Saed Kubenea: Rostam kinara wa Dowans

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,531
Anajuana na Dowans, Kagoda

Serikali yamwangalia tu Rostam Aziz

MWANASIASA na mfanyabiashara Rostam Aziz ana siri kubwa kuhusu makampuni ya Dowans na Kagoda Agriculture Limited yanayotuhumiwa kwa kuhujumu uchumi. Dowans ambao imekuwa vigumu kujua makazi ya ofisi zao na maofisa wake wanaowasiliana na serikali, imekuwa kampuni kivuli kama ilivyo Kagoda.

Lakini Rostam Aziz alinukuliwa na vyombo vya habari wiki iliyopita akikiri kuwafahamu wamiliki wa kampuni ya Dowans iliyorithi mkataba wa kufua umeme wa Richmond.

Wakati Rostam anakiri kufahamu wamiliki wa Dowans, kwa madai kwamba aliwahi kuwaomba kazi, taarifa zilizopo zinamtaja mfanyabiashara huyo kuwa na mkono katika mkakati wa kukwapua zaidi ya Sh. 40 bilioni kutoka Benki Kuu (BoT) kwa jina la Kagoda. Kwa mujibu wa taarifa za Wakala wa Usajili wa Makapuni nchini (BRELA), wenye hisa wote wa Dowans wana anwani za nje ya nchi za Costa Rica na Singapore.

Wenye hisa katika kampuni hiyo ni Dowans Holdings SA ya Avenida de la Rosas 3J; CALLE BLANCOS, 1150 ya San Jose, Costa Rica wenye hisa 81. Wengine ni Portek Systems wenye hisa 19 na Equipment PTE Ltd., wenye hisa 35 na ambao wanatumia anwani moja ya 20 Harbour Drive,
#02 01 PSA VISTA ya Singapore. Hata hivyo ni Dowans Holdings SA ya Costa Rica ambayo hadi sasa imefahamika kutokuwa na ofisi nchini humo; kutokuwa na gari, simu wala sanduku la barua.

Kukiri kwa Rostam kufahamu wamiliki wa Dowans kunamfanya awe mtu muhimu nchini katika kuchunguza tuhuma zinazokabili kampuni hiyo. Aidha, mmoja wa wafanyakazi katika kampuni ya Rostam Aziz ya Caspian, anadaiwa kuwa mmoja wa watia saini kwenye hundi za malipo yaliyofanywa kwa kampuni ya Zakhem Contractors Limited ya Mbagala, Dar es Salaam iliyojenga msingi wa kuweka mashine za Richmond/Dowans.

Gazeti hili liliwahi kuchapisha kivuli cha moja ya hundi mbili zilizolipwa kwa Zakhem kupitia EuroAfrica Bank (sasa BOA Bank) ambako, hata hivyo, zilirejeshwa bila kulipwa kwa maelezo kuwa akaunti haikuwa na fedha.
Ni Rostam huyohuyo ambaye imethibitika kuwa mmoja wa wafanyakazi wake, John Kyomuhendo, alikuwa mmoja wa waanzilishi wa kampuni ya Kagoda ambayo ilichota mabilioni ya shilingi kutoka BoT.

Namba ya kiwanja na kitalu, Na 87 katika eneo la viwanda Kipawa (Industrial Area) zilizotajwa kuwa makazi ya Kagoda, hazipo kwenye ramani ya jiji. Wiki mbili zilizopita, wakili Bhyidinka Michael Sanze alinukuliwa na gazeti hili, katika andishi maalum kwa Kamati ya Rais kuhusu wizi kwenye akaunti ya madeni ya nje (EPA), akimtaja Rostam kuwa mtu muhimu katika ukwapuaji wa mabilioni benki.

Sanze alieleza kwa maandishi kuwa aliitwa na Rostam katika ofisi yake iliyoko Mirambo 50 jijini Dar es Salaam, ambako aliambiwa na wakili wake kiongozi, Bered Malegesi kusaini mkataba wa Kagoda wa kuchota mabilioni ya shilingi kutoka BoT. Kwa mujibu wa Sanze, katika ofisi ya Rostam alikuwemo pia Peter Noni ambaye hivi sasa ni Mkurugenzi wa Mipango Kimkakati wa BoT na shahidi wa serikali katika kesi za ufisadi.

Alisema Rostam alimweleza kuwa ni rais mstaafu Benjamin Mkapa aliyeagiza fedha hizo zichotwe na kukabidhiwa kwake (Rostam) kwa ajili ya kusaidia CCM katika uchaguzi mkuu wa 2005. Tangu kutangazwa kwa taarifa hizo, si Rostam wala yeyote aliyetajwa katika andishi la Sanze amejitokeza kukana. Kwa ushahidi uliopo, na kwa kuzingatia kukiri kwake, Rostam ana uhusiano wa karibu na Dowans, Richmond na Kagoda, makampuni ambayo wananchi wanalia nayo kuhusu ufukarishaji wa nchi.

