Mkuu Rwanda ni nchi ndogo sana kieneo, na population density yake ni kubwa sana - wakati mwingine huwa awataki Wanyarwanda walio kimbilia nchi za nje warudi kwao kwa sababu ya ukosefu wa aridhi ya kutosha, vile vile Kagame anajuwa fika kwamba Wahutu na WATWA wote wakirudi RWANDA kuna uwezekano mkubwa kuondolewa madarakani yeye na chama chake kwa hiyo matokeo yake anajihami masaa YOTE, anajuwa hayuko salama hata kidogo siyo kwa Wahutu tu hata Watutsi wenzake walio kuwa naye jeshini wakakimbilia nje baada ya kutoelewana naye kikazi.
Kwa kifupi chokochoko zake zinatokana na sababu kuu tatu: Sababu ya kwanza ni ARIDHI, wana mkakati wa kutafuta kisingizio cha kumega sehemu ya aridhi ya jirani zake - Jimbo la KIVU in particular: Sababu ya pili ambayo actually ndio ingekuwa ya kwanza, inahusu usalama wake na chama chake, ana wasi wasi sana na Wanyarwanda ambao wako uhamishoni hasa hasa Wahutu na Watutsi wanajeshi walio muhasi, anajuwa wakirudi Rwanda hana CHAKE tena :Sababu ya mwisho ni ndoto zao za siku nyingi za kutaka kuanzisha HIMA EMPIRE katika Great Lakes mawazo hayo bado wanayo HAYAJAFA. Onyo alilopewa na Viongozi kusini mwa Africa si bure hata nchi za Magharibi zimekwisha mshitukia hila kuna Wafrica wenzetu wenye mawazo ya mgando au wanao tumia msemo wa your imaginary enemy is my ENEMY wajifanya kumtetea bila kujuwa kwamba jamaa huyu ni hatari sana in East and central Africa akihanzisha vita vyake na agenda zake za siri hakuna ambaye atasalimika, Dunia nzima haiwezi kuwa inamsingizia bure Kagame - kuna KITU, mwenye macho ahabiwi TAZAMA. Mimi mchango wangu ndio huo mkuu.