Saikolojia ya rangi

Lumbi9

JF-Expert Member
Oct 12, 2014
8,638
12,061
Hii nimeipata mahali nikaona ni vema ku-share nanyi,

Njano: Inapopakwa ndani ya chumba inahamasisha mazingatio, huamsha akili kuwa tayari na ndio maana hupakwa katika mabasi ya shule ili watoto wasiachwe wanapoyasubiria. Haishauriwi kupaka rangi hii pekee kuzunguka chumba kizima.

Kijani: Hii inahusishwa na afya na mimea asili, pia hufanya mwili u-relax ndio maana mara nyingi hupakwa mahospitalini. Pia ikiwa waalimu watatumia marker pen ya kijani katika ubao mweupe atachochea uelewa wa mtoto.

Nyekundu: Hii haishauriwi kabisa kupakwa ktk shule za watoto au vituo vya kulea watoto kwa kuwa mara zote inahusishwa na ukorofi. Na mara zote hutumika kuashira hatari.

Bluu: Hii ni mbadala wa nyekundu, inaelelezwa kwamba hii ni rangi ya utulivu na umakini. Inashauriwa sana kupakwa ofisini na ktk madarasa ya hesabu.

Machungwa: Rangi hii inasemekana ni nzuri kutetea mahusiano, lakini pia huchochea mawasiliano, lakini pia ukipaka rangi hii unashauriwa uchanganye na rangi nyingine ili kupata muonekano ulio bora.
 
Pia rangi nyeupe haishauriwi kupakwa popote ikiwa pekee sababu huchochea akili kulala kifikra.
[HASHTAG]#Rangi[/HASHTAG] ya bluu pia husaidia kupunguza kasi ya mapigo ya moyo na hofu, pia huchochea utendaji kazi.
 
Asante kwa somo
naona nyekundu naendana nayo nitapaka chumbani kwangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom