Nimeisoma story yote ila kuna kitu sijaelewa, ni kwanini ulikuwa unalilia sana? Ni nini kilichokuwa kinakuliza? Tokea mwanzoni huyo Angel alionyesha kutokukupenda, bado ukalazimisha, sasa ni kwanini ujilize pale yalipojitokeza ambayo yanatarajiwa kufanywa na mtu yeyote asie na mapenzi na mtu? Ni obvious kuwa ulijua hakupendi.
Umeonyesha undezi/Unyonge sana kwa mtu mzima alieyaona maisha yalivyo.
Mwanamke kukukataa wakati mwingine ina faida yake kwani inaepusha lawama ya kumuacha na pia inakupa nafasi ya kuexplore na kukutana na wengine wazuri zaidi. Huyo Angel hakuwa na kosa, ulimlazimisha tu.