Safari hii nampa kura yangu fisadi

mwananchit

JF-Expert Member
Oct 13, 2008
242
296
Jamani nimechoka, mwaka 1995 nilitapeliwa, niliuziwa mbuzi kwenye gunia baada ya kuletewa mmachinga mmoja nikaambiwa ni mr. clean na bila hiana nikatoa kura yangu. Matokeo, amekaa ikulu miaka 10 akaua viwanda vyangu, akauza benki yangu ya taifa na akafungua ya kwake, akaua shirika langu la bima ili afungue la kwake, akafungua kampuni kwa anuani ya ikulu na kujimilikisha migodi yangu mimi mpiga kura, akawa na kiburi cha ajabu na kuanza kuniita mchwara, akauza nyumba zangu zote akishirikiana na ma-padlocks. Siku hizi anatembelea magari ya tinted ili asizomewe kwa jinsi alivyochafuka, sasa eti amesafiri hadi Chato kumuibua another mr clean kama yeye! Sikubali.

Ok hayo yakapita ikaja 2005, nikaletewa malaika mwenye sura nzuri kutoka Msoga hana kitu chochote zaidi ya sura yenye mvuto. Akaja na ahadi kemkem za maisha bora kwa kila mtanzania lakini baada ya miaka mingine 10, amefanikiwa kutimiza hiyo ahadi kwa familia yake tu, taifa zima bado tunasubiria hizo ahadi. Tumeshuhudia mambo ya ajabu kama escrow, utapeli kwenye bomba la gesi na mikataba ya kuchimba madini, gesi, nk.

Safari hii sifanganyiki, hawa ninaoletewa wanaoitwa wasafi halafu nikishawapa kura yangu wananiliza, wanasema kwamba kwa miaka yote 10 waliwasahau wazazi wangu wakulima, wanachomoka na mali zangu mimi mpiga kura, halafu hawataki hata niwaulize chochote.

Safari hii nimebadilisha mawazo. NAMCHAGUA FISADI maana yeye sitamshangaa akiniibia maana mmeshasema kwamba ni fisadi. Naumia sana ninaposhawishiwa kumchagua "msafi" halafu ananiibia. SAFARI HII SIDANGANYIKI, NAMCHAGUA FISADI.
 
Jamani, nimechoka. Mwaka 1995 nilitapeliwa. Niliuziwa mbuzi kwenye gunia baada ya kuletewa mmachinga mmoja nikaambiwa ni Mr. Clean, na bila hiana nikatoa kura yangu. Matokeo, amekaa ikulu miaka 10 akaua viwanda vyangu, akauza benki yangu ya taifa na akafungua ya kwake.

Akaua shirika langu la bima ili afungue la kwake, akafungua kampuni kwa anuani ya ikulu na kujimilikisha migodi yangu mimi mpiga kura, akawa na kiburi cha ajabu na kuanza kuniita mchwara, akauza nyumba zangu zote akishirikiana na ma-padlocks. Siku hizi anatembelea magari ya tinted ili asizomewe kwa jinsi alivyochafuka, sasa eti amesafiri hadi Chato kumuibua another Mr Clean kama yeye! Sikubali.

Ok, hayo yakapita, ikaja 2005. Nikaletewa malaika mwenye sura nzuri kutoka Msoga, hana kitu chochote zaidi ya sura yenye mvuto. Akaja na ahadi kemkem za maisha bora kwa kila Mtanzania, lakini baada ya miaka mingine 10, amefanikiwa kutimiza hiyo ahadi kwa familia yake tu, taifa zima bado tunasubiria hizo ahadi. Tumeshuhudia mambo ya ajabu kama Escrow, utapeli kwenye bomba la gesi na mikataba ya kuchimba madini, gesi, n.k.

Safari hii sifanganyiki. Hawa ninaoletewa wanaoitwa wasafi halafu nikishawapa kura yangu wananiliza, wanasema kwamba kwa miaka yote 10 waliwasahau wazazi wangu wakulima, wanachomoka na mali zangu mimi mpiga kura, halafu hawataki hata niwaulize chochote.

Safari hii nimebadilisha mawazo. NAMCHAGUA FISADI, maana yeye sitamshangaa akiniibia maana mmeshasema kwamba ni fisadi. Naumia sana ninaposhawishiwa kumchagua "msafi" halafu ananiibia.

SAFARI HII SIDANGANYIKI, NAMCHAGUA FISADI.
 
Kwani nyoka akiingia ndani ya nyumba yako, unachagua fimbo ya kumpigia ? Nadhani unampiga na chochote kilicho karibu ambacho unamini kuwa kitamuua.:laser: Lengo ni kuindoa CCM na mfumo wake kwa kutumia njia yoyote halali ambayo ni uchaguzi.
 
