Sababu za tatizo la kutokwa na damu puani (Mhina), jinsi ya kuzuia na tiba yake

Nakushauri umpeleke mtoto hospitali akapimwe damu. Anaweza akawa na tatizo la chembechembe zinazogandisha damu kuwa kidogo (Low Blood Platelets).

Hizi husababisha damu kutokuganda na hivyo kuweza kutoka kutokea puani, au mdomoni au hata akijikata damu inatoka mfululizo bila kuacha. Mara nyingi hii huwa ni hatari sana kwani husababisha kuwa na upungufu wa damu. Tatizo hili analo mwanangu wa kiume tangu akiwa na umri wa miaka minne. Alikuwa anatoka damu nyingi sana puani mpaka inaogopesha.

Kwa sasa ana miaka ishirini. Hata circumcision tulimfanyie akiwa mkubwa baada ya kushauriana na madaktari kwa kuogopa asije akatokwa na damu nyingi na ikawa hatari. Anaishi kwa kufuata ushauri wa daktari na hali yake ni nzuri. Kwa sasa tumeweza ku-control kwa kiasi kikubwa na hatoki tena damu puani mara kwa mara kama ilivyokuwa awali. Anaweza hata kumaliza mwaka mzima hajaona kitu.

Nakushauri pia usisahau MAOMBI kwani yanasaidia sana. Wote waliokupa ushauri hapo juu ni mzuri, ila nenda kwanza hospitali ili ujue tatizo ni nini.
 
Mimi damu ilikuwa inatoka puani kama maji nilitumia dawa zote za hospitali na kienyeji lakini sikupona .ila nakumbuka nilipelekwa hospitali ya al hilal enzi hizo pale nyuma ya starlight hotel nilichomwa sindano tano at interval na nikaambiwa nisitumie asprin wala aspro. kipindi hicho nilikuwa standard six mpaka leo hii na nilipomaliza chuo 2005 sijawahi kupata tatizo hilo tena
 
Tafuta miba ya mnyama anaitwaye nungunungu kisha uuchome na kunusa puani hutakaa uone tena.

Nimetumia hii dawa nikiwa mdogo lakini damu ziliendelea. Nilipona nikiwa secondari-O-level kwa msaada wa tu wa Mungu, lakini anaweza kujaribu
 
Habari wanaJF,narudi tena jamvini nikitaka msaada toka kwenu wa kidaktari zaidi. Kwa kifupi boy wangu anatatizo la kutoka damu puani,humtokea mara chache sana. Mwenyewe huwa anadai inatokea hvyo akiwa na hasira sn k2 ambacho kinanitia wac2 sana kwani nahc kuna uwezekano wa kuwepo tatizo kubwa zaidi km kansa halafu yeye hajui. Hivyo wadau naombeni msaada ktk hilo.
 
inawezekana ni tatizo au sio maana hata mimi huwa zinatoka ila ni kipindi cha kiangazi. Wajuzi tunaomba mzsaada wenu
 
Chukuwa Maziwa uyachemshe hadi yachemke vizuri na uyatie katika gilasi, kisha chukuwa yai bichi ulipasue na kulimimina ndani ya hayo Maziwa. Koroga mchanganyiko huo wa maziwa na mayai na kuacha hadi yapoe. Kunywa yakisha poa.
 
Jaribu kutumia hii dawa huenda ikakusaidia inshallah akipenda Mwenyeezi Mungu utapona. Chukuwa Maziwa uyachemshe hadi yachemke vizuri na uyatie katika gilasi, kisha chukuwa yai bichi ulipasue na kulimimina ndani ya hayo Maziwa. Kisha UKoroge huo mchanganyiko wa maziwa na mayai na kuacha hadi yapoe yakisha poa uyanywe.
 
Mkuu Qixima mQiqa, maswali yako too general in such a way unaweza kuorodhesha hapa sababu za actually, more than general.. Ingekuwa vizuri ukaeleza:

-jinsia na umri wa mwenye tatizo

-kwanza hiyo damu inaaatokaje?

