Sababu za tatizo la kutokwa na damu puani (Mhina), jinsi ya kuzuia na tiba yake

Iza

JF-Expert Member
Jan 8, 2009
2,001
588
1591518994863.png

MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU TATIZO HILI
Nishaurini tafadhali,

Huwa nawashwa na pua sana (muda mrefu sasa) hasa wakati wa usiku nimezisugua mpaka zinatoka damu, nilidhani ni vumbi lakini nasafisha ninapolala sana, lakini tatizo ni kwamba siku moja nilishangaa kuona damu zinamwagika sana kutoka puani baada ya kama sekunde 20 zilikata hii ilikuwa 2006 sikujali sana, afu juzi kati hapa zikatoka kwa style ileile. Nimecheki Hosp wakasema ni malaria kucheki haipo.

Ni kwasababu ya kuzisugua au?

Habari wajuvi?

Mama fulani ni mjamzito wa miezi tisa kasaro siku chache sana.

Amepatwa na hili tatizo la kutokwa na damu puani.

Wataalam, kwa wajawazito hilo tatizo huwa linatokea au humaanisha nini?
---
Waasalam
Nimekua nkisumbuliwa na hilo tatizo kwa muda mrefu sasa way back nipo mdogo nilikua naambiwa ni kukaa juani ndio kisababishi lakini kadri nlivokua nakua nikagundua sio lazima nikae juani damu zitatoka tuu niliwahi kuambiwa labda nna damu nyingi nikajaribu kutoa ila nikaambiwa damu inanitosha mwenyewe tuu hivyo siruhusiwi kutoa damu.

Sio kwamba damu hutoka puani kilasiku nop kunamda naeza kaa hata miezi4 5 bila hilo tatizo na likianza naeza fululiza wiki nzima afya yangu ni nzuri tuu kilo 85 urefu 6ft sina historia ya magonjwa chronic isipokua nilipokua mdogo nilikua na aleji na vumbi kwamba nikikutana nalo tuu kifua kinabana ila asaiv nmekua na tatizo la kifua sina kabisa

JE HILI TATIZO LA DAMU KUTOKA PUANI LINASABABISHWA NA NINI?

Nimechoka kujichafua na kuchafua mashuka naombeni msaada chanzo na jinsi ya kulizibiti.'kwa mwenye uelewa tunaweza ku share hapa!

NB: mimi ni muoga wa dawa na kwa muda mrefu nmekua nikijitibu kwa maji,mpangilio wa chakula na mazoezi so kama kunaeza patikana tiba tofauti na dawa za hospitali nitashukuru ingawa haina maana siezi kutumia kabisa
---
Wasalaam ndugu zangu,

Eti hili ni tatizo gani la kutokwa na damu puani usiku ukiwa umelala (usingizini) na unaamka kichwa kinakuwa na maumivu makali sana. Kibaya zaidi unashindwa hata kuona vizuri pamoja na kuwa na kizunguzungu?
---
Jamani wataalam naomba msaada wenu wa kitabibu pamoja na kwamba ninakuwa na furaha ndani ya humu lakini leo naomba msaada wa kitabibu hata kwa ushauri na mawazo au njia hipi ni ifate inisaidie kutatua tatizo la wingi wa damu

Hali inayopelekea kuwa joto kali muda wote pamoja na kutokwa na damu mara kwa mara puani muda huu naandika lkn damu inatoka tu puani

Nisaidieni jaman na pia kujua huu ugonjwa unasababishwa na nini
---
Naomba msaada mwenye kujua hili no tatizo gani na tiba yake in nini?Nina matatizo ya kuuma kichwa upande mmoja Lina kama mwaka hivi,kinauma then kinaacha,sasa katika.

Siku hizi za karibuni nikiwa na mafua kamasi za tundu moja la pua ambalo lipo upande ambao kichwa kinauma zinakuwa zimechanganyika na damu pia nikiinamisha kichwa kinauma sana.naomba msaada wenu mwenye kujua.

UFAFANUZI WA JUMLA WA TATIZO HILI
TATIZO LA KUTOKWA NA DAMU PUANI NA TIBA YAKE (NOSEBLEED)

👉👉Ni kuvuja kwa mishipa midogmidogo ya damu iliopo puani(blood vessels), hili nitatizo lakawida sana kwa watu wengi na sio hali hatarishi sana japo kwe wengine hujirudia mara kwa mara kwa kiwango cha juu (chronic).