Vilevile Rostam anatajwa kuwa mfuatiliaji mkuu wa malipo ya Richmond/Dowans kutoka Hazina na BoT kila alipoona malipo yanacheleweshwa. Bali hakuna ushahidi wowote kuhusu juhudi za serikali kutumia mtu huyu, mwenye ukaribu na makampuni haya ya kifisadi, kuchunguza na hata kurejesha asilimia ndogo tu ya fedha zilizoibwa.

Kwa wiki nzima, gazeti limekuwa likimtafuta Rostam kupata kauli yake, lakini simu yake ya mkononi, Na. 0754 555555 imekuwa ikijibu kuwa hapatikani. Hata ujumbe wa maandishi uliopelekwa kwake haukujibiwa ingawa ulionyesha kuwa ulipokelewa.

"Huo ndio umaarufu wa Rostam; biashara zake zenyewe hazionekani lakini yuko kila mahali penye shina la fedha," ameeleza mmoja wa wafanyabiashara wakubwa jijini Dar es Salaam. Kutoonekana kwa Rostam katika maandishi kuhusu umiliki wa makampuni ya Kagoda, Richmond na Dowans, kumeelezwa kuwa siyo jambo la bahati mbaya kwake.

Rostam Aziz haonekani hata katika New Habari Group iliyonunua kampuni ya Habari Corporation, wachapishaji wa magazeti ya Rai, Dimba, Mtanzania, Bingwa na The African.

Lakini ni Rostam anayetajwa na kufahamika kuwa mmiliki wa kampuni hiyo; mwenye mamlaka ya kuteua na kuajiri menejimenti; kuajiri na kulipa wafanyakazi.
 
Kwa waliofanikiwa kufuatilia ITV live uzinduzi wa kampeni za ubunge wa Ubungo za Saed Kubenea kuna hoja mpya kabisa Saed Kubenea aliibua, Eti Samwel Sitta kuna report yenyewe 'original' kuhusu Richmond aliifungia kwenye briefcase na Mwakyembe na kamati yake hawawezi kuaminika.

Sasa angalia gazeti lifuatalo la MwanaHalisi toleo Na.227 Jumatano, February, 2011 ambalo front page tu bila hata kulinunua unajua tu kuwa Rostam Aziz ndiye mumiliki wa Dowans ambayo ilipewa kienyeji mkataba wa kufua umeme na kampuni feki ya Richmond Development Company LLC na baadaye kuunganishwa kienyeji na Tanesco.

Sasa nani hastahili kuaminika Kubenea au Mwakyembe? Sasa kubenea kama uliweza kutuchapia haya yote yaliyo kwenye gazeti hili, nini kilikuzuia usituchapie na hiyo report ambayo Sitta aliificha maana wewe unaijua na kama hauijui huwezi kujua kama ilifichwa.
 
Waberoya,

..Kikwete, Lowassa, Kinana, na Rostam, ndiyo washirika wakubwa ktk mtandao.

..sasa ni vipi watu wamng'ang'anie Lowassa peke yake huko hao wengine wakipeta?

..kama Richmond ingekuwa ni ya Lowassa basi angeondoka nayo baada ya kujiuzulu uwaziri mkuu.

..lakini Richmond imeendelea kuwepo hata baada ya hapo, na imetakaswa kwanza kwa kuuzwa kwa Dowans, na baadaye Symbion.

..yaani walichofanya hakina tofauti na kutakasa fedha chafu/ money laundering. lakini in this case wametakasa kampuni chafu--richmond-dowans-symbion.

..suala hili ni pana na kubwa kuliko tunavyolijadili hapa JF. naamini akipatikana mtu akachimba zaidi humo atakutana na mambo ya ajabu kabisa kuhusu RUSHWA, UZANDIKI, FITINA,MARAFIKI KUSALITIANA, etc etc. Wanaposema politics is a dirty game basi hatakiwa uangalie mbali zaidi ya hii kashfa ya richmond.

..mvurugano wote unaoendelea ktk siasa za Tanzania chanzo chake ni JK kumgeuka na kumdhulumu Lowassa ktk yamini waliyokula.

cc Pasco, Rev. Kishoka, Nguruvi3, Kimweri, Eric Cartman, Ocampo four
 
Last edited by a moderator:
Haiwezi kutuondoa UKAWA mpk kieleweke nyambavu zenu na buku.seven zenu
 
Kwa waliofanikiwa kufuatilia ITV live uzinduzi wa kampeni za ubunge wa Ubungo za Saed Kubenea kuna hoja mpya kabisa Saed Kubenea aliibua, Eti Samwel Sitta kuna report yenyewe 'original' kuhusu Richmond aliifungia kwenye briefcase na Mwakyembe na kamati yake hawawezi kuaminika. Sasa angalia gazeti lifuatalo la MwanaHalisi toleo Na.227 Jumatano, February, 2011 ambalo front page tu bila hata kulinunua unajua tu kuwa Rostam Aziz ndiye mumiliki wa Dowans ambayo ilipewa kienyeji mkataba wa kufua umeme na kampuni feki ya Richmond Development Company LLC na baadaye kuunganishwa kienyeji na Tanesco. Sasa nani hastahili kuaminika Kubenea au Mwakyembe? Sasa kubenea kama uliweza kutuchapia haya yote yaliyo kwenye gazeti hili, nini kilikuzuia usituchapie na hiyo report ambayo Sitta aliificha maana wewe unaijua na kama hauijui huwezi kujua kama ilifichwa.

