Sad story of varsity student who failed to secure loan

Mi nafikiri kaka ungemshauri tu abadili course coz kwa maisha ya sasa watu wamchangie 4m na maisha ya sasa yalivyo dah naona dada ataishi maisha magumu sana dsm nafikiri aachane na law atafute temple afundishe na mwakani aombe education ili aweze pata elimu na kama atahitaji kusoma law akiwa na kazi ajiendeleze kutimiza ndoto yake if she is 20 yrs then still is young it take almost 7yrs that is my suggestion other wise maisha yatamshinda soon atakuwa miongoni mwa mademu watakao anikwa Jf wakiwa kwenye picha za uchi tukaanza kuwasifia kama si kuwaponda ndo taifa analotuandalia mkweere hapa piga ua uzalendo unaenda kwao huwezi nambia niwe mzalendo afu nashindwa kutimiza ndoto zangu. Kama anasimu ya huyu dada mpe ushauri huu.
 
tatizo kazi ya Mbunge sio hiyo na utatuzi huo wa suala hili si ung'amuzi wa ukubwa wa tatizo hili! Hebu fikiria wale 4000 waliobaki wenye tatizo kama hili nao Tibaijuka atawalipia au wabunge wao? kuwa na uwezo wa kuelewa ujumbe wa hii story hapa! uvumbuzi endelevu wa hili suala ni serikali kuingilia kati na kuongeza hela ya Mkopo! hivi ile change ya radar itapelekwa wapi vile? kwanini isiingizwe kwenye mfuko wa mikopo wa HESLB?

sio hivyo tu kaka wiki mbili zilizopita nilikuwa ninatizama taarifa ya habari ITV 'tena aliongea kiswahili balozi wa Ufaransa aliyekuwa anamaliza muda wake nukuu ''nchi yangu ya Ufaransa imeisamehe nchi ya Tanzania deni la dola bil. 21 pesa hizi zichangae elimu Tanzania'' mwisho wa kunukuu. Je kuna haja gani ya kuendelea kusikia maswali ya serikali haina fedha za kuwakopesha wanafunzi wa wakitanzania kugharimia masomo yao ya chuo kikuu? Na Vasco Da Gama kimya?
 
Bajeti imefika kikomo. Serikali kwa sasa inahangaika na kutatua tatizo la umeme kwanza.
 
Inasikitisha mno, kina Mama wa Bunge, Chama Cha Wanasheria wanawake, Mama Tibaijuka, hata Wanaume na Wanawake wengine walio viongozi na wasio viongozi, wanaoweza kumsaidia binti huyo, wasimtupe, wamsaidie ili na yeye aweze kuikomboa familia yake, Wanawake na Taifa kwa ujumla, viongozi wengi leo hii, enzi zile walisoma bure au kwa kuchangia kiasi kidogo sana cha pesa, baada ya kusoma na kufanikiwa kwao, wasiwasahau watoto wa masikini, asilimia kubwa ya hawa viongozi wetu walitokea kwenye familia masikini sana, hata viatu vya kuvaa kwendea hata shule, walikuwa hawana, wengi walivijua viatu miguuni mwao wakiwa Sekondari, lakini leo hii hawakumbuki wema waliofanyiwa naTanzania ya kipindi cha Nyerere na wakati wa wamissionari, wamekuwa na kiburi hata soksi na miswaki wananunua Ulaya, hivi hawa watu hawamuogopi Mungu, kweli shukrani ya punda mateke, wanaonaje kama wanashindwa kuchangishana pesa ili kuwasaidia hawa wanafunzi wanaotaabika na kuangusha machozi yao juu ya ardhi ya Tanzania, kwa sababu ya mioyo yao migumu, isiyojali na kuwahurumia wananchi wa Tanzania, basi wale mafisadi wafilisiwe ili hawa watoto wapate fedha za ada, malazi na matumizi mengine wanapokuwa Chuoni, sio kuanza kujiuza kwa Mashugadadi na Mashugamami ili waishi vizuri Vyuoni, tutapoteza nguvu kazi ya taifa kwa Ukimwi, ni nini tunataka wengi wao wakishafariki kwa Ukimwi, kuwaajiri Wageni au wale ambao wako bado Sekondari na shule za Msingi kama miaka ya 60, karne hii, si tutazidi kuwa masikini na kuchekwa na Dunia, au kama vipi, fisadi mmoja ama wawili wajitolee kuwasaidia hawa vijana ili hatimaye, Wananchi na Mungu wawasamehe kosa lao la ufisadi. Eeh!, Baba anayeshindwa kujitahidi kuwajali wanae na kuwapenda, ni Baba kweli, au ni Baba jina tu!, viongozi wa Tanzania vipi???!
 
