Saikolojia: Kushindana na wanaobeba Chuki

Education Mentor

JF-Expert Member
Oct 26, 2016
393
1,000
SAIKOLOJIA: KUPAMBANA KUSHINDANA CHUKI
Katika somo la leo najaribu kuangazia Saikolojia ya kuhusu chuki ambao katika Ulimwengu wa leo uliotaharuki kwa visasi na ukatili kutokana na tatizo hilo.

Lakini kuhusu chuki si kwamba tu imekuwepo katika ulimwengu huu tu ni jambo ambalo limekuwepo kwa karne na karne nyingi, lakini shida inakuja sababu hatujui namna ya kupambana na chuki au kuelewa kwanini chuki zinakuwepo au unajikuta unaingia katika mazingira ya kuchukia au kuchukiwa.

Chuki mara nyingi anazaliwa na Hasira inayochochewa na fitina au taarifa zinazochochewa vibaya. Na Chuki ndio baba wa vita na machafuko Ulimwenguni kote kuanzia katika familia, koo, jamii, kabila, taifa na hadi mataifa.

Sababu chuki anabebwa kirahisi na kutumika kama propaganda ili kuunganisha jamii kuwa na adui mmoja katika dhana ya Utaifa (Nationalism), mifumo ya kimaisha mfano ubepari na ujamaa na hata katika dini pia.

BASI TUANZE NA TAFSIRI MUHIMU KWANZA JE, CHUKI NI KITU GANI?

Tafsiri

Chuki ni hali ya kutokuwepo upendo hali ya kuwa na roho mbaya hali ya kuwa na kinyongo.

Tunaona misamiati mitatu muhimu inatokea katika tafsiri ambayo ni kukosekana upendo, roho mbaya na kinyongo.

Kisaikolojia
Chuki ni hisia za ndani za kutokutaka, kuvutiwa au kupenda

Jambo au kitu chuki kinaweza tofautiana kwa kiwango tofautitofauti na muelekeo wa tabia za uadui ambapo upelekea uharifu, mauaji au hata vita.

Kwanini basi kuna Chuki? sababu kuna wakati unaweza jiuliza kwanini nachukiwa na pengine ukatafuta suluhu pasipo kupata majibu ya kuridhisha.

Aina za chuki
Chuki katika dunia ya leo zinagawanywa katika makundi kama yafuatayo chuki za kisiasa, Kidini, kijinsia na zile za rangi (Racism)

Chuki hubeba sifa nyingi lakini baadhi ni hizi
 • Chuki husambaa haraka sana kuliko hasira
 • Chuki ni chombo kinachotumika kutengeneza na kusambaza propaganda
 • Chuki huwa inatoa ujasiri wa kitambo tu
 • Chuki ni hasira iliyojengwa muda mrefu hata kukomaa kutokana na taarifa za aina ya fitina

  BASI FAHAMU MAZINGIRA YANAYOWEZA SABABISHA CHUKI?
 • Fikira potofu
Katika suala la fikra linaweza kuwa na chanzo tofauti za kiasikolojia au zile za kimazingira.

Mfano kama mbeba chuki ana matatizo kama vile Schizophrenia au Bipolar disorder na mengine mengi yanaweza kumpelekea kuwa na chuki pasipo mantiki.

Lakini katika suala la fikra inaweza kuwa shida ya kimazingira tu labda kiburi mfano labda ndugu mmoja anaona jamii flani au jinsia flani ni duni au washamba basi hawapaswi kuwa na fursa au nafasi katika jamii.
 • Kujifunza
Pia chuki unaweza jifunza kupitia malezi ya familia au kujifunza kupitia vikundi au vyama vyenye itikadi kali na misimamo mikali kwa jamii nyingine. Chuki ni hisia rahisi sana kusambaa kwa njia ya taarifa au mafundisho hivyo wakati mwingine ni chombo cha propaganda na ndipo mahali pengine neno ugaidi linapozaliwa.

1595248113791.png


 • Sumbua Tendea Vibaya au Tesa jamii au kundi flani
Chuki pia inaweza tokana na majeraha ya nafsi au ya kimwili baada ya mtu kutenda au kutendwa na jamii na kikundi flani basi tangia wakati huo huamsha hisia za chuki ambazo husumbua jamii zao ikiwa kama haki inayodhaniwa haitatendeka au kuwepo kwa tume ya upatanishi.

1595248198797.png

 • Misiguano ya kimasilahi
Hii mara nyingi sana maeneo ya jamii kama makazini au hata kwenye jumuiya inapotokea kuwa kisababishi cha masirahi ya watu au kikundi Fulani kuzuia au mfumo huo kuharibiwa basi ni rahisi kusababisha chuki.

Hata kama masirahi hayo ni halali au batili kwahiyo wakati wote unaweza kujikuta unatumbikua katika chuki bila kufahamu labda pengine umekuwa sehemu ya kupambana na rushwa au uharifu Fulani.
 • Husuda
Tafsiri ya husuda ni hisia za wivu hasi ambazo humpelekea mtu kutofurahia mafanikio na maendeleo ya mwingine. Kila mwanadamu ana hisia za wivu lakini wivu tunapohurusu kugeukia upande wa hasi ndipo ujitokeza

Husuda mara nyingi sana ndizo zina zaa Majungu na fitina hasa kama kuna ushindani wowote makazini na kwenye jamii.

Kutokana husuda huanza na wivu unaoegemea upande hasi. Hivyo ni muhimu sana kujifunza kufurahia mafanikio ya wengine na pia yakikupa motisha.

UFANYE NINI UNAPOKUMBANA NA TATIZO LA CHUKI KATIKA JAMII AU MAKAZINI
 • Muhimu fahamu kwamba sio wakati wote unaweza fahamu kwa nini unachukiwa?. Hivyo muhimu kuchukua hatua za kiusalama hasa pale vitisho vinapokuwa vinachukua hatua.
 • Pata washauri wazuri sababu wakati mwingine kuna vitu tunafanya tunakosea hivyo kwa hali ya kibinadamu inakuwa sio rahisi kufahamu. Hivyo ni muhimu kuondoa kiburi na kukubali kuweza shauriwa au shaurika.
 • Wakati mwingine hii utokea kazini hasa pale unapokuwa labda pengine una juhudi katika kujituma kwa kazi sana (do gooders) hii pia zipo tafiti zinazodhibitisha huwa ni vichochezi vya chuki makazini au mashuleni.
 • Wakati mwingine katika ushindani wa namna yoyote kati ya mtu na mtu au watu na vikundi hasa unapojitokeza kutoa msaada upande mmoja kwa kufahamu au kutofahamu.
 • Wakati mwingine ni muhimu sana kujifunza kukaa kimya sababu kuongea ongea napo pia huchochea kujenga chuki.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom