Saini ya gavana imebadilika?

Sci_fimovies

Member
Sep 15, 2019
43
97
Jamani wanajukwaa,

Leo nimeshangaa nimeenda kwa duka kufika nilikuwa na noti ya 1000 mpya kabisa kufika dukani muuza duka akaikagua kwenye saini akasema hii ni hela feki sababu saini ya gavana imeandikwa Mpango akaikataa na ukicompare na zile noti zingne haijaandikwa Mpango saini yake

Kwa anayefahamu juu ya hili naomba anijuze .

Nawakaribisha wanaojua juu ya hili

Asante
1574447851278.jpeg
 
Hakuna kitu kama hicho. Kuna siku nilienda na laki nne noti mpya zaelfu tano tano, nimetoka kuchukua benki ili niweke kwenye Mpessa. Dada wa mpessa akaanza kuzikagua akasema mbona zimechanganyika na feki!!! Duuh! Nikamwambia nipe pesa zangu,nikaenda kudeposit kwa mwengine.
 
Duuh... Inabidi serikali itupe knowledge ili tujue pesa fake na original kipi kinatofautisha
Maana watu wanakariri asa kwenye hii swala la saini
 
Apa itabidi tuweke Hela ATM tu
Sema Tz atuna mambo ya kulipa kwa Card kama wenzetu kwaiyo itatubidi tu kuzifahamu izo noti feki zipoje
Benki moja tu ndo ina huo mfumo wa kuweka hela kwenye ATM zingine bado hazijaingia huko ni NBC pekee kwa Tz.
 
Sahihi ya Waziri wa Fedha kwenye 10000 na 1000 zina utofauti japo ni Waziri yule yule.
Chunguza
 
Sahihi ya Waziri wa Fedha kwenye 10000 na 1000 zina utofauti japo ni Waziri yule yule.
Chunguza
Anhaaa nimeona za tofautiana ila mbna zaman zilikuwa sawa kwann noti za 1000 za sasa zimechange ila kwenye 10000 ipo ile ile na atujapata ata maelekezo ya mabadiliko... Ndo maana watu wanahisi ni hela feki
 
Benki moja tu ndo ina huo mfumo wa kuweka hela kwenye ATM zingine bado hazijaingia huko ni NBC pekee kwa Tz.
Sio kweli, First National Bank (FNB) unafanya deposit pia kwenye atm za nje ya branch zao.

Limit kwa muamala mmoja ni 1M.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom