Sakata la CAG: Tafakuri ya Askofu Bagonza

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,709
Reaction score
35,712
YAMETOKEA, Itakuwaje sasa?

Kuna maswali magumu mbele yetu baada ya bunge kupitisha uamuzi wa kihistoria tarehe 2 Aprili 2019.

1. Je, Bunge limepitisha azimio la kutofanya kazi na Prof. Assad au na CAG?

2. Kama ni Prof Assad, basi Bunge bado linaweza kufanya kazi na CAG Assad.

3. Kama Bunge halitafanya kazi na CAG, linamuingiza Rais ktk mgogoro mkubwa wa Kikatiba, kwa sababu:

- Ndani ya siku 7 tangu kupokea Ripoti ya CAG, Rais anatakiwa kuipeleka Ripoti Bungeni iliyofanywa Kazi na CAG ambaye ni Prof. Assad.

4. Asipoileta atakuwa amevunja Katiba ya Nchi aliyoapa kuilinda.

5. Akiileta, atakuwa amelidharau Bunge wakati naye ni sehemu ya Bunge.

6. Akiteua CAG mwingine, huyo mpya hatakagua upya bali ataleta iliyokaguliwa na CAG Prof. Assad ambaye hatakiwi Bungeni.

7. Katiba inatamka kuwa; mchakato wa kumuondoa CAG ni mrefu na iko kimya kuhusu kuendesha mchakato wakati kuna Kaimu CAG.

Ukiwahi kuzaliwa unaona mengi. Ukiwahi kufa unakosa mengi.

Dumisha Uhuru na Umoja.

(Copy and Paste)
FB_IMG_1554230830933.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
(Copy and Paste)View attachment 1061433

Sent using Jamii Forums mobile app
Pascal Mayalla njoo huku namba 3 inakuhusu!
 
Inafaa wabunge waelewe kuna muhimili uliojichimbia chini zaidi.
 
Bungeni tumewekewa spika,anayetoa sauti kupitia hiyo spika hatujamjua,spika ni kifaa tu cha kukuzia sauti
 
Kwa sasa sioni sheria au katiba yoyote inayofuatwa, lolote laweza kutokea.Prof Assad amesimamia ukweli bunge letu dhaifu sana.Sioni hata sababu ya vikao dodoma spika amekua ni katibu wa magogoni siku hizi
Bora profesa akapumzike chuoni afundishe vijana kuliko kufanya kazi katika mazingira yaliyojaa unafiki ubaguzi

FaizaFoxy
PASKALI mayalla
 
Akiwa Mstaafu period, Katiba aimpi ruksa tena kufanya kazi yoyote ya Umma.
 
Back
Top Bottom