Siri ya sifuri
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 2,621
- 2,273
Binafsi yangu napenda sana kuangalia channel inayotangaza masuala ya utalii nchini, ni channel nzuri na ninahakika inawavutia wengi, pongezi ziwaendee waanzilishi wake. wakati ukiangalia pichanzuri za maisha ya wanyama mara kwa mara zinasimamishwa kupisha matangazo mengine, moja ya matangazo hayo linaonesha picha zinazovuta hisia kua ni asili ya mwanaadam, picha za mnyama Sokwe zinazoonyesha akibadilika taratibu na kua mtu. Dhana hii ya kua mwanaadam ametokana na mnyama ni yazamani sana na imeshapingwa sana na wasomi wengi wa dunia yaleo. kiuhalisia dhana hii haina ukweli wowote na imeshapitwa na wakati, hamna sababu wala umuhimu wowote kwa safari channel kuendelea nayo, kwa upande wa imani(Dini)dhana hii ni kufuru kwa muumba na inaweza kusababisha kupungua kwa watazamaji kwa kiasi kikubwa. kwa maoni yangu ni vyema kuachana nayo.