Safari ya Mwanza-Shelisheli kwa uongo yaishia Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Safari ya Mwanza-Shelisheli kwa uongo yaishia Dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, May 17, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  MTU mmoja anayedaiwa kuwa ni mchawi alidondoka kwenye nyumba moja eneo la Mbezi Luis jijini Dar es Salaam akiwa safarini kwa njia ya ungo akielekea Shelisheli kwenye mkutano wa wachawi.

  Taarifa za awali zilieleza kwamba mtu huyo alijieleza kwamba alitokea mkoani Mwanza akiwa na wenzake sita wakielekea kwenye mkutano nje ya nchi , lakini bahati mbaya yeye alidondoka katika jiji la Dar es Salaam.

  Pmaoja na bahati mbaya yake ya kudondoka, lakini pia alikubwa na kipigo kikali kutoka kwa wakazi wa eneo la Mbezi asubuhi ya jana na kusababisha kifo chake.

  Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, marehemu ambaye jina lake halikujulikana alidai alidondoka na ungo wake katika eneo hilo alipokuwa safarini.

  “Huyu mtu ana umri wa kati ya miaka 28 na 35, alikuwa hana nguo, bali alijifunga kipande kidogo cha nguo kukinga sehemu za siri na alikuwa amejipaka masizi usoni na sehemu zingine za mwili,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

  Naye mwenye nyumba alipodondoka marehemu , Mwajabu Shabani alisema aliamka jana saa 12 asubuhi na kwamba alipofungua mlango wa kutoka nje, ghafla alimuona mtu huyu akiwa amekalia ungo na kujiinamia.

  “Nilishtuka kuona mtu wa namna hiyo, katika hali ya kiwewe na kutaka msaada kwa watu, wakaja na kuanza kumhoji huku vurugu mshangao vikizidi kuongezeka na kusababisha mlango wa nyumba yangu kuvunjwa,” alisema mama huyo.

  Alisema katika mahojiano hayo mtu huyo alidai kuwa alitoka Mwanza akiwa na wenzake sita wakiwa safari kuelekea Shelisheli kwenye mkutano ambapo wenzake wamemwacha.

  Mwandishi alishuhudia ungo aliokuwa akitumia mtu huyo kusafiria ambao ulikuwa ukichomwa na baadhi ya watu waliokuwa katika eneo hilo , lakini haukuungua .

  Ungo huo ukawa kivutio kwani hata baada ya kuweka mfuta ya taa moto haukuwaka.


  Pamoja na ungo huo kulikuwa na vitu vingine kama, pembe ya ng’ombe iliyokuwa imefungwa na matambara.

  Jitihada ya kumpata mwenyekiti wa mtaa aliyejulikana kwa jina moja la Kayanda hazikufanikiwa na ilisemekana alikuwepo kwenye eneo la tukio ila aliondoka baada ya kupingwa na kukimbia kutokana juhudi zake za kuwazuia watu wasimpige mtu huyo.

  Mwandishi aliona vurugu zilivyozidi na aliamua kwenda kituo cha polisi Mbezi kwa Yusuf, lakini alipishana na polisi waliokuwa wakielekea kwenye tukio ingawa walikuta tayari mtu huyo alishauawa.

  Polisi waliuchukua mwili wa mtu huyo ingawa waliauacha ungo wake na vitu vingine huku watu wakiendelea kuushangaa ungo huo uliokuwa hauungui moto.


  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga alipoulizwa juu ya tukio hilo, alisema bado hajapata habari hizo.

  “Ndiyo kwanza nazisikia habari hizi kwako, hata asubuhi nilipoambiwa matukio yaliyotokea katika mkoa wangu, hilo sikuambiwa, lakini nitafuatilia tukio hilo,” alisema Kamanda Kalinga
   
 2. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mkuu mimi siaminigi kabisa uchawi naogopa sumu tu. Uliwahi kuwa na bosi mchawi wewe?
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  Namwamini yesu,
  yeye ni kinga na ngao ya maisha yangu.
   
 4. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kama hauamini uchawi, basi wamekuchawia na kukufunga akili yako yote hata haujitambui, unahitaji msaada....uchawi upo, wote wanaofikiri uchawi haupo wamelogwa tayari. kama Mungu alivyo yupo, na shetani na uchawi wake upo pia, na vinafanya kazi kama kawaida...na watz asilimia kubwa wameshaathirika kwa namna moja au nyingine na uchawi.
   
 5. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,991
  Likes Received: 3,740
  Trophy Points: 280
  Kuna roho mbili. Ya kwanza ni ya Ki-Mungu (wanasayansi wanaiita eti "nature") na ya pili ya ni ya kibini-Adamu. Hii ya pili inaji-manifest katika vitu vinavyoitwa "uchawi","shetani" na vitu vinavyonana na hivi. Uchawi, shetani, etc ni vitu vya kisaikolojia tu. Mchawi wako ni wewe mwenyewe na huyo unayemwita "shetani" ni wewe mwenyewe pia - inategemea jinsi brain, soul and heart zinavyo-respond against certain situations. I have dared the so called "wachawi" to try and bewitch neraly so many times lakini sikuchawika. Hata mafua sikupata. Conclusion - hadithi ya hapo juu ni ya kuuza gazeti tu!
   
 6. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Unajua ni vizuri kuwa na theory kama hizi.

  Ninacho elewa uchawi upo hata kwenye vitabu vya dini umeandikwa. Ila ili usikudhuru unatakiwa kumcha mungu kwa kiwango cha juu kabisa, kama una imani haba na ya kawaida huwezi kukwepa kusumbuliwa na uchawi.

  Watanzania wala rushwa hawawezi kukwepa uchawi, pia wazinzi hawawezi kukwepa kusumbuliwa na uchawi maana hizi zote ni dhambi hata kupokea kitu kidogo na kutoa kitu kidogo.

  Inatakiwa kumuamini mungu si kwa maneno, hila ni kwa vitendo na siyo kujionyesha machoni mwa watu kuwa ni mcha mungu hila gizani unafanya mambo mengine.

  Hivyo wanadamu hili kutosumbuliwa na mambo haya ya kidunia tunatakiwa tuwe wacha mungu wa kweli kabisa. Hata kama unamdanganya mume wako au mke wako hujue si msafi ati.
   
 7. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Kuna dunia mbili ya mchana na ya ucku. Akili ku mukichwa
   
 8. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #8
  May 17, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kalagabahoo subiri watakapo kukwida ndo utajua kumbe uchawi ni laivuuuuu
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  May 17, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Lakiini inasikitisha jamaa ameuawa. Ingekuwa uzunguni huyu wangempeleka kwenye maabara awafundishe jinsi ya kupaisha ungo wake.
   
 10. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #10
  May 17, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  nimeshuhudia uchawi kwa macho yangu haya ya nyama alafu mtu anasema haamini uchawi, kama si unafiki ninini hiyo?
   
 11. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #11
  May 17, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,991
  Likes Received: 3,740
  Trophy Points: 280
  nawasubiri kaka/dada. nawasubiri.
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  May 17, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  hehehehehehe
  jiji tetesi bwana
   
Loading...