asipoileta atakuwa amevunja Katiba ya Nchi aliyoapa kuilinda.

5. Akiileta, atakuwa amelidharau Bunge wakati naye ni sehemu ya Bunge.

6. Akiteua CAG mwingine, huyo mpya hatakagua upya bali ataleta iliyokaguliwa na CAG Prof. Assad ambaye hatakiwi Bungeni.

7. Katiba inatamka kuwa; mchakato wa kumuondoa CAG ni mrefu na iko kimya kuhusu kuendesha mchakato wakati kuna Kaimu CAG.

Ukiwahi kuzaliwa unaona mengi. Ukiwahi kufa unakosa mengi.

Dumisha Uhuru na Umoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwanazuoni huyu... Aliyesoma na kuelimika..... Hakusoma ili afaulu mitihani na kupata madaraja

Jr[emoji769]
 
Ameandika Askofu Benson Bagonza (PhD)

YAMETOKEA, Itakuwaje sasa?

Kuna maswali magumu mbele yetu baada ya Bunge kupitisha uamuzi wa kihistoria tarehe 2 Aprili 2019.

1. Je, Bunge limepitisha azimio la kutofanya kazi na Prof. Assad au na CAG?

2. Kama ni Prof Assad, basi Bunge bado linaweza kufanya kazi na CAG Assad.

3. Kama Bunge halitafanya kazi na CAG, linamuingiza Rais ktk mgogoro mkubwa wa Kikatiba, kwa sababu:

- Ndani ya siku 7 tangu kupokea Ripoti ya CAG, Rais anatakiwa kuipeleka Ripoti Bungeni iliyofanywa Kazi na CAG ambaye ni Prof. Assad.

4. Asipoileta atakuwa amevunja Katiba ya Nchi aliyoapa kuilinda.

5. Akiileta, atakuwa amelidharau Bunge wakati naye ni sehemu ya Bunge.

6. Akiteua CAG mwingine, huyo mpya hatakagua upya bali ataleta iliyokaguliwa na CAG Prof. Assad ambaye hatakiwi Bungeni.

7. Katiba inatamka kuwa; mchakato wa kumuondoa CAG ni mrefu na iko kimya kuhusu kuendesha mchakato wakati kuna Kaimu CAG.

Ukiwahi kuzaliwa unaona mengi. Ukiwahi kufa unakosa mengi.

Dumisha Uhuru na Umoja.

Sent using Jamii Forums mobile app

Bunge DHAIFU.
 
Back
Top Bottom