Tunaelekea wapi? Mali zetu zitawatoa roho wanetu!

Tunaelekea wapi? Mali zetu zitawatoa roho wanetu!

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
22,756
Reaction score
27,481
Imeandikwa kwenye kuruan tukufu!,:-
Mwenyezi mungu ameshatutahadharisha kuhusu watoto na wake

يٰۤاَيُّهَا الَّذِيۡنَ اٰمَنُوۡۤا اِنَّ مِنۡ اَزۡوَاجِكُمۡ وَاَوۡلَادِكُمۡ عَدُوًّا لَّكُمۡ فَاحۡذَرُوۡهُمۡۚ

Maana: Enyi mlio amini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu wamo maadui zenu. Basi tahadharini nao.
============
============

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limethibitisha kuwa mtu aitwaye Ramadhan Jafari miaka 47, mkazi wa Mbezi Luguruni aliyedaiwa kuwa amepotea alikuwa ameuawa na kufukiwa ndani ya moja ya chumba katika nyumba yake iliopo eneo la Mbezi Luguruni Kwembe Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam.

Taarifa ya leo Juni 23, 2026 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam imeeleza kuwa mnamo Juni 16, 2026 katika kituo cha Polisi Kimara Gogoni Ubungo, jeshi hilo lilipokea taarifa za kupotea kwa mtu huyo kutoka kwa ndugu wa karibu kabla ya kuanza uchunguzi na ufuatiliaji kwa kuhusisha Kamisheni mbalimbali zilizomo ndani ya Jeshi la Polisi na wananchi kwa ujumla na kubaini hayo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo uchunguzi wa kina ulipofanywa ulibaini kuwa aliyefanya tukio hilo ni mtoto wa marehemu aitwaye Juma Ramadhan miaka 21 ambapo mtuhumiwa alikamatwa maeneo Msufini Msoga na baada ya mahojiano ya kina alieleza jinsi alivyomuua baba yake na kumfukia baada ya kuchimba shimo kwenye moja ya chumba cha nyumba yake.

Sababu halisi za mtuhumiwa kufanya tukio hilo la kinyama bado zinachunguzwa huku Polisi Dar es Salaam likilaani kwa nguvu kubwa tukio hilo na mengine ya kijinai na kusisitiza kuwa wote wanaojihusisha na matukio ya kihalifu ushahidi unapokuwa umekusanywa watakamatwa na kushughulikiwa vikali kwa mujibu wa sheria.
 
Back
Top Bottom