Safari ya kuitafuta hekima-falsafa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Safari ya kuitafuta hekima-falsafa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mzee Mwafrika, Dec 19, 2009.

 1. M

  Mzee Mwafrika Senior Member

  #1
  Dec 19, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 168
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Falsafa ni nini?

  Ni vigumu sana kupata maana halisi ya neno "falsafa".Falsafa sio wazo:falsafa sio maono:falsafa sio njia ya kufikiri:falsafa ni tofauti ya hivi vyote.

  Falsafa ni mapenzi ya hekima:ni safari ya kuitafuta hekima.Katika safari hii yakupasa kutafakari kila kitu na kuvijaribu kupitia mazungumzo na majibizano(discussion):Falsafa haitaki uwakili wa kile unachokiamini bali utetezi wa kweli.

  Yawezekana umeianza hii safari pasipo kufahamu:Umeshawahi kujiuliza haya maswali(au yafanayo na haya)?

  • Je kuna uwepo wa Mungu?nini maana ya maisha?-dini
  • Kuna uwezekano wa kusimama kwa muda?-sayansi
  • Je demokrasia ni mfumo mzuri wa kuendesha serikali?-Siasa
  • sheria zipi zafaa kuongoza jamii fulani? n.k
  kama ndio basi kuna uwezekano umeshaianza safari hii!

  Hii ni thread maalumu kwa wanafalsafa wachanga;wakongwe na wale wenye wapenzi ya hekima kujifunza na kupeana mawazo mapya pamoja na kubadilishana nondoz zinazohusiana na falsafa.Karibuni sana akina Bruley,mwanakijijji,companero na wengine wote tupikane.

  Mimi nimejikita hasa kwenye Metafizikia maana napenda kujua zaidi masuala kuhusu imani na uwepo wa Mungu.karibuni wote!!
   
 2. M

  Mzee Mwafrika Senior Member

  #2
  Dec 19, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 168
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  "one cannot be said to know something just b'se one beleives it:knowledge is distinguished from belief by justification"
   
 3. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nakupa pole sana mzee mwafroka.

  nani kakudanganya hapa kuna watu wanaweza kujadili falsafa? hapa watu wanataka mambo ya kwenye mikeka ya vibarazzani. we anzisha hapa thread ya mambo ya "wapwa", "tusker baridi" na "mabikira" uone jeshi la wachangiaji litakavyofumuka.

  juzi nguli alianzisha thread ambayo haikuwa na content bali kichwa cha habari tu kisemacho"eti mtu wa kwanza kufanya ngono na mwanamke ana access siku zote hata kama mwamnamke yule kaolewa" alikusanya uwanja mzima wa wana JF na sijui amepewa thanks ngapi?

  haya ndo wana JF wanataka. sana sana ukitoka nje kidogo, ujadili mambo ya zito.

  hiyo metafizikia uliyogusia hapo juu unadhani wangapi wanaweza hata kukuambia ni mnyama gani????

  hakuna great thinkers hapa!!!!!!!!!
   
 4. M

  Mzee Mwafrika Senior Member

  #4
  Dec 19, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 168
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  mkuu nimekubali!
   
 5. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  unajua mi nimeishawaelewa hawa wanaochangia hapa JF. kuna wengine wameishajuana na wanachangiana kuungana mkono hata kwa mambo ya kipuuzi kabisa. kuna wengine wanatoka kwenye kujadili suala la msingi wanaanza kuchati masuala yao binafsi nje ya mada, hivyo wanwachanganya watu makini wanaofuatilia hoja inavyojadiliwa.

