wabongo ni maiti tu ndio maana watu wanavumyiwa nyumba zao na hawaseme kituWabongo bwana, eti MTU akihoji utendaji wa serikali na maamuzi yake ya kukurupuka, na kujaribu kuonyesha hasara nchi hii imeipata, zaidi akiwatanabahisha wanasheria watende kwa weledi katika uingiaji wa mikataba na kuishauri serikali ipasavyo inapotaka kuvunja mkataba, badala ya kuhanikizwa na wanasiasa.
Leo MTU huyo anaitwa si mzalendo. Je uzalendo ni kupiga vigelegele kwa kila serikali inachokifanya, pasi na kuishauri, kukosoa au kuonya? Wengi tunakumbuka mikataba ya madini inayopigiwa kelele kwa sasa huko nyuma ulipokuwa ukihoji majibu yake yalikuwa kama haya. Ooh! Wavivu wa kufikiri, ooh wawekezaji wanatumia mitaji mikubwa tuwalinde.
Ooh tunajenga mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji na tusipofanya hivyo wataenda nchi zingine, hivyo Rais wetu ( BWM) anahitaji kuungwa mkono na mguu sasa yako wapi?
Sent using Jamii Forums mobile app