Sahihi kuvuta Sigara baada ya kufuturu?

Soda,mafuta ya kula,sukari vinadhuru mwili,ni Haram!?
Sukari ni muhim katika mwili wa binadam ndo maana Kuna muda hata hospital mtu anapewa glucose.
Niambie ni ipi faida ya sigara kwenye mwili wa binadam na lin ulienda hospital ukavutishwa hata fegi ili urudi kwenye hali yako baada ya kuonekana Kuna kiwango Cha fegi kimepungua mwilini

Alafu hata maji yanauwa ikiwa utayatumia matumizi yasiyo sahihi , Unaambiwa maji ni uhai lakin nenda kajirushe baharini uone Kama utaishi.
Katika uislam kila chenye madhara ni Haram na kila kilicho halali kinatakiwa kitumiwe kwa kiasi hata chakula ukila kwa pupa bila kiasi kiasi Cha kuuletea shida mwili wako(kuvimbiwa) unapata dhambi kwa mujibu wa mafundisho ya uislam
 
Sijutii wala sijisifu

Nimejikuta tu sivuti sigara , sinywi pombe , wala sivuti bangi.. mpaka najisemeaga nna bahati gani? Karibu rafiki zangu wote wanavichakata hivyo vitu.

Na wanasemaga kama hivyo vitu haupendi utakuwa mpenzi wa wasichana ( malaya) kwa mwanaume na Sipo hivyo kabisa ..
 
Soda,mafuta ya kula,sukari vinadhuru mwili,ni Haram!?
Kama vina dhuru mwili ni haramu. Hata samaki kama ukimla anakudhuru wewe na mwingine hamdhuru, wewe ukimla unapata madhambi na anakuwa haramu kwako ila kwa mwingine ambaye hadhuriki na samaki huyo ni halali kwake.
 
Acha kuharamisha ambavyo Allah hakuharamisha,unajipa uungu,mwenye mamlaka ya kuharamisha ni M/mungu pekee
 
Sukari ni muhim katika mwili wa binadam ndo maana Kuna muda hata hospital mtu anapewa glucose.
Niambie ni ipi faida ya sigara kwenye mwili wa binadam na lin ulienda hospital ukavutishwa hata fegi ili urudi kwenye hali yako baada ya kuonekana Kuna kiwango Cha fegi kimepungua mwilini

Alafu hata maji yanauwa ikiwa utayatumia matumizi yasiyo sahihi , Unaambiwa maji ni uhai lakin nenda kajirushe baharini uone Kama utaishi.
Katika uislam kila chenye madhara ni Haram na kila kilicho halali kinatakiwa kitumiwe kwa kiasi hata chakula ukila kwa pupa bila kiasi kiasi Cha kuuletea shida mwili wako(kuvimbiwa) unapata dhambi kwa mujibu wa mafundisho ya uislam
Huna elimu jamaa yangu,Wala huna uwezo kidogo wa kutafakari
 
Wakati wa mfungo wengi wanaacha kuzini na kunywa pombe ,lakini wavuta sigara wakifuturu tu moja kwa moja wanavuta sigara, je sigara siyo anasa? Na ni sahihi kuvuta sigara baada ya kufuturu?
sigara ni MAKURUHU, unaweza kuvuta baada ya kupata futari, lkn si kabla ya hapo ndani ya mwezi wa RAMADHANI. bali UISLAMU unakataza kutumia kitu chenye kudhuru afya yako, sigara ikiwemo.
 
Kama mufti anavuta ma wewe vuta

Igeni viongozi wenu ili mkifika jahanam muwasingizie waliwapotosha
 
Kama vina dhuru mwili ni haramu. Hata samaki kama ukimla anakudhuru wewe na mwingine hamdhuru, wewe ukimla unapata madhambi na anakuwa haramu kwako ila kwa mwingine ambaye hadhuriki na samaki huyo ni halali kwake.
The same way na kwa nguruwe?

Kama mwingine akimla na hadhuriki kwa kigezo hicho hiyo ina maana inakuwa ni halali kwake?
 
Acha kuharamisha ambavyo Allah hakuharamisha,unajipa uungu,mwenye mamlaka ya kuharamisha ni M/mungu pekee
Nimeharamisha kipi kijana ? Naona umeamua kunizushia siyo ?