SABABU KUU ZA TATIZO
Zipo sababu nyingi ili kubwa ni hizi:- 👇👇
->kukauka kwa kiwambo/utando wa ndani ya pua (nasal membrane) hali inayopelekea kutungeneza nyufa na kuchanika kwa mishipa ya damu puani... "Membrane inaweza kukauka kwa sababu ya hali ya hewa, upepo, na baridi kali.
->Kufikicha ama kuingiza vidole puani (hasa kwa watoto)
->Dawa zinazozuia damu kuganda na kufanya mishipa ya damu kuwa myembamba kiasi cha kurahisisha kuchanika. Mf warfarin, Asprin n.K
->shinikizo la juu la damu(hypertenstion)
->Matumizi yaliyokithiri ya pombe
->uvimbe puani na matatizo ya kurithi

KUNDI LINALOKUMBWA SANA NA TAIZO HILI
1.Watoto (kwa kufikicha pua kwa vidole)
2.Wazee
3.wajawazito (kubadilika kwa homoni mwilini)
1581579273066.png

NJIA ZA KUZUIA DAMU INAYOTOKA
1.Inamisha kichwa kuelekea upande wa mbele... 👉 EPUKA kuinamisha kichwa kwa upande wa nyuma(kulala chali) kwani kutasababisha damu kurudi ndani ya koo la hewa ama chaukula na hivyo kusababisha kichefuchefu,kutapika na tatizo ktk upumuaji

2. bana pua kwa kutumia vidole hku ukipumulia mdomo ili kusaidia damu kuganda na mishipa kuziba

3. Tumia barafu, kwa kuiweka ktk kitambaa kizito na ukande juu/nje ya pua

4.Kaa kimya utulie huku ukihakikisha kichwa kinakuwa usawa wa juu ya moyo😯

5.Tatizo likiendelea zaidi fika kituo cha afya kilicho karbu kwa msaada zaidi wa matibabu

ONYO 👇👇

-> Usiweke pamba ama kitambaa puani
->usitumie dawa zinazosababisha kupunguza kuta za mishipq ya damu, dawa hizo nikama
Antimflamatory drugs(Ibuprofen),Asprin, warfarin n.K kwani hufanya damu iendelee kutoka ... Muone daktari kama ulikuwa kwenye dozi ya dawa hizo

KUZUIA TATIZO LISIJIRUDIE TENA

Fanya yafuatayo:- 👇
👇
1.Usifikiche pua ama kuweka kitu chochote puani, unapopiga chafya fungua mdomo ili hewa isipitie puani

2. Usifanye kazi ngumu zinazokulazimu kuinama kunyanyua vitu vizito

3. weka kichwa usawa wa juu wa moyo, kuzuia damu nying kusukumwa kuelekea upande wa kichwani (puani)

4. Usivute sigara

5. Kula mlo laini na vinywaji baridi(beverage), usitumie vinywaji vya moto ndan ya masaa 24 mf chai kahawa n.K

-> USITUMIE ASPRIN, IBUPROFEN, WARFARIN nadawa zingne za makundi hayo

NJIA RAHISI ZA KUTIBU

1. Pakaa ointment mfano vasseline.. Hapa waweza kutumia mafuta ya mgando/mazito ili kulainia ndani ya pua kuzuia mishipa kuchanika

2. Zuia mtoto asifikiche pua

3. KITUNGUU
Kitunguu kinasaidia sana kutibu hili tatizo,
->kata vipande vidigovidogo kisha weka chini ya tundu za pua na uvute harufu ndani ya dakika kadhaa tatizo litaisha

-> pia unaweza kukamua juice yake kisha dondoshea matone 2-3 katia tundu zote zapua tiba itatokea ndani ya muda mfupi

4. matibabu ya hospitali pia yanafaa endapo tatizo litakuwa bado halijaisha, daktari atakupatia tiba mbalimbali mf nassal spray, nk

"Hatima ya afya zetu ipo mikononi mwetu"

PIA SOMA:

Kinachosababisha damu itoke puani


KUTOKA damu puani ni hali ambayo damu inatoka kutoka ndani ya matundu ya pua.

Watu wengi wameshawahi kupata hali hii angalau mara moja kwenye maisha yao na hujitokeza zaidi kwa watoto.

Ingawa hali ya kutoka damu puani inapotokea huleta hofu, mara nyingi huwa inatokea kwa mtu kwa kipindi kifupi na huwa haihusiani na tatizo lolote kubwa la kiafya. Mtu anasemekana kuwa ana tatizo la kutoka damu puani mara kwa mara endapo tatizo hili linamtokea mara mbili au zaidi kwa wiki.

