Sababu za vegetarians kutokula nyama

Sababu za vegetarians kutokula nyama

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,022
Reaction score
828,793
Hapa nazungumzia wale ambao hawali nyama kiimani na si wale ambao hawali kwasababu za kiafya tofauti na ukristo na uislam, dini kama buddhism, krishna nk wanaamini sana katika karma ya kila kiumbe na uwepo wake katika uso wa dunia, kwamba bata, mbuzi, samaki, punda na chochote chenye uhai kuna sababu maalum ya kuwa hivyo kilivyo.

Kwahiyo huwezi kutoa uhai wake kwa ajili ya shibe yako, utakuwa unajitengenezea karma mbaya, yani leo ukimuua mnyama ukala nyama yake next reincarnation yeye atazaliwa binadamu na wewe mnyama halafu atatenda kama wewe ulivyotenda imani hii imezama mno mioyoni mwao kiasi kwamba ni ngumu mno kuwakuta wanakula nyama. Kuna mazingira ambayo yanaweza kuwafanya wale nyama nayo ni.

1.Hawakushuhudia mnyama akichinjwa/akiuliwa

2. Hakuchinjwa kwa ajili yao.

3. Isiwe ni nyama kwa ajili ya biashara, hapo anaweza kula na karma isimdhuru kila imani ina uchizi wake, kuna mavegetarian ambao kwa compassion kwa viumbe hufagia kabla ya kukanyaga ili wasiwadhuru viumbe.

1625735948874.png

Mimi pia ni mmoja katika ya watu ambao hawali nyama. Mwanzoni nilifanya kutokana na Imani Yangu, lakini kwa sasa naona umuhimu na faida yake hata kwa nje ya Imani.

Sio tu Buddhism, Hinduism, Rastafaris, Ethiopian Monks, Nazarenes(Jews), na ancient Egyptians hata ukristu kuna makundi yasiyokula nyama hasa ukristu wa kale ulielewa umuhimu wa vegetarianism.

Kihistoria, imani za kale zilianza kuuliza kwanini sisi wanadamu tupo hapa duniani? Nini kinachotutofautisha na wanyama na mimea? Hivyo watu waliokuwa ENLIGHTENED kama Krishna, Buddha, Waisraeli wa kale, waliona umuhimu wa kuishi kwa Amani. Sio kuishi tu kwa amani na mwanadamu mwenzako bali kwa viumbe vyote. Haina haja ya kumpiga mnyama bila sababu na baadaye wakaona hata kumpiga mnyama haitoshi, ili kuwa na amani na kuweza kuboost Third Eye, Karma, na kubalance Chakras zako, Ishi kwa kutoua mnyama kabisa. Kila kiumbe kina haki ya kuishi.

Mimea ndio source ya kwanza ya chakula then Nyama ni Secondary source. Haina haja ya kumchinja mnyama na kumla wakati kuna vyakula vingi haviitaji kuua kiumbe. Tunapaswa kuishi kwa kuheshimu all aspects of life duniani. Kuna sababu nao wakaishi hivyo yanini niwaue, nao husikia maumivu, wanyama wanahisia ambazo hata sisi tunazo mfano upendo, huhisi maumivu, n.k lakini pia nao wanahaki kuhishi. Sisi wanadamu tuna akili ya kuwatunza na kuwajali kwani wote tumeumbwa pamoja.

Tatizo ni ego ya mwanadamu kuwa sisi ndio kila kitu na kila uhai wa kiumbe tunaweza kuutoa. Kuwa vegetarian kunakupa sio tu afya ya mwili hasa katika miaka ya vyakula vya madawa bali hata inatupa afya kiroho na kiakili. Ni vigumu kumuelezea mtu. Lakini ni kitu ambacho hakiitaji Kiongozi wa dini, wala kitabu cha dini, ni kitu kitokacho kwa hisia, hisia ya upendo tuliyozaliwa nayo sisi wanadamu kutoka aliyetuumba.
 
Apollo nimeukubali mno uchambuzi wako umegusa maeneo mengi ambayo sikuyagusia suala na ENLIGHTMENT na EGOISM, ni mambo muhimu mno ambayo wengi hatuyajui lakini vile vile kuna CRAVING ambayo haiachani sana na EGOISM, vyote vinahusika na tamaa na uchoyo uliopitiliza
 
Thanks mkuu. Nafurahi kuona hayo masomo unayafahamu. Ni masomo ambayo yanaridhisha kimaelezo hasa ukiyaexperience zaidi ya kuyasoma na kuyasikia ndio maana wengi hawajui.
 
Mi nimesoma kidogo imani za kibuda na hata zile five prisets(sheria)/misingi yao,nilichokiamini na kikuibwa mno ni kwamba mtu asiekula kitu chenye roho mara nyingi huwa na huruma sana, na hata hawa jamaa wana msingi mzuri sana ktk dini yao, huu uislam na ukristu mbwembwe nyingi mno
 
Thanks mkuu. Nafurahi kuona hayo masomo unayafahamu. Ni masomo ambayo yanaridhisha kimaelezo hasa ukiyaexperience zaidi ya kuyasoma na kuyasikia ndio maana wengi hawajui.

Nimepractice veg kwa miaka sita ni nzuri sana hata kiafya, niliporudi nyumbani nikashindwa kwakuwa wigo wetu na variety za vyakula ni mdogo mno. ilinipa shida sana mwanzoni nilikuwa nikila nyama mwili unasisimka
 
mi nimesoma kidogo imani za kibuda na hata zile five prisets(sheria)/misingi yao,nilichokiamini na kikuibwa mno ni kwamba mtu asiekula kitu chenye roho mara nyingi huwa na huruma sana, na hata hawa jamaa wana msingi mzuri sana ktk dini yao, huu uislam na ukristu mbwembwe nyingi mno

Exactly mkuu. Hata hasira na egoism zinaisha unapokula chakula kisicho na umwagaji damu.
 
mi nimesoma kidogo imani za kibuda na hata zile five prisets(sheria)/misingi yao,nilichokiamini na kikuibwa mno ni kwamba mtu asiekula kitu chenye roho mara nyingi huwa na huruma sana, na hata hawa jamaa wana msingi mzuri sana ktk dini yao, huu uislam na ukristu mbwembwe nyingi mno

Hapo kwenye priseps ni PRECEPTS ambazo ni 1.usiuwe 2.usizini 3. usiseme uongo 4.usiibe 5.usitumie vilevi. sasa kwenye ukristo amri ya kuuwa haijachambuliwa, na hizi pricepts tano ni kwa mujibu wa imani ya kibuddha
 
nimepractice veg kwa miaka sita ni nzuri sana hata kiafya, niliporudi nyumbani nikashindwa kwakuwa wigo wetu na variety za vyakula ni mdogo mno. ilinipa shida sana mwanzoni nilikuwa nikila nyama mwili unasisimka

Hahaha. I can feel that ndugu Yangu. Hata mimi baada ya mwaka mmoja wa kuacha kula nyama, nikaanza kuona nyama ni kitu mwili wangu usichokitaka tena. Nimepata faida nyingi, hasa katika kutafuta enlightment, meditation na amani ya moyo. Upendo umeongezeka sio tu kwa wanyama bali kwa kila kiumbe na wanadamu.

Japokuwa kuna challenges but as long as I'm doing this kwa ajili ya safari Yangu ya maisha hapa duniani sina wasiwasi tena.
 
Ni vizuri sana unapata piece of mind na unakuwa si mtu wa kukurupuka kwenye lolote na hata magonjwa yanakaa mbali nawe
 
Back
Top Bottom