Waberoya,
..Kikwete, Lowassa, Kinana, na Rostam, ndiyo washirika wakubwa ktk mtandao.
..sasa ni vipi watu wamng'ang'anie Lowassa peke yake huko hao wengine wakipeta?
..kama Richmond ingekuwa ni ya Lowassa basi angeondoka nayo baada ya kujiuzulu uwaziri mkuu.
..lakini Richmond imeendelea kuwepo hata baada ya hapo, na imetakaswa kwanza kwa kuuzwa kwa Dowans, na baadaye Symbion.
..yaani walichofanya hakina tofauti na kutakasa fedha chafu/ money laundering. lakini in this case wametakasa kampuni chafu--richmond-dowans-symbion.
..suala hili ni pana na kubwa kuliko tunavyolijadili hapa JF. naamini akipatikana mtu akachimba zaidi humo atakutana na mambo ya ajabu kabisa kuhusu RUSHWA, UZANDIKI, FITINA,MARAFIKI KUSALITIANA, etc etc. Wanaposema politics is a dirty game basi hatakiwa uangalie mbali zaidi ya hii kashfa ya richmond.
..mvurugano wote unaoendelea ktk siasa za Tanzania chanzo chake ni JK kumgeuka na kumdhulumu Lowassa ktk yamini waliyokula.
cc
Pasco,
Rev. Kishoka,
Nguruvi3,
Kimweri,
Eric Cartman, Ocampo four
Mkuu sisi Watanzania bi viumbe wa aina yake. Tunaweza kuchezewa akili na wajanja kadri wanavojisikia
Juzi , kiongozi aliyepewa dhamana ya mali na watu wa nchi hii naye kajiunga katika treni la Richmond akilalamika
Kwamba, mwenye Richmond anaongozana na Lissu. Hapa kunasikitisha sana, hivi kweli kauli hii ilipaswa kutolewa na mtu aliyekabidhiwa nchi , mali na watu wake. Kwamba naye anapita akilalamika kama sisi
Pili, Watanzania wanaposema Richmond ni Lowassa, wangeenda mbali na kujiuliza.
Hivi Mwakyembe aliyesema mambo mengine ameyaacha kutoivua nguo serikali, aliacha nini? Hicho ndicho tunatakiwa tujue
Tatu, Sitta alizuia mjadala ule usirudiwe bungeni kuweka ukweli. Watanzania hawamuulizi kwanini alizuia
Nne, CCM wanaolalamika wamekaa na Lowassa huyu miaka yote kasoro miezi miwili iliyopita.
Hakuna mahali wamechukua hatua za kichama kutokana na tuhuma hizo tena wakiwa na serikali.
Walimchagua awe mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya taifa. Kamati nzito sana ndani ya bunge
CCM hao hao wakampitisha akawa mbunge. Na CCM hao hao wakampa nafasi ya kuchukua fomu
Leo CCM hao hao wanaiona Richmond kwa jicho chongo. Hawamuulizi mwenyekiti wa chama chao, anawaachaje na Richmond?
Nani wapo nyuma ya Richmond ? CCM wanaaminisha watu kuwa Richmond ni ya mtu na si mtandao mpana
Mkuu, nikuonyeshe jinsi Watanzania tunavyolaghaiwa na hawa watu.
Juzi Morogoro, YUsuph Mamkamba amesema Sumaye ni Kabaila kwasababu amenyang'anya watu mashamba na kujimilikisha
Huko nyuma, Yusuph akiwa katibu mkuu wa CCM na Mkapa akiwa Mwenyekiti, wananchi waliwahi kuuliza hilo swali
Mkapa akasema '...wanamwandama waziri mkuu wangu bila sababu''
Huyo aliyemtetea Sumaye ni mwenyekiti wa CCM akiwa na katibu mkuu wa CCM Bwana Mkamba
Leo Makamba ndio anaona tatizo. Ndivyo ilivyo Richmond. Wote walikuwemo leo wanatuaminisha wao ni wasafi na hilo ni zigo la Lowassa.
Hakuwambuki kuwa aliyeisafisha Richmond kupitia Dowans ni mwenyekiti wa CCM tena kijana wa Yusuph alipiga debe sana kupitia kamati ya nishati ya bunge.
Tusiangalie tulipoangukia, tuangalie tumejikwaa wapi. Richmond ina mikono mingi mizito , tunachezewa shere ili tubabaike na kuzungusha vidole haraka tukiaminishwa ni mazingaombwe