Sababu za tatizo la kutokwa na damu puani (Mhina), jinsi ya kuzuia na tiba yake

nilikuwa na tatizo hili wakati nikiwa praimare skuli, japo niliishi kwenye baridi mostly. namshukuru Mungu lilitoweka kwani sidhani kama nilipata matibabu yoyote.
 
heshima kwenu wakuu. Nina mdogo wangu huwa anatatizo la kutokwa na damu puani limekuwa ni tatizo linalo jirudia mara kwa mara. Pia alishaenda hospitalini na huwa anapewa dawa lakini hili tatizo hutulia na kujirudia.. Naombeni mawazo yenu wakuu na ni kipi kifanyike kuzuia..
Note; anaunene wa wasitani...pia ni mwanamke..
 
Ndugu yangu I talk from my experience, nimesumbuliwa na hili tatzo utotoni mwangu mpaka kiasi cha kuhisi ningepoteza maisha at that age. Cha kushangaza nadhani nilipoanza sekondary umri huo ndhani sikumbuki tatizo hili liliondoka lenyewe mpaka sasa.

Lkn sio siri nilikuwa natokwa na damu karibia daily na kuna muda nilikuwa natokwa damu kwa masaa hata matano au sita mfululizo.
Mpe pole dogo.
 
tafuta dawa inaitwa SYLATE,generic name yake ni Etamsylate,hii ndo kiboko,kama upo Dar nenda kwenye pharmacy kubwa muone mtaalamu..please ulizia hyo ni very effective.!
 
Mkuu Frekim Jaribu Dawa zangu tumia kwa muda wa siku 3 kisha uje hapa unipe Feedback.

Kila Tiba kati ya zifuatazo ni zenye kujitegemea. Chagua iliyo rahisi kwako, Isipokufaa ndipo uchague nyengine

TIBA


(1) Changanya tone mbili mbili za mafuta ya habat soda na siki yoyote ile iwe ya Siki ya Zabibu au Siki ya Apple (Tufaha) kwenye maji ya mawaridi.Kisha utie ndani ya pua tone moja kila siku Asubuhi.


(2) Pia mgonjwa unaweza ukawa ananusa siki ya Zabibu au siki ya Tufaha tu na kijiko kimoja cha mafuta ya Habat Soda.

(3) chukuwa Maziwa Fresh ya Ng'ombe uyachemche hadi yamechemka vizuri na uyatie katika glasi, kisha chukuwa yai bichi la kuku wa kienyeji ulipasue na kulimimina ndani ya hayo Maziwa. Koroga mchanganyiko huo wa maziwa na mayai na kuacha hadi yapoe. Kunywa yakishapoa, fanya hivyo na kutumia kwa muda wa siku Mara 3 Asubuhi mchana na usiku kwa muda wa siku 3. Mkuu.@steveach hujambo lakini?

Chanzo:MziziMkavu
 
1. tafuta limau au ndimu chukua majani yake yaponde na uchanganye na maji ya ndimu au limau umuwekee kwenye pua asilale awe ameaka kwa muda. 2. kuna mnyama mmoja anaitwa Nungunungu tafuta miiaba yake awea anafukiza ule moshi awea ana vukiza kila mara.

kuna miti siijui kwa kiswahli ila naijua kwa kilugha tu sasa siwezi kukushauri hapa kama vipi wewe ni pm nitakuelekeza ni dawa komesha mimi nilikuwa natatizo hili nilikaa nalo muda mrefu sana lakini kwa leo ni takribani miaka 20 sijawahi ttoka damu tangia niitumie ila naifahamu tu kwa kilugha (kisukuma) kama na mimi siko tz kwa sasa labda useme uko wapi naweza wasiliona na jama zangu wanaweza kukutumia nje ya hapo tuonane mwezi ujao nitakuwa nimerudi Tanzania.
 
kuna mdogo wangu mwenye umri wa miaka 10 anatokwa na damu puani kila asubuhi kwa wiki anaweza kutokwa mara 3.ni ugonjwa gani jamani na tiba yake ipi?
 
mkuu kwanza pole sana pia jaribu kumpeleka hospitalini alafu mwambie mode aamishe thread yako kwenye jukwaa la madaktari nadhani utapata ushauri na tiba.
 
mkuu kwanza pole sana pia
jaribu kumpeleka hospitalini alafu mwambie mode aamishe thread yako
kwenye jukwaa la madaktari nadhani utapata ushauri na tiba.

Ahsante sana kwa ushauri.
 
Mpeleke hospital apate vipimo! Kitaalam hilo tatizo linaitwa EPISTAXIS ( bleeding from the nose), . Hili tatizo hasa linatokea pale ambapo vijimishipa vidogo vidogo , vilivyondani ya pua vinapasuka na kujilia mtu kuanza kutoa damu puani. Na mara nyingi watoto huwa linawapata hasa pale wanapokuwa na homa kali,, au kama kuna mgonjwa mengineyo ya damu , ambayo utaambiwa baada ya kumfanyia vipimo . Ahsante
 
Mpe pole. nngekuwa mnafuatilia mabandiko ya MziziMkavu mwaka 2011 alimshauri mmoja wetu hivi ...chemsha maziwa fresh yachemke vizuri chukua yai vema liwe la kienyeji gongea kwenye chombo kisha changanya kwenye yale maziwa weka yapoe kisha kunywa. mi nilipata tatizo la kutoa damu puani nikatumia hivyo ikaacha hadi leo. isipokuwa ilibidi niende pia hosp. now iam fine.
 
Last edited by a moderator:
Namuaonea huruma.Sasa ana maliza mwezi na karibu kila siku damu zikianza kumtoka puani zinaendelea hadi kwa nusu saa au zaidi. Hii inamtokea hata wakati amelala usiku na anajikuta mto umelowa damu. Hata mchana inamtokea.

Imefikia hatua sasa anajua hata dalili za damu kutoka, hivyo anakimbilia kwenye ubaridi na kupumzika. Kuna wakati hii inamsaidia, ila maranyingi zitatoka tu. Kuna wakati anajisikia kichwa kuuma, ingawa wakati mwingine zinatoka bila kichwa kuuma. Hospitali kaenda, wanapima pressure wakati mwingine ipo normal na damu inatoka, ila kuna wakati wanakuta ipo juu na akipumzika kidogo inarudi normal. Ni mwanamke kwenye mid 40s.

Hili ni tatizo gani? Wapi kuna tiba ya hii kitu? Namuonea huruma maana inamnyima raha, ebu mwenye information ya kumsaidia aziweke hapa ili tumsaidie.
 
Back
Top Bottom