Sababu za Wanafunzi wengi kufeli somo la Hisabati

iQ255

Member
May 28, 2017
7
9
Wanafunzi wengi wa Primarily na Secondary wamekuwa hawafanyi vizuri katika somo la Hisabati kutokana na sababu zifuatazo.

1. Wanafunzi wengi hawajui misingi ya Hisabati kama Kujumlisha, Kutoa, Kuzidisha na Kugawanya. Maswali mengi ya hesabu huwa yanaishia na matendo haya manne.

2. Wanafunzi wengi hawaweki kichwani mathematical tables kichwani jambo linalowafanya Washindwe kuzidisha Namba za kawaida.

3. Vitabu Vingi vya Hisabati vinavyotumika mashuleni haviko sahihi, vina makosa mengi sana.

4. Kutokuwepo kwa waalimu wanaoweza kufundisha na kuwaelewesha wanafunzi hisabati kwa ufasaha.

5. Mitihani ya hisabati kuwa na majibu ya kuchagua (Multiple Choice) kitu ambacho kinawafanya wanafunzi kufaulu Hisababi kwa kukisia majibu bila kufanya maswali husika.

6. Kuwa Vitabu Vingi vyenye maswali, njia na Majibu (Review books with Questions, Solutions and Answers)

Kwa wale wataam wa Hesabu Endeleeni kutoa sababu zingine..
 
Nikiwa olevo nilifeli hesabu kwasababu ya motisha ndogo pia mwalim kuondoka! Naweza pia kusema japo alikua anajua hesabu ila hakua the best!

Nilipoenda alevo nilifaulu hesabu kwasababu ya kuwa na mwalim mzuri na anayejua hesabu! Pia alitupa motisha na kutufanya tuoende hesabu!!

Nilipofika chuo kila semester tulikua na wastan wa kozi moja ya hesabu! Semester zilikua nane...na katika kozi zote za hesabu moja nilipata C na nyingine nilipata A na B+!

Inshort, wanafunzi hawanafaulu hesabu kwanza kwa kuichukia hesabu...pili kutokua na motisha na kukata tamaa pia kuto kuwa na mwalimu mzuri wa hesabu!! Period!
 
its more physchological, kama vitabu vimekosewa, hao wanaopata 100 wasingekuepo na kushinda tuzo za additional maths and such ... watu wanakaririshwa na kuaminishwa hesabu ni ngumu hivyo kutoitilia mkazo na kutojali akifeli.
Comrade,

Hili la Vitabu kukosewa ni mtambuka..

It is also true, sababu moja Wapo ni kuwaamisha Wanafunzi kuwa hisabati ni Kigumu..
 
Back
Top Bottom