Safari yangu ya kwanza na Air Tanzania

Tunaelekea njia ya kuruka na mambo ni bam bam! Nikiishatua Charo nitakwenda kuona kaburi la JPM. Mungu ibariki Tanzania .... Mashine inavuta Kasi na tuko angani sasa.
Mwamba haya matukio.yametokea ndani ya muda gani. Jinsi ulivyosimulia hapa ni kama sekunde 20 tangu mnaelekea njia ya kuruka hadi kuvuta kasi hadi kuwa angani

Anyway mi sijawahi panda ndege nisije kukubishia bure

Alafu si wanasemaga ukiingia kwenye ndege unazima simu?
 
Bila shaka umo ndani ya hiiView attachment 1777234
Naam, ndio yenyewe.
Mwamba haya matukio.yametokea ndani ya muda gani. Jinsi ulivyosimulia hapa ni kama sekunde 20 tangu mnaelekea njia ya kuruka hadi kuvuta kasi hadi kuwa angani

Anyway mi sijawahi panda ndege nisije kukubishia bure

Alafu si wanasemaga ukiingia kwenye ndege unazima simu?
Ni kweli nilikuwa naandika huku tukio likiendekea. Baada ya kupaaza nilizima Simu.

IMG_20210508_125011_824.jpg
 
Wapo kiasi chake. Huenda wakaongezeka,lakini kwa watu wa Magharibi kwa maana ya Biharamlo Geita Ngara Runzewe Kakonko na Kibondo ni poa sana kwani itapunguza masaa ya kusafiri kutoka 24 hadi 12 au chini yake.
Just good! Sory pale kuna hifadhi ya wanyama vipi nayo katika safari yako ulikuwa na mtu yeyote ambae uliweza kumuhisi kama ni mtalii?
 
Just good! Sory pale kuna hifadhi ya wanyama vipi nayo katika safari yako ulikuwa na mtu yeyote ambae uliweza kumuhisi kama ni mtalii?
Sikuona mtalii au anayefanana nao, ila kuna jamaa nahisi ni watu wa migodini walikuwa kwenye safari
 
Just good! Sory pale kuna hifadhi ya wanyama vipi nayo katika safari yako ulikuwa na mtu yeyote ambae uliweza kumuhisi kama ni mtalii?
Kwa mtazamo wangu, jamaa alikuwa na ndoto ya kuyaendeleza maeneo yaliyobaki nyuma kimaendeleo ikiwemo Chato.

Kimji hicho kidogo kina miradi mikubwa ambayo ikikamilika na kuendeshwa kwa ufanisi kulingana na mpango kazi, tutegemee Boom kwenye ukanda huo au tembo mweupe maono yasipotekelezwa.
 
Safari ya kurudi Dar es salaam kutoka Chato kwa ndege ya Air Tanzania ilichelewa kwa saa moja. Kati ya mapungufu niliyoyaona kwenye shirika ni kutokutoa taarifa kwa abiria kuhusu uchelewaji na ofisi ya wakala wa Air Tanzania pale Chato kufungwa asubuhi tu.

Taratibu za upekuzi pale uwanjani zilifanyika vizuri na kwa haraka. Kulikuwa na abiria wapatao Kumi, idadi ambayo inatia matumaini kwa kiwanja kidogo vile na hasa ukizingatia kuwa ilikuwa inakwenda kushusha na kupakia abiria wa Mwanza.

Ndege ilijaa hadi kuvuka nusu ya viti, kulikuwa na mapengo machache. Ndege iliyotumika TC-TCB kwenye njia hiyo inaonyesha uchakavu kwa kiasi fulani kwenye viti na vishikio, rangi pia zinaanza kufifia kwa ndani, nje safi. Nashauri matengenezo madogo madogo yafanyike na sisi abiria tutunze mali zetu vizuri. Wahudumu wote waliokuwa kazini jana wako vizuri na walitoa huduma iliyotukuka.

Marubani pia wako vizuri nawapongeza kwa weredi na umakini katika kufanya kazi yao. Kuruka Chato safi kutua Mwanza safi sana, hakukuwa na mkito!.
Abiria wa Mwanza walikuwa wengi hadi kujaza viti karibu vyote, nyomi ya uhakika kabisa ilitamalaki. Kuruka Mwanza kama ilivyokuwa Chato safi ila kutua Dar, yumba yumba kidogo mkito ulisikika...lakini safi.

Kwa ujumla Air Tanzania imeishaingia kwenye Ligi ya usafiri wa anga na mashirika ya kimataifa, hadi sasa wanafanya vizuri,waongeze bidii zaidi katika kazi ya kuwahudumia watanzania. Marubani waongeze umahiri na weredi wakati sisi watanzania tukiwajibika kutunza mali hii ya umma.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Air Tanzania.

IMG_20210522_111131_196.jpg
 
Back
Top Bottom