Kwa mujibu wa HESLB, wanafunzi takriban elfu 37 (37,000) wanastahili kupata mkopo mwaka huu. Bodi ina uwezo wa kuwalipia wanafunzi takriban elfu 24 (24,000). Wengine wote waliobaki, yaani 37,000-24,000=13,000 hawatapata. Hakika huu ni utani.
Kwa taarifa ambazo sijathibitisha, Mke wa RIDHIWANI anaenda kusoma IR (Internatinal Relations) UDOM na kapewa mkopo. Inakuwaje?
 
Huyo Binti wala asiwe na hofu, amuone tu mbunge wake wa Muleba Prof Tibaijuka waziri wa Ardhi atamlipia tu. Anaweza hata akatoa toka shuleni kwake ile shule ghali saaana sijui yaitwa Bablojonson???

hiv kumuona huyo wazir n kaz ndogo??!!, na hawa viongoz wanavyojifanya miungu watu!
 
Its Sad story, to be honest i feel bad after thinking alot, this goverment sucks, Pia wadau wote tukumbuke kumshukuru mungu kwa opportunity alizotupa, nashindwa kuelewa vigezo walivyotumia, jirani yangu kuna dogo amemaliza form 6 na amepata div 3 point 15 amechaguliwa tumaini Law na amepata loan 3.7million na tena amesoma shaaban robert na anatoka familia ya geti kali yenye kila kitu, hapo ndo nashindwa kuelewa bodi wanatumia vigezo gani maana hata yeye haelewi imekuaje akapata loan aliomba kufata mkumbo baada ya kuona wenzake wana apply,

Enzi zetu ukipata div 1 au Two una uhakika wa kulamba boom hata uwe mtoto wa bakhresa but nowdays waliofaulu wanaambiwa budget exhausted wakati waliopata lowest pass marks wanapata mkopo
 
Huu mwaka HESLB wamefanya mambo ya ajabu na kibaya zaidi haya yote hatujui wameyaanza kuyapanga.Nakumbuka mwanzoni mwa mwezi wa tano kulikuwa na maonyesho ya vyuo vikuu pale ubungo plaza na waliopata nafasi kuudhulia sio wengi miongoni mwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita mwaka 2011,pale wawakilishi wa bodi ya mkopo(HESLB) waliongea na kusisitiza kuwa kwa yeyote aliyepata div 1 na 2 kwa masomo ya sanaa na sayansi basi huyo ana uhalali wa kupata mkopo bila kuhoji wala wasiwasi,pia akaongezea kusema kwa yeyote wa sayansi aliyepata div 3 na anaenda kusomea masomo ya sayansi chuo kikuu basi huyo nae atafaidi mkopo,pia akamalizia kwa kusema kwa yeyote ambaye amepata div 3 na anatarajia kusomea masomo ya sanaa na biashara akifika chuo basi huyo asijiangaishe kuomba mkopo.Ila sasa kilichotokea na kinyume na yale aliyoongea yule mwakilishi sasa sijui alikuwa chizi tu wamemuokota huko au kweli ni mwakilishi maana wenye div 1 ndo haswa waliochinjwa mikopo halafu div 3 wanaogelea tu na ela za bodi tena kunawatu wazima wamemaliza mwaka 1988 kidato cha nne nao wanafaidika na huu mkopo.
 
Hii nchi ya ajabu, na hii migazeti yetu, hamna hata moja linalotuwakilishia matatizo yetu, wao ni IGUNGA TU.
 
Until we stand up and join hands to fight for education rights of these poor 'kids' the government will never listen their cries.
 
Back
Top Bottom