  Mimi binafsi napenda sana mambo yanayojenga na kuimarisha maarifa, ningependa sana kufuatilia mjadala wa thread yako mpaka mwisho. Mimi binafsi sijajikita sana katika falsafa, lakini ninaweza kubaini mtazamo Fulani unafuata falsafa gani. hivyo utaona kama tungekuwa na great thinkers wa kweli, sie wengine tungefaidika sana kwa kufuatilia michango hapa jamvini

  inasikitisha sana
   
 6. epigenetics

  epigenetics JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2009
  Joined: May 25, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45

  ukifanya tathmini ya chapchap, utaona kuwa jukwaa la elimu lina posts kidogo mno ukilimganisha na jukwaa la mapenzi, celebrities, sports, habari etc
  it is just the way our society is shaped, magazeti ya udaku and soft news ndio kipenzi cha watanzania wengi. ni watu wachache mno wanasoma magazeti kama RAI, au kuingia online na kutembelea site zenye kuprovoke critical thinking...
  revolution inahitajika nchini, hasa hasa kuhusu swala la elimu. hapa nipo naandika proposal ya kuja TZ kuhamasisha public understanding of Science and the world around them,. kaeni chonjo wadau wa TBC
   
 7. Companero

  Companero Platinum Member

  #7
  Dec 20, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  badala ya kuja kufanya sayansi unakuja kuhamasisha!
   
 8. epigenetics

  epigenetics JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2009
  Joined: May 25, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  inabidi watu kuhamasishwa kwanza in masses, kabla ya kuanza kufanya sayansi ya maana yenye kuleta innovation ktk biomedicine, environmental microbiology, biotech etc. huwezi fanya sayansi TZ bila kuwa na personell wa kutosha na wenye motisha. Vijana wengi wenye vipaji wameenda kusoma Accounting, Finance, na Journalism huku kozi za sayansi na uhandisi haziko kwenye "fashen"
   
 9. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #9
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
 10. M

  Mzee Mwafrika Senior Member

  #10
  Dec 20, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 168
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Bado mkuu ila nimeshafuatilia kidogo baadhi ya kazi zake na hasa maisha yake!yah one of the best katika karne iliyopita!nitachimba zaidi na nitarudi hapa tena.Nilikuwa napitia Arguments of God's existance katika mitandao mbali mbali,mtu wangu kuna watu wamezaliwa kufikiri na kama ufikiri basi umekufa!
   
 11. Companero

  Companero Platinum Member

  #11
  Dec 20, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hii miradi yenu ya kuhamasisha wananchi kwa kutafuna hela za wafadhili wa miradi ndiyo inayoilostisha nchi hii. Hivi Newton, Archimedes, Einstein na wengineo walisubiri fedha za wafadhili wa kuwahamasisha? Science happens when it is done and not just spoken about. Kama unataka sayansi njoo uifanye!
   
 12. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #12
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mbona hizi hata hapa tumezichambua sana.Ulipata wasaa wa kuzipitia?

  Mfano mmoja tu huu hapa chini

  https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/42260-why-i-am-not-a-christian-bertrand-russell.html
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Dec 20, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mi nilitegemea ungemtaja Mpemba and Co.
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  Dec 20, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,467
  Trophy Points: 280
  Asante Mzee Mwafrika, tangu ulipojoin JF mwaka 2007
  Na hiyo idadi ya posti zako, ndio unakuja leo kuwakaribisha kina Mzee Mwakijiji, Blueray, Campanero
  Na wengineo kuja kujadili falsafa?.

  Kweli nondo zote zinazopita JF huzioni, au kwa vile sio za metafizia, hakuona mambo ya freemasons humu!. Hukuona mambo ya Yoga humu?. Hukuona mambo ya Psychic humu?. Mind of Matter?. Life After life?. Metafizikia gani unayotafuta wewe?.
   
 15. M

  Mzee Mwafrika Senior Member

  #15
  Dec 20, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 168
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
 16. M

  Mzee Mwafrika Senior Member

  #16
  Dec 20, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 168
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  mkuu heshima yako!mara nyingi napenda kusoma sana na kufuatilia pasipo kuchangia kwa hiyo hizo hoja nilishafuatilia na nyingine nilitolea michango.Sitafuti Metaphysics hapa bali nimeonelea umuhimu wa kuwa na thread moja ya kuongozana hasa sisi wenye ugeni katika nyanja hii;hapa waweza bandika kitabu ama hata muongozo kusaidia wengine kama anavyofanya hapa bwana bruley na wengineo.Dhumuni ni kukumbushana kuhusu falsafa kwa ujumla.

  Hii sio thread yangu ni kwa wote wenye mapenzi ya hekima.
   
Loading...