Mkuu, naona unajua kufikiri logically ahahahah,

Hata Uhuru aliitwa fisadi na kweli ni tajiri lakini pia akaongezewa na muuaji, lakini jamaa alikuwa mvumilivu mpaka akaonekana mwenye huzuni hata siku ya mdahalo! Wakenya wakamhurumia wakampa kura! Sasa hivi Kenya inasonga mbele maana jamaa anawaheshimu wananchi wake sana! Tunataka mtu anayewaheshimu Watanzania, sio maigizo ya CCM!
 
Mwananchit:

UFISADI ni mfumo na sera ya CCM, hata wewe ukiingia CCM tu unakua fisadi bila kupenda, ona mzee Mkapa yaliyomkuta!

Kuna maKada wa CCM wengi tu miaka 10 iliyopita walikuwa shule wanasoma, lakini leo ni MATAJIRI wa kutisha tu, kisa wameingia kwenye mfumo 'system'.

Lowasa alijiuzulu uwaziri mkuu miaka 8 iliyopita, Je ESCROW, MABEHEWA, Meli za Kivita, Mikataba ya Gesi, Gharama za bomba la Gesi, Katiba mpya n.k vimezalishwa na nani??????

UFISADI ni CCM..... delete kabisa hiyo kitu.
 
Ahaaaaaa, mkuu hii imekaa safi sana. Tunamchagua fisadi sababu hao wasafi ndio wametuibia mpaka basi! Tukimchagua fisadi hata akiiba hatutushangaa sababu tumemchagua wenyewe.
 
Nafikiri we just have to sell our souls to the devil in order to uproot evils za system hii. Mi nitamchagua Lowassa na kiukweli akiwa ccm nilimpinga sana!
 
dah huu uzi umenihamasisha sana kupiga kura. tuko pamoja mwanawane kweli nyoka hachaguliwi fimbo ya kumuulia. yaani kwa sasa ccm kuiondoa lazima hata kama tutasimamisha mbuzi
 
Jamani, nimechoka. Mwaka 1995 nilitapeliwa. Niliuziwa mbuzi kwenye gunia baada ya kuletewa mmachinga mmoja nikaambiwa ni Mr. Clean, na bila hiana nikatoa kura yangu. Matokeo, amekaa ikulu miaka 10 akaua viwanda vyangu, akauza benki yangu ya taifa na akafungua ya kwake.

Akaua shirika langu la bima ili afungue la kwake, akafungua kampuni kwa anuani ya ikulu na kujimilikisha migodi yangu mimi mpiga kura, akawa na kiburi cha ajabu na kuanza kuniita mchwara, akauza nyumba zangu zote akishirikiana na ma-padlocks. Siku hizi anatembelea magari ya tinted ili asizomewe kwa jinsi alivyochafuka, sasa eti amesafiri hadi Chato kumuibua another Mr Clean kama yeye! Sikubali.

Ok, hayo yakapita, ikaja 2005. Nikaletewa malaika mwenye sura nzuri kutoka Msoga, hana kitu chochote zaidi ya sura yenye mvuto. Akaja na ahadi kemkem za maisha bora kwa kila Mtanzania, lakini baada ya miaka mingine 10, amefanikiwa kutimiza hiyo ahadi kwa familia yake tu, taifa zima bado tunasubiria hizo ahadi. Tumeshuhudia mambo ya ajabu kama Escrow, utapeli kwenye bomba la gesi na mikataba ya kuchimba madini, gesi, n.k.

Safari hii sifanganyiki. Hawa ninaoletewa wanaoitwa wasafi halafu nikishawapa kura yangu wananiliza, wanasema kwamba kwa miaka yote 10 waliwasahau wazazi wangu wakulima, wanachomoka na mali zangu mimi mpiga kura, halafu hawataki hata niwaulize chochote.

Safari hii nimebadilisha mawazo. NAMCHAGUA FISADI, maana yeye sitamshangaa akiniibia maana mmeshasema kwamba ni fisadi. Naumia sana ninaposhawishiwa kumchagua "msafi" halafu ananiibia.

SAFARI HII SIDANGANYIKI, NAMCHAGUA FISADI.
Ina maaana hakukuwa na mtu safi katika ukawa kutoka kwenye vyama vyote hivyo wa kumsimamisha mpaka mumchukue mtoto wa jirani ambaye kafukuzwa na baba yake. Hapa kuna tatizo kubwa na Mtaja lijutia huko mbele.
 
Nchi hii ya ajabu sana, eti naye Rizi1 anataka kutuchagulia Rais!!! Sasa tumechoka, Ole wenu mnaokula vinono kupitia CCM, wenye nchi wamechukia.

Karibu Lowassa na wote wenye wito wa kuliondoa joka kuu. Lowassa tunajua unafahamu LIKICHWA la joka kuu lilipo, mwenye mshale sawa, mwenye shoka, mwenye upinde, mwenye polinium, mwenye SMG,.... wote njooni tupige kichwa, uaaaaaaaaa kabisa hili JOKA.
 
Back
Top Bottom