Ndani ya pua kuna ukuta mlaini ambao una mishipa ya damu midogo midogo mingi na ambayo ipo juu juu hivyo kuwa rahisi kuumizwa na kupasuka. Mambo mawili makubwa yanayosababisha kutokwa kwa damu puani ni hali ya ubaridi au upepo mkali na kukuna ndani ya pua.

Hewa ya ubaridi au upepo mkali husababisha kukauka kwa ukuta ndani ya pua na mtu kuwa katika hatari ya mishipa kupasuka au kupata maambukizi ya bakteria.

Vilevile kugusagusa ndani ya matundu ya pua, mfano kujikuna ama kwa vidole au kwa kutumia kitu chochote kile huwa kunasababisha kupasua mishipa ya damu iliyopo ndani ya pua. Watu wengi wanaotokwa na damu puani sababu mojawapo kati ya hizi huwa imehusika.

Hata hivyo, zipo pia sababu nyingine kama vile maambukizi kwenye mfumo wa pua, aleji, kuwa na kitu kilichokwama ndani ya pua, matumizi ya dawa zinazosababisha utokwaji wa damu, na baadhi ya magonjwa ambayo yanasababisha mwili kushindwa kugandisha damu mfano, hemofilia. Kwa ujumla, kutokwa damu puani siyo dalili ya ugonjwa wa shinikizo la damu.

Hata hivyo, kuwa na shinikizo la damu la juu kunaweza kumsababishia mtu mwenye tatizo la kutoka damu puani, zitoke kwa wingi au kwa muda mrefu zaidi. Mara nyingi tatizo la kutoka kwa damu puani si kubwa na damu huacha kutoka zenyewe baada ya muda mfupi.

Viashiria vya hatari kwa mtu anayetokwa na damu puani ambavyo ni lazima kuhudhuria hospitali mara moja ni kama damu zimeanza kutoka puani baada ya kupata ajali; damu inayotoka mfululizo nyingi, endapo utokaji wa damu puani unasababisha kushindwa kuhema vizuri, damu zimeendelea kutoka kwa zaidi ya nusu saa hata baada ya kukandamiza pua, na damu inatoka kwa mtoto chini ya miaka miwili.

Mtu mwenye hali kama hizi lazima ahudhurie hospitali mara moja kwa kusindikizwa na mtu mwingine na sio kwenda akiwa peke yake.

Vilevile, ni vizuri kumwona mtaalamu wa afya kama damu itakuwa inatoka mara kwa mara (zaidi ya mara mbili kwa wiki) hata kama huwa inaacha kutoka baada ya muda mfupi.

Huduma ya kwanza mara damu zinapoanza kutoka puani ni kukaa na kuinamia mbele kidogo. Kutumia kitambaa au karatasi maalumu za kujifutia kukinga damu. Kulala kifudifudi au kuinama chini hakutakiwi.

Kukaa na kuinamia mbele kidogo, kunapunguza presha ya kwenye mishipa ya damu ya ndani ya pua na hivyo kupunguza damu kutoka.

Kuinamia mbele kunazuia damu kuingia njia ya chakula na kwenda tumboni ambapo inaweza kuleta madhara mengine.

Baada ya kukaa na kuinamia mbele kidogo, ni vizuri kupuliza pua kidogo kidogo mithili ya kutoa mafua ili kutoa mabonge ya damu yaliyo ndani ya pua.

Halafu pua zote mbili zibanwe kwa kutumia kidole gumba na kidole cha kwanza wakati mtu anahema kwa kutumia mdomo.

Pua ibanwe kwa dakika tano, halafu iachiwe ili kuangalia kama damu imeacha kutoka. Kubana pua kunaweza kurudiwa kwa dakika tano nyingine kama damu inaendelea kutoka.

Endapo damu itaendelea kutoka kwa muda mrefu, madaktari watatumia dawa na vifaa maalumu vya kuweka kwenye pua ili kubana mishipa inayotoa damu.

Damu itakapoacha kutoka, pua zisipulizwe (kupenka), jitahidi kutoinama na kutoingiza vidole ndani ya pua kwa saa kadhaa.

Kama tatizo linajirudia mara kwa mara zipo njia za tiba ambazo wataalamu wa afya watajadiliana na mgonjwa kuzitumia ili kumaliza tatizo.