Kwani hekima ya kuharamishwa ni ipi ? Unatakiwa ukasome dini, usiwazushie watu uongo.
 
The same way na kwa nguruwe?

Kama mwingine akimla na hadhuriki kwa kigezo hicho hiyo ina maana inakuwa ni halali kwake?
Nguruwe ana dhuru mwili na kumekuja nususi za wazi zikimuharamisha, kwahiyo hata kama angekuwa hadhuru ila dini imesha muharamisha kwa wazi, kwahiyo ni haramu.
 
Mi kuna jamaa yangu mmoja anasema pombe imekatazwa na vifungu vipo ila hakuna verse iliyoyoa katazo kwa sigara
Ni sahihi alichosema Sigara kuna mawazo tofauti baina ya wanazuoni wa kiislamu kwamba ni haramu au ni kwamba inachukiza tu.

Kutokuwepo kwa aya au hadithi ya wazi kukataza jambo hilo ni moja ya sababu ya kutofautiana kwa wasomi.

Wapo wasomi wanaosema hii ni makruhu yaani inachukiza haipendezi kufanya lakini sio kwamba ukifanya kitendo cha kuvuta unapata dhambi ila haipendezi kabisa muislamu au binaadamu kufanya hayo.

Wengine wakasema sigara ni haramu kabisa kwa sababu inaharibu mapafu na ina madhara kwa binaadamu kwa sababu ni risk factor ya magonjwa mengi kama vile cancer,myocardial infarction,TB,pneumonia etc.

Na wakasema maadamu ina madhara basi haifai ni haramu kwa sababu mtume wa Allah kasema kwamba "haitakiwi kujidhuru wala kuwadhuru wengine" na mwenye kuvuta sigara anajidhuru taratibu.

Ila wasomi wa dini wengi wa sasa wanaisema ni haramu moja kwa moja kwa kutumia vipimo vya sheria ambavyo havikuja wazi kuharamisha.
 
kuna sigara zinatangazwa (hata humu JF niliona tangazo lake) kuwa sigara hizo ni tiba ya baadhi ya magonjwa na lia inakuja na extra tiba ya kuondoa addiction ya sigara zingine

Hii kidini imekaaje?

Itakuwa ni ruksa kuvuta kwasababu haina madhara mwilini na kuwa treated kama dawa au nayo itakuwa considered kama haramu?
 
Hapana Mkuu Hairuhusiwi Vitu Vyote Tulivyokatazwa Waislamu Hatutakiwi Kufanya Sio mwezi huu tu Hata baada ya Ramadhani
Kwa mara ya kwanza naona mnyiha wa mbozi Muslim utaenda kuswali wapi kule mbozi? Vwawa,mlowo,Tunduma, msiya ? Haya wamwitu
 
kuna sigara zinatangazwa (hata humu JF niliona tangazo lake) kuwa sigara hizo ni tiba ya baadhi ya magonjwa na lia inakuja na extra tiba ya kuondoa addiction ya sigara zingine

Hii kidini imekaaje?

Itakuwa ni ruksa kuvuta kwasababu haina madhara mwilini na kuwa treated kama dawa au nayo itakuwa considered kama haramu?
Kuna mswanachuoni aliwahi kusema الأسماء لا تغير الأحكام yaani "majina hayabadilishi hukumu ya kitu.

Kwa maana kama zinaa ukaiita ibada bado itabaki kuwa haramu hata kama jina lake zuri.

Na hata kama tendo la ndoa na mke ukaiita zinaa bado litabaki kuwa halali hata kama jina lake limekuwa baya.

So kama ipo sigara ambayo ni tiba ya magonjwa na kutibu kwake ni kwa kuvuta mimi sioni tatizo binafsi kwa sababu lengo sio kuitwa sigara bali lengo ni inafanya kazi gani.

Ni sawa na leo tunaotumia nyungu kujifukiza mtu aseme kwamba nyungu ni haaramu kwa sababu ule mvuke ni kama sigara tu au moshi,ataambiwa hapana ule mvuke ni tiba.

Hii kidini imekaaje?
Siwezi kusema kidini imekaaje kwa sababu sio msemaji wa dini ila kwa kuwa nina haki ya kuweka maoni yangu basi mimi nimeweka maoni ila niko tayari kusahihiswa na wanazuoni wa humu
 
Back
Top Bottom