Sakata la CAG: Tafakuri ya Askofu Bagonza

Sakata la CAG: Tafakuri ya Askofu Bagonza

Rais hawezi kuteua CAG mwingine wakati huyu aliyepo bado yupo kazini. Ofisi ya CAG imeundwa kiKatiba kama vile Bunge. Ili kumwondoa CAG itabidi kuunda tume ya Majaji, itakayoangalia kama alikiuka Sheria na maadili ya ofisi ya CAG. Kwa kifupi huyu Assad hangoleki kirahisi rahisi hivyo.
Ameandika Askofu Benson Bagonza (PhD)

YAMETOKEA, Itakuwaje sasa?

Kuna maswali magumu mbele yetu baada ya Bunge kupitisha uamuzi wa kihistoria tarehe 2 Aprili 2019.

1. Je, Bunge limepitisha azimio la kutofanya kazi na Prof. Assad au na CAG?

2. Kama ni Prof Assad, basi Bunge bado linaweza kufanya kazi na CAG Assad.

3. Kama Bunge halitafanya kazi na CAG, linamuingiza Rais ktk mgogoro mkubwa wa Kikatiba, kwa sababu:

- Ndani ya siku 7 tangu kupokea Ripoti ya CAG, Rais anatakiwa kuipeleka Ripoti Bungeni iliyofanywa Kazi na CAG ambaye ni Prof. Assad.

4. Asipoileta atakuwa amevunja Katiba ya Nchi aliyoapa kuilinda.

5. Akiileta, atakuwa amelidharau Bunge wakati naye ni sehemu ya Bunge.

6. Akiteua CAG mwingine, huyo mpya hatakagua upya bali ataleta iliyokaguliwa na CAG Prof. Assad ambaye hatakiwi Bungeni.

7. Katiba inatamka kuwa; mchakato wa kumuondoa CAG ni mrefu na iko kimya kuhusu kuendesha mchakato wakati kuna Kaimu CAG.

Ukiwahi kuzaliwa unaona mengi. Ukiwahi kufa unakosa mengi.

Dumisha Uhuru na Umoja.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Speaker ametumia kamati ya bunge kumtia hatiani CAG,na bunge limetumika kummaliza kabisa.
Ni wazi CAG amejichimbia mkwala na kuzikwa akiwa hai.
Kwa bunge mchezo umekwisha,wataletewa CAG mwingine.
Misaada aliyokuwa anaomba na kupewa na Speaker,imemtokea pabaya Raisi Magu.
Ilii kuprove kuwa siyo dhaifu Speaker Ndugai amegeuka kuwa mbogo,na sidhani kama Raisi Magu ana ushawishi wa kuzima hasira za Speaker Ndugai.
Speaker Ndugai ana historia akishafika boiling point harudi nyuma.kumbuka alivyompiga yule daktari hadi akazimia wakati wakiwania ubunge kwa tiketi ya CCM jimboni kwao.
CAG jiandae kupewa Ubalozi Zambia.

Kwahiyo unataka kusema Ndungai ni Untouchable?
 
Kwani aliyedharau bunge ni CAG au Assad?
Ofisi ya CAG haikuwahi kutoa ripoti ya kuwa bunge ni "dhaifu" ila Assad baada ya kukaa kwenye kiyoyozi akabwatuka kuwa bunge ni dhaifu.
Bunge linataka CAG Mwingine na sio huyu anayeliita bunge dhaifu kwa kutumia "akili" zake badala ya evidence kama taaluma yake inavyomtaka.

Mfano:
Askofu Bangoza anaropoka mambo ya kisiasa kama Bangoza na sio hiko cheo cha uaskofu.
Kweli nimeamini kuwa wewe ni "jingalao" kama avatar yako inavyo reflect.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri watamtisha ili atangaze kujiuzuru. Akiiiuzuru nia zao ovu zitatimia kwa mchakato mfupi sana

Akibisha wanaua. Ccm siyo ya mchezo
Watafunga baadhi ya mitaa wafanye party na vinywaji vya nusu bei[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkasa huu wa bunge kususa kufanya kazi na CAG
unanifanya nikumbuke msemo usemao " Ukiwa mwongo jitahidi uwe na kumbukumbu"
Wabunge hawa hawa wamekuwa wakiwananga kambi ya upinzani
kususia mijadala mbalimbali ya kupitisha sharia ambazo walikuwa hawakubaliani nazo.
sasa bunge hili hili linapitisha kususia kufanya kazi na CAG?
Najiuliza ni kwa manufaa au hasara ya nani? Sisi wapiga kura tunanufaikaje?

