Saddam Hussein' Alipolazimishwa Kucheza Video ya Ngono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Saddam Hussein' Alipolazimishwa Kucheza Video ya Ngono

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Oct 23, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: ecxMsoNormalTable, width: 393"]
  <tbody>[TR]
  [TD="width: 393, colspan: 3"]'Saddam Hussein' Alipolazimishwa Kucheza Video ya Ngono[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 200, bgcolor: #E1E1E1"]
  [​IMG]
  Raia wa Misri, Mohamed Bishr ambaye kufanana kwake na Saddam Hussein kunamletea matatizo[/TD]
  [TD="width: 253, bgcolor: #E1E1E1"]Sunday, October 09, 2011 7:17 PM
  Raia wa Misri anayefanana sana na aliyekuwa rais wa Iraq, Saddam Hussein amenusurika kuuliwa baada ya kuwatoroka watu waliomteka na kisha kumlazimisha acheze video ya ngono ili baadae video hiyo iuzwe kwa vyombo vya habari ikidaiwa kuwa ni video ya kweli ya Saddam Hussein.
  [/TD]
  [TD="bgcolor: #E1E1E1"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 393, colspan: 3"]Raia wa Misri, Mohamed Bishr alipigwa na kujeruhiwa vibaya sana na kundi la watu toka Iraq lilipomteka kisha kumlazimisha ashiriki kwenye video ya ngono ili baadae video hiyo iuzwe kwenye vyombo vya habari vya magharibi ikitajwa kama video ya ngono iliyopatikana kwenye nyumba ya aliyekuwa rais wa Iraq, Saddam Hussein.

  Bishr anafanana sana na Saddam Hussein kiasi cha hata raia wa Iraq nchini Misri
  kuamini kuwa yeye ndiye Saddam wa ukweli na amejificha nchini Misri.

  Bishr akiwa amelazwa hospitali kwenye mji wa Alexandria, alisema kuwa alikuwa akienda kazini siku ya jumapili wakati kundi la watu watatu wenye silaha walipomvamia kumlazimisha aingie kwenye gari lao.

  "Wanaume watatu wenye bunduki walinilazimisha nishuke kwenye gari langu niingie kwenye gari lao huku wakinipiga", alisema Bishr ambaye ni muumini safi wa kiislamu alipokuwa akiongea na gazeti la Ahram.

  Bishr alisema kuwa watu hao walimlazimisha ashiriki video ya ngono ili baadae video hiyo iuzwe kwa pesa nyingi watu wakidanganywa kuwa ni ya aliyekuwa rais wa Iraq, Saddam Hussein ambaye alinyongwa mwaka 2006.

  Alipokataa alipigwa sana na kisha kutupwa pembeni ya barabara.

  Mtoto wa Bishr aliyejulikana kwa jina la Mahmoud, alisema kuwa wiki chache zilizopita baba yake alifuatwa na kundi la wanaume raia wa Iraq ambao walimtaka ashiriki video ya ngono kwa malipo ya paundi za Msiri milioni 2 ambazo ni sawa na dola laki tatu na nusu za Marekani. Bishr alikataa ofa hiyo.

  Hii si mara ya kwanza Bishr kushambuliwa kutokana na kufanana kwake na Saddam Hussein.

  Hadi sasa Bishr ameishabadilisha makazi yake mara nne ili kuepuka kero za watu wanaodhania yeye ni Saddam Hussein.

  "Tuliwaomba polisi wamuwekee ulinzi baba yetu kwakuwa tatizo kama hili limekuwa likitokea mara kwa mara", alisema Mahmoud.
  [/TD]
  [/TR]
  </tbody>[/TABLE]
  image002.jpg

  [TABLE="class: ecxMsoNormalTable, width: 393"]
  <tbody>[TR]
  [TD]Sunday, October 09, 2011 7:17 PM
  Raia wa Misri anayefanana sana na aliyekuwa rais wa Iraq, Saddam Hussein amenusurika kuuliwa baada ya kuwatoroka watu waliomteka na kisha kumlazimisha acheze video ya ngono ili baadae video hiyo iuzwe kwa vyombo vya habari ikidaiwa kuwa ni video ya kweli ya Saddam Hussein.

  [/TD]
  [/TR]
  </tbody>[/TABLE]
   
 2. Bambanza jr.

  Bambanza jr. JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2011
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mm pia ni muathirika wa kufananishwa, mtaani watu wananiita jk, siku moja kwnye daladala jamaa1 aliniita fisadi. ''wengine watoto wa wa kubwa alafu mnapanda daladala, au ndo kuonyesha mnatupenda wakat hal yetu ngumu, fisadi mkubwa ww'' nlijisikia vibaya ila nilkausha tu, nnakereka sana kwan mm sina uhusiano wowote na akina riz one.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Ujichunge mkuu usitembee mitaa ya wahuni au wabakaji watakupiga ile mbaya uwe muangalifu sana
   
 4. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  kazi kweli
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ni bora huyo aliyefananishwa na Sadam kuliko ufananishwe na EL.
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Duh kweli jamaa linafanana na Saadam Hussein tatizo la waarabu hawajui kutumia fursa vizuri.Huyu jamaa anafaa sana kuigiza filamu ya maisha ya Saadam Hussein.

  [​IMG]
   
Loading...