Safari yangu ya South Africa

Kanali mwime

Member
Joined
May 5, 2018
Posts
71
Reaction score
171
Wakuu as salaam aleikum,

Nimejiunga JF ili nipate wadau wazoefu na hii safari yangu ya SA adventure natumia njia ya barabara nitasafiri na taqwa hapo kesho nikitokea Ubungo mpaka Lusaka.

Sijawai kufika, elimu yangu darasa la saba kingereza najua pia siendi kujiunga na Watanzania walioshindikana huko.

Nina pesa ya kujikimu wakati natafuta kazi sina mwenyeji nilizaliwa kupambana, kila la kheri wakuu mwenye kuniongezea ushauri nitashukuru
 
Haya bana
 
sema unataka ushauri wa kuhusu nini mzee baba.

Wa njiani.. vikwazo... vya South ukishaingia au ushauri upi wahitaji yakhee!
 
sema unataka ushauri wa kuhusu nini mzee baba.

Wa njiani.. vikwazo... vya South ukishaingia au ushauri upi wahitaji yakhee!
Sihitaji vitisho vya mambo nitakayo yakuta huko nipe ushauri WA Kawaida mkuu
 
Sihitaji vitisho vya mambo nitakayo yakuta huko nipe ushauri WA Kawaida mkuu
hakuna vitisho mzee baba... umeamua kwenda mwenyewe kama mwanaume utakalo likuta uendako likabili kiume.

usisahau kadi ya njano... hapo Nakonde wazambia wasumbufu saana.

lingine, hapo hapo Nakonde unaweza kupigwa pesa kwenye kubadilisha pesa kuwa makini usimwamini mtu.
 
Nitabadili Pesa benk na si kwingineko pia kadi ya manjano ninayo mkuu, nipo full labda wanionee tu
 
Unafikiria kufanya kazi gani ukifika huko ...!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…