CAG ni mkaguzi Wa hesabu za serikali anayelisaidia taifa kuhakiki hesabu
za serikali kama fedha za mlipakodi zinatumika ipasavyo,
wabunge ambao ni wawakilishi wetu sisi walipakodi
wanasusa kufanyakazi na CAG,si kwa ubaya wa ripoti zake
bali kwa CAG kuwaambia ambalo sisi walipakodi tungewaambia
pindi wakirudi kutuomba kura.Hii si sawa.
Natoa rai kwamba wabunge watuombe samahani sisi wapiga kura
kwa sababu sisi hatukuwatuma bungeni wasusie mambo yenye tija kwetu.
 
Kwani aliyedharau bunge ni CAG au Assad?
Ofisi ya CAG haikuwahi kutoa ripoti ya kuwa bunge ni "dhaifu" ila Assad baada ya kukaa kwenye kiyoyozi akabwatuka kuwa bunge ni dhaifu.
Bunge linataka CAG Mwingine na sio huyu anayeliita bunge dhaifu kwa kutumia "akili" zake badala ya evidence kama taaluma yake inavyomtaka.

Mfano:
Askofu Bangoza anaropoka mambo ya kisiasa kama Bangoza na sio hiko cheo cha uaskofu.

Sasa Bunge limesusa kufanya Kazi Na Mussa Assad Au Na Ofisi ya NAO?
 
Kwani aliyedharau bunge ni CAG au Assad?
Ofisi ya CAG haikuwahi kutoa ripoti ya kuwa bunge ni "dhaifu" ila Assad baada ya kukaa kwenye kiyoyozi akabwatuka kuwa bunge ni dhaifu.
Bunge linataka CAG Mwingine na sio huyu anayeliita bunge dhaifu kwa kutumia "akili" zake badala ya evidence kama taaluma yake inavyomtaka.

Mfano:
Askofu Bangoza anaropoka mambo ya kisiasa kama Bangoza na sio hiko cheo cha uaskofu.
Hizi ndizo akili za kiccm zilizojazana bungeni kuhukum kwa wasema kweli, Huku wakishindwa kuisimamia serikali kwa madudu yake.
 
Kwani aliyedharau bunge ni CAG au Assad?
Ofisi ya CAG haikuwahi kutoa ripoti ya kuwa bunge ni "dhaifu" ila Assad baada ya kukaa kwenye kiyoyozi akabwatuka kuwa bunge ni dhaifu.
Bunge linataka CAG Mwingine na sio huyu anayeliita bunge dhaifu kwa kutumia "akili" zake badala ya evidence kama taaluma yake inavyomtaka.

Mfano:
Askofu Bangoza anaropoka mambo ya kisiasa kama Bangoza na sio hiko cheo cha uaskofu.
Hakuna mahali CAG amesema kuwa bunge ni dhaifu.
Amesema kama bunge haliranya kazi yake sawasawa basi ni UDHAIFU wa bunge kwa suala mahususi.

Huenda mambo mengine Bunge ni imara kama vile kiwashughulikia wapinzani Bungeni.

Bunge ni imara katika Kudai maslahi yao.
Bunge ni imara katika michezo ya mabunge kuna mambo Mengi Bunge linaonyesha uimara wake.
Kama hawakujadili kwa umakini ripoti ya CAG basi ni Udhaifu wa Bunge na sio yeye.
Kosa lake hapo ni nini!

Udhaifu wa Bunge ulionekana kwenye suala la Kikokotoo na uimara wa Raid ukaonekana kulishughulikia.

Bunge likiwa dhaifu kwenye kujadili riport ya CAG hii nchi itapigwa sana.
Mana wananchi nao ni dhaifu kuwachagua Wabunge dhaifu kama akina Naursary,Musukuma,Kibajaji na wengine wengi wagonga meza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio takataka zinazojua kuropoka tu
Kabisa kuna wengine ni fedheha kuweka title hizo maana ni kuwadhalilisha Phd halisi wanaojitambua eg Le Profeseli anayetambulika na Msajili kumuita prof ni kuwadharirisha real profs kama Kina Prof Assad.
 
Back
Top Bottom