Mbona ujaelezea na hiyo habari ingine hapo chini.inayo sema sifuri zingine wenyewe Kikwete na Lowasa. Na wasi wasi na wewe kama sio gamba.unataka kutuingiza mkenge !!??
 
Kubenea ni moja kati ya waandishi maKanjanja wa hali ya juu kuwahi kutokea hapa TZ Magazeti yake ya Mwanahalisi na Mawio hayawezi kuwa vya kuaminika kwa habari nyeti kama hizo.
 
Tatizo la watanzania ni IQ ndogo tu, kila jambo la kitaifa linatafsiriwa kichama ndio maana nchi haiendi. Kama kubenea sasa hivi yuko sahihi maana yake ni kuwa habari alizokuwa anaandika kwenye magazeti yake ni uongo, na kama ndivyo basi alikuwa ni mchochezi na kufungiwa kwa gazeti la mwanahalisi ilikuwa ni haki yake.
 
Waberoya,

..Kikwete, Lowassa, Kinana, na Rostam, ndiyo washirika wakubwa ktk mtandao.

..sasa ni vipi watu wamng'ang'anie Lowassa peke yake huko hao wengine wakipeta?

..kama Richmond ingekuwa ni ya Lowassa basi angeondoka nayo baada ya kujiuzulu uwaziri mkuu.

..lakini Richmond imeendelea kuwepo hata baada ya hapo, na imetakaswa kwanza kwa kuuzwa kwa Dowans, na baadaye Symbion.

..yaani walichofanya hakina tofauti na kutakasa fedha chafu/ money laundering. lakini in this case wametakasa kampuni chafu--richmond-dowans-symbion.

..suala hili ni pana na kubwa kuliko tunavyolijadili hapa JF. naamini akipatikana mtu akachimba zaidi humo atakutana na mambo ya ajabu kabisa kuhusu RUSHWA, UZANDIKI, FITINA,MARAFIKI KUSALITIANA, etc etc. Wanaposema politics is a dirty game basi hatakiwa uangalie mbali zaidi ya hii kashfa ya richmond.

..mvurugano wote unaoendelea ktk siasa za Tanzania chanzo chake ni JK kumgeuka na kumdhulumu Lowassa ktk yamini waliyokula.

cc Pasco, Rev. Kishoka, Nguruvi3, Kimweri, Eric Cartman, Ocampo four

niyamini gani hiyo waliyokula. inawezekana unataarifa sahihi. hebu funguka zaidi mkuu.
 
...exactly joka.....na kwa kuongezea tu ni kwamba katika ushirika wao (mtandao) sasa wamegawanyika kuwa timu mbili zinazokinzana.....yaani timu JK na Kinana na team Lowassa na Rostam.....wakati wa kumweka JK madarakani hawa wote walikuwa timu moja.....lakini sasa wamegawanyika kuwa timu mbili pinzani...na matokeo yake ndicho tunachoona TZ....Labda niseme tu kuwa timu JK na Kinana wanaweza kuwa na upper hand kwenye mtifuano huu...maana wana access na state machinery zooote...ila team Lowassa na Rostam wao mtaji wao ni nguvu ya umma.....tusubiri mengi kwenye vita hii...maana sioni JK akikubali kukabidhi nchi....pale nguvu ya umma itakapoonekana kutamalaki....
 
Kubenea, aibu kwake na vizazi vyake vyote!

maandishi hayafutiki

binafsi namuona huyo jamaa kama kachanganyikiwa vile. angekuwa silence tu kama wenzake akina mbowe, msigwa, lisu, mnyika walivyofanya. au kama anataka kuliendeleza basi angekuwa kama slaa basi tujue moja. jamaa anaonekana ni zaidi ya mbabaishaji.
 
Nnachojua raisi ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri na mkataba wa richmond uliridhiwa na baraza la mawaziri lowassa aketakaje kuuvunja mkataba km ananufaika na kwa nn alipigwa stop
 
niyamini gani hiyo waliyokula. inawezekana unataarifa sahihi. hebu funguka zaidi mkuu.

..hawa wameanza harakati zao zamani

..mwaka 95 walikuwa pamoja, ila Mwalimu aliwazidi maarifa wote wawili.

..sasa waliendelea kushikamana mpaka walipodhulumiana kwenye richmond.

..95 Lowassa alikuwa na support kubwa zaidi. Jk alikuwa kama msindikizaji tu.

..yamini waliyokula ni kusaidiana ktk harakati zao za kisiasa.

..mtu wao mwingine wa karibu alikuwa capt.ukiwaona ramadhani mwinshehe ditopile mzuzuri.

nb.

..kuna uvumi kwamba plan b ya jk mwaka 2005 ilikuwa kuhamia chadema.

..samuel sitta, mwanamtandao mwingine, naye according to dr.slaa ilikuwa agombee uraisi kupitia cdm mwaka 2010.
 
Back
Top Bottom