Sababu zinazopelekea kondakta kuruka wakati anakusanya nauli

bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
1,134
2,010
Habari wanajamii wenzangu.

Kama kichwa kinavyojieleza nimepanga kuongelea juu ya dalili za kuangalia kwa kondata pale unapokua abira ndani ya daladala zetu ili kuzuia kitendo cha konda kukuruka akiwa anakusanya nauli hivyo kupelekea konda kukosa mapato anayostahili.

Kwanza kabla sijaingia ndani kabisa napenda kuweka bayana ustarabu wa kuzingatia kama abiria, Endapo umekosa siti basi simama upande upande ili wewe na wenzako muweze kujipanga vizuri kama ndizi kwenye mkungu ni jambo la kustaajabisha pale abiria anapokwamisha juhudi za konda kujaza watu wengi zaidi ni AJABU SANA konda jukumu lake ni kuhakisha watu wengi Zaidi wamepanda kwenye gari yapaswa kumpongeza konda ambaye anajaza watu wengi ( anafanya kazi vizuri sana )

Zifwatazo ni sababu ambazo hupelekea konda kukuruka, hizi sababu zipo katika makundi makuu mawili kundi la kwanza ni kutokana na muundo wa basi, na kundi la pili ni kutokana na ubinadamu

Kundi kutokana na muundo

Gari ambalo seat za kushoto na kulia hazipo katika mstari mmoja, yaani seat za kushoto zimepishana na seat za kulia hivyo wakati konda anakusanya nauli akitoka upande wa kushoto kuja kulia kunapelekea kuruka double seat ambazo zipo upande wa kulia. Kama umegundua hili inabidi mmvute konda na umpatie nauli yake anayoshahili ingawa jirani yako anaweza kukuangalia vibaya kama alikuwa na lengo la kusepa na nauli hiyo.

Gari ambalo ni finyu katikati, endapo gari kutokana na seat zilivyokaa inapelekea kuwa na nafasi finyu hivyo wakati konda anakusanya nauli kwa watu waliosimama huwa anaitaji abiria arudi nyuma wakati anaenda mbele ili aweze kupishana vizuri, hizi movement hupelekea konda kuconcetrate na kupishana hivyo kusahanu jukumu lake kuu la kukusanya nauli, hivyo utakaporudi nyuma mpige vibao vidogo kwenye bega na kumpatia nauli yake anayostahili.
Kundi la pili kutokana na ubinadamu

Hapa sababu zitaingia nyingi kwa upande wa konda na abiria kama konda anamawazo au anaumwa kama binadamu tunavyoumwa hii hupeleke ufanisi wake katika kazi kushuka hivyo kusahau kukusanya nauli kwa abiria wapya waliongunga ndani ya safari, kurudisha chenji kubwa, yahitaji kushirikiana na konda katika kuhakisha tunafanya kazi yake kuwa rahisi.

Imenibidi niyaseme haya maana KONDA ni fani ambayo kwa sasa ipo kufutika katika jiji la dar es salaam kutokana na magari ya MWENDOKASI hivyo tuonyeshe umoja kabla makonda wote hawajaisha na tuanze kuwamisi asante kwa kunisikiliza.
 
Mkuu mimi nikiwa katika hali ya kawaida huwa namuita nampa nauli ila kama nishavurugwa na mambo ya dunia ndo kwanza najidai nachezea simu au kusinzia kiuongo
 
MKUU MIMI NIKIWA KATIKA HALI YA KAWAIDA HUWA NAMUITA NAMPA NAULI ILA KAMA NISHAVURUGWA NA MAMBO YA DUNIA NDO KWANZA NAJIDAI NACHEZEA SIMU AU KUSINZIA KIUONGO
Kujitia usingizi wa uongo huku nauli yenyewe mia 4 ikizidi mia 6. Lol
 
Na sisi wenye private cars tocomment humuhumu au tutafunguliwa thread yetu
 
Back
Top Bottom