Sahihi kuvuta Sigara baada ya kufuturu?

Dabil

JF-Expert Member
Sep 30, 2021
5,889
13,256
Wakati wa mfungo wengi wanaacha kuzini na kunywa pombe ,lakini wavuta sigara wakifuturu tu moja kwa moja wanavuta sigara, je sigara siyo anasa? Na ni sahihi kuvuta sigara baada ya kufuturu?
 
Kaka naweka Kambi hapa,Kuna washkaji zagu kabla ya kutia chochote wanaanza na fegi kwanza Kila nikiwaelewesha wananijibu we Bado Mtoto huijui arosto.
 
Dah! Wavuta fegi tuonewe huruma. Tunaandamwa sana. Tukigeuka huku TMDA, hatujapoa vizur sasa hata wakati wa futari tunayaka kuwekewa nongwa. Fegi sio dhambi!
 
Dini ya mnyaazi inakataza kunywa pombe tuu na sio kuvuta sigara... Tuliteremshiwa dini ila hatujakatazwa kuvuta sigara...
 
Wakati wa mfungo wengi wanaacha kuzini na kunywa pombe ,lakini wavuta sigara wakifuturu tu moja kwa moja wanavuta sigara, je sigara siyo anasa? Na ni sahihi kuvuta sigara baada ya kufuturu?
Sigara ni haramu muda wowote.
 
Mi kuna jamaa yangu mmoja anasema pombe imekatazwa na vifungu vipo ila hakuna verse iliyoyoa katazo kwa sigara
Kila chochote chenye kuzuru mwili ni haramu, hii ni kaida ya kiusuli iliyotokana na maneno ya mtume, ndiyo maana hata Bangi ni haramu lakini hukuti aya wala hadithi ikisema bangi ni haramu.

Haya mambo ni ya kielimu, na kuna somo maalumu kuhusu haya, dini inakupa misingi (usuli) kisha kutokea katika misingi hiyo hukumu zinaenea katika mambo mengine.
 
Sigara siyo haramu,haikuwepo wakati wamtume saw,kwa hiyo hakuna wa kuharamisha
Uislam haujaacha kitu chochote mzee
Chochote mzee
Amesema Allah ktk Surat Al-maida aya ((4))
((يَسْأَلُونَكَمَاذَا أُحِلَّ لَهُمْ ۖ قُلْ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۙ وَمَا عَلَّمْتُمْ مِنَ الْجَوَارِحِ ..))
Maana yake :-
""Wanakuuliza wamehalalishiwanini? Sema: Mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri na mlicho wafundisha wanyama kukiwinda. ......""

Sigara unaandikiwa No smoking ninhatari kwa afya yako
Moja kwa moja mwenyezi Mungu alishakataza vyovyote vinavyo dhuru kuwa siyo halali, hata shisha kwakua Ina madhara hiyo siyo halali katika uislam japo huenda haikuwepo kabla
 
Wakati wa mfungo wengi wanaacha kuzini na kunywa pombe ,lakini wavuta sigara wakifuturu tu moja kwa moja wanavuta sigara, je sigara siyo anasa? Na ni sahihi kuvuta sigara baada ya kufuturu?
sigara sio rahisi kumaintain inafika point mwili ndo unadai
 
Kila chochote chenye kuzuru mwili ni haramu, hii ni kaida ya kiusuli iliyotokana na maneno ya mtume, ndiyo maana hata Bangi ni haramu lakini hukuti aya wala hadithi ikisema bangi ni haramu.

Haya mambo ni ya kielimu, na kuna somo maalumu kuhusu haya, dini inakupa misingi (usuli) kisha kutokea katika misingi hiyo hukumu zinaenea katika mambo mengine.
Sio "kuzuru" ni "kudhuru"
 
Uislam haujaacha kitu chochote mzee
Chochote mzee
Amesema Allah ktk Surat Al-maida aya ((4))
((يَسْأَلُونَكَمَاذَا أُحِلَّ لَهُمْ ۖ قُلْ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۙ وَمَا عَلَّمْتُمْ مِنَ الْجَوَارِحِ ..))
Maana yake :-
""Wanakuuliza wamehalalishiwanini? Sema: Mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri na mlicho wafundisha wanyama kukiwinda. ......""

Sigara unaandikiwa No smoking ninhatari kwa afya yako
Moja kwa moja mwenyezi Mungu alishakataza vyovyote vinavyo dhuru kuwa siyo halali, hata shisha kwakua Ina madhara hiyo siyo halali katika uislam japo huenda haikuwepo kabla
Mafuta ya kula,sukari,soda vina madhara,mbona hamuachi!!!?...Qur'an imeshaweka kipi Haram kipi siyo
 
Kila chochote chenye kuzuru mwili ni haramu, hii ni kaida ya kiusuli iliyotokana na maneno ya mtume, ndiyo maana hata Bangi ni haramu lakini hukuti aya wala hadithi ikisema bangi ni haramu.

Haya mambo ni ya kielimu, na kuna somo maalumu kuhusu haya, dini inakupa misingi (usuli) kisha kutokea katika misingi hiyo hukumu zinaenea katika mambo mengine.
Soda,mafuta ya kula,sukari vinadhuru mwili,ni Haram!?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom