Sai baba na princess muro tunduma acheni usanii huu.

Jaguar

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2011
Messages
3,412
Points
1,225

Jaguar

JF-Expert Member
Joined Mar 6, 2011
3,412 1,225
Kuna ka-tabia nimekashuhudia kwa booking office za princess muro na Sai baba pale Tunduma.Hawa jamaa wana ka-tabia ka kukataa kuwakatia ticket abiria wa kawaida wa ki-Tanzania na badala yake zile ticket wanawauzia madalali na wahuni mbali mbali.Kinachofanyika inapojiri muda wa asubuhi kwa ajiri ya safari,wale madalali wanawauzia zile ticket abiria wanaotoka nchi za kigeni za DRC,ZAMBIA,MALAWI na hata wazungu pia.
Kibaya ni kwamba hawa jamaa wanaziuza zile ticket kwa ulanguzi wa hali ya juu.Kwa kawaida nauli ya Dar-Tunduma ni kati ya 30000-35000Tshs,lakini hawa jamaa wanaziuza kwa 60000Tshs na zaidi.Na hii haifanywi kwa abiria wa kigeni tu,hata m-TZ pia ukifika mida ya asubuhi na una shida kubwa ya usafiri,wembe ni ule ule,unapigwa chanuo 60000Tshs na kuendelea.
Nawaomba kama kuna wahusika wa karibu wa mabasi haya na wanasoma uzi huu,basi wajaribu kulifanyia kazi hili suala coz linachafua majina ya makampuni yenu.Tena huu uhuni unafanyika miezi ya kawaida kama august,september na october,vipi itakapofika december?si mtatupiga laki!?
 

Forum statistics

Threads 1,390,085
Members 528,081
Posts 34,042,413
Top