-how frequent,? ikoje(fresh au ile iliyoganda)?

-kama damu inatoka sehemu nyingine yeyote ya mwili.

-kama kuna mtu katika familia/ukoo mwenye au aliyekuwa na tatizo kama hilo.

-anatumia dawa zozote kwa muda mrefu sasa/au amekuwa/alikuwa anatumia dawa kwa muda mrefu?

-Je, anashida(mgonjwa) nyingine yeyote tofauti na kutoka damu mfano(kulegea kwa nguo mwilini, kutoka damu nyingi akijikata, vifundo vya miguu na mikono kuvimba?
 
wana jamii forums amani kwenu.napenda mnifahamishe pia kwa faida ya wengine. kitu gani kinachomsababisha mtu atoke damu za puani anapotembea au anapolala.na mtu mwenye hali hiyo atasaidiwaje.
 
Mkuu mgange asante kwa kuleta huo uzi hapa, mimi pia nina tatzo la kutoa damu puani,ni tatizo la muda mrefu toka nikiwa mdogo mpaka ninachukulia km ugonjwa wa kurithi. Mara nyingi ni pua 1 tu huwa inatoa damu.

Mkuu Mzizimkavu karibu kwa maneno yenye busara.
 
Hata mimi mtoto wangu ana tatizo hilo kuna wakati mtoto wangu anatoka damu puani huwa zikimtoka namlaza chali zinakata halafu namsafisha ila tiba sahihi sijapata na sijui inasababishwa na nini Mh. Mzizimkavu tusaidie
 
Tatizo hili kisayans hujulikana kama "epitaxis" husababishwa na vitu vingi ikiwemo kurithi kwa mfano mtoto anaweza kurith "haemorage talengtasia" kutoka kwa wazazi

Hii ni hali ambayo inafanya mwili kushindwa kugandisha damu kwa wakati au haraka, vile vile damu zinaweza kutoka puani kama mtu amepungukiwa "calcium "au "vitamin k" au kunywa pombe au wakati mtu anapiga chafya kwan saa nyingine husababisha kuchanika kwa mishipa midogo midogo kwenye pua!

Au matumizi ya antgloagulant! Kama "warfaring" kwa wale wenye tatizo la "diseminating intravascular coagulation" pia joto na pressure! first aid husaidia kwakuweka pamba puani wakati mgonjwa ameegemea kwenye kiti usinyanyue kichwa kuangalia juu, au mgonjwa anaweza ku mumunya ice, zaid ya hapo huwa tunafanya surgery na matibabu mengine kama ku activet coagulation
 
Dawa ya kutibu Maradhi ya kutoka Damu Puani. Chukuwa maziwa uyachemshe hadi yamechemke vizuri na uyatie katika gilasi, kisha chukuwa yai bichi ulipasue na kulimimina ndani ya hayo maziwa. Koroga mchanganyiko huo wa maziwa na mayai na kuacha hadi yapoe. Kunywa yakishapoa. Tumia hivyo Asubuhi kabla ya kula kitu na usiku kila siku mpaka apone hayo maradhi inshallah atapona kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu .

Au tumia dawa hii pata siki kwa kiingereza inaitwa (Vinegar) kijiko kidogo changanya na maji ya wa mawaridi kwa kiingereza inaitwa (rose water) kijijko kidogo, mtilie matone matone kwenye tundu za pua yake hukatisha kutoka hiyo Damu.

Au tumia dawa hii jaribu kumnusisha huyo mgonjwa hiyo siki kwa kiingereza inaitwa (Vinegar) hiyo damu itakatika.

Au tumia dawa hii chukuwa mavi ya njiwa uyaponde, kisha uchanganye na siki kwa kiingereza inaitwa (Vinegar) ya zamani ,kisha mgonjwa awe ananusa kila mara damu ya kutoka puani itakatika inshallah jaribu Mwenyeezi Mungu atajaalia mwanao atapona inshallah.
 
Back
Top Bottom