Pia watafanya uchunguzi kubaini kama kuna tatizo la kiafya linalosababisha damu itoke.

Vitu vinavyopunguza uwezekano wa kutokwa na damu puani ni kuhakikisha ukuta wa ndani ya pua haukauki. Hii inawezekana kwa kupaka mafuta mazito mfano Vaseline ndani ya pua hasa wakati wa baridi.

Kwa kuwa watoto hupenda kuingiza vidole ndani ya pua, kucha zao mara zote ziwe fupi.

Vilevile vipo vifaa maalumu vinavyoweza kutumika kulainisha ndani ya pua. Mambo yote haya ni rahisi na yanaweza kusaidia kupunguza kutoka damu puani.

AU SOMA:
Tatizo la kutokwa na damu puani husababishwa na kupasuka kwa mishipa midogomidogo inayosambaza damu puani. Tatizo hili hutokea kwenye tundu moja ama yote ya pua na linaweza kusababisha hata kifo kama halitapatiwa ufumbuzi kwa muda muafaka.

Nini sababu za kutokwa na damu puani?
Kuna sababu nyingi sana zinazoweza kusababisha mtu kutokwa na damu puani na miongoni mwa hizo sababu ni;
 • Kupasuka kwa mirija ya damu inayopeleka damu kwenye maeneo ya pua.
 • Shinikizo la damu kuongezeka (High blood pressure)
 • Kupiga chafya (sneezing)
 • Kupenga kwa nguvu.
Jinsi ya kutoa huduma kwa mtu anayetokwa damu puani
 • Mruhusu mginjwa akae. (Usimlaze chali maana damu inaweza kurudi na kuziba mirija ya hewa na mgonjwa akashindwa kupumua)
 • Hakikisha milango ya hewa (Mdomo) iko wazi ili mgonjwa aendelee kupata hewa safi ya Oksijeni.
 • Mkalishe akiwa ameinama kidogo kuelekea mbele.
 • Binya kidogo matundu ya pua yake kwa muda kidogo. (Mgonjwa mwenyewe anaweza kufanya hivi pia kama hajazidiwa sana)
 • Mwambie avute hewa kupitia mdomo na siyo pua maana utakuwa umeiziba.
 • Baada ya muda kidogo achia halafu uangalie kama damu imeacha kutoka.
 • Endelea kwa utaratibu huu (wa kubinya pua na kuachia baada ya muda) kama mara nyingi.
Kama damu haijaacha kutoka kwa muda wa dakika 30, basi MWAHISHE MGONJWA WAKO HOSPITALI kwa matibabu zaidi

ZINGATIA

Kama mtu anatokwa damu puani, lengo lako kubwa la kumsaidia ni kuhakikisha unaondoa au unapunguza tatizo la damu kuendelea kutoka kwa mtu huyu.
Wakati unaendelea kumsaidia mgonjwa, mwambie azingatie haya;
- Asiongee.
- Ajizuie kukohoa.
- Asiteme mate.
- Kumzuia mgonjwa kufanya niliyokueleza hapo juu ni ili kuzuia kuharibu mabongemabonge ya damu ambayo yanaweza kuwa yamejitengeneza puani na kusababisha damu ziendelee kutoka.


MAONI YALIYOTOLEWA NA WACHANGIAJI
Ndugu yangu Capitalist...kutoka damu puani (Epistaxis) si tatizo dogo la kubeza, kwani inaweza ukawa unapata attacks ndogo ndogo kisha zinastop ukadharau, kuna siku zitatoka tuu non-stop na huwa kucontrol hiyo bleeding..Nimeona cases kama hizo kadhaa!

Tafadhali nenda haraka kamuone daktari specialist ENT (Ear, Nose and Throat) akufanyie evaluation ya kutosha na kukushauri tiba na nini cha kufanya unapopata attack.
---
Dawa ya kutibu Maradhi ya kutoka Damu Puani. Chukuwa maziwa uyachemshe hadi yamechemke vizuri na uyatie katika gilasi, kisha chukuwa yai bichi ulipasue na kulimimina ndani ya hayo maziwa. Koroga mchanganyiko huo wa maziwa na mayai na kuacha hadi yapoe. Kunywa yakishapoa. Tumia hivyo Asubuhi kabla ya kula kitu na usiku kila siku mpaka apone hayo maradhi inshallah atapona kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu .

Au tumia dawa hii pata siki kwa kiingereza inaitwa (Vinegar) kijiko kidogo changanya na maji ya wa mawaridi kwa kiingereza inaitwa (rose water) kijijko kidogo, mtilie matone matone kwenye tundu za pua yake hukatisha kutoka hiyo Damu.

Au tumia dawa hii jaribu kumnusisha huyo mgonjwa hiyo siki kwa kiingereza inaitwa (Vinegar) hiyo damu itakatika.

Au tumia dawa hii chukuwa mavi ya njiwa uyaponde, kisha uchanganye na siki kwa kiingereza inaitwa (Vinegar) ya zamani ,kisha mgonjwa awe ananusa kila mara damu ya kutoka puani itakatika inshallah jaribu Mwenyeezi Mungu atajaalia mwanao atapona inshallah.

View attachment 596170
---
Tatizo hili kisayans hujulikana kama "epitaxis" husababishwa na vitu vingi ikiwemo kurithi kwa mfano mtoto anaweza kurith "haemorage talengtasia" kutoka kwa wazazi

Hii ni hali ambayo inafanya mwili kushindwa kugandisha damu kwa wakati au haraka, vile vile damu zinaweza kutoka puani kama mtu amepungukiwa "calcium "au "vitamin k" au kunywa pombe au wakati mtu anapiga chafya kwan saa nyingine husababisha kuchanika kwa mishipa midogo midogo kwenye pua!

Au matumizi ya antgloagulant! Kama "warfaring" kwa wale wenye tatizo la "diseminating intravascular coagulation" pia joto na pressure! first aid husaidia kwakuweka pamba puani wakati mgonjwa ameegemea kwenye kiti usinyanyue kichwa kuangalia juu, au mgonjwa anaweza ku mumunya ice, zaid ya hapo huwa tunafanya surgery na matibabu mengine kama ku activet coagulation
---
Nilikuwa na tatizo hilo la kutokwa na damu sanaaa nikiwa mdogo mpaka nilipofika form two/three nilichogundua kuwa ni sababu kwangu mimi ni:-

-kukaa muda mrefu au kucheza muda mrefu mahali penye joto mara nyingi kwenye jua,na nilikuwa naweza kukaa au kucheza mchana ila damu inanitoka usiku nikiwa nimelala.
-Pia unaweza kuona kuwa ni utani ila nilipokuwa naogea maji ya moto au kumimina maji ya moto kichwani damu inanitoka haswa. Pia nilikuwa na tabia ya kuchokonoa pua like everytime.

Sababu: niliambiwa na daktari kuwa kuna watu wana mishipa milaini sana maeneo ya puani ambayo inacollapse na kukatika na hata kuachia flowing ya damu,ila sii watu wote.

WARNING: Usimlaze chali mtu anayetokwa na damu puani kama wafanyavyo watu wengi na hata mimi nilikuwa nafanyiwa hivyo.Hii ni kwasababu ile damu huwa inarudi tumboni na baadaye inasababisha tumbo kuuma ILA inaweza kutokea ikarudi kwny mishipa ya ubongo na ni vibaya mno kwsbb inaweza kusababisha kifo.

SOLUTION: Muinamishe tu huyo mtoto kawaida huku ukimwekea barafu au maji ya baridi sana utosini,kwny paji la uso na hata shingoni kwa upande wa nyuma na damu itakata.Aepuke kukaa mahali penye joto sana na ikiwezekana kama chumbanii anapolala kuna joto aijifunike gubigubi.Hiyo ilinisaidia na mpk sasa sijapata tatizo hilo.
---
KUTOKWA NA DAMU PUANI AKA (MHINA)

Kutokwa na damu puani ni hali inayotokea watu wengi hasa wakati wa utoto na uzee. Damu hii hutoa kwenye kuta za ndani za pua. Kuta hizi zimejaa mishipa ya damu iliyo membamba na kufunikwa na kiasi kidogo cha seli laini. Kwa hali hii huwa ni rahisi kupasuka pale inapoguswa au kukutana na hali ya ukavu mkali. Inapopasuka damu humwagika na kutoka puani hali inayojulikana kwa kitaalamu kama epistaxis.

Mara nyingi hali hii huisha yenyewe bila kuhitaji matibabu, ingawa mara chache inaweza kuwa ya kuhatarisha maisha kiasi cha kuhitaji matibabu ya haraka.
Damu inaweza kutoka sehemu ya mbele au nyuma ya ndani ya pua. Mara nyingi damu hutokana sehemu ya mbele ya ndani ya kuta za pua (anterior nose bleeding).

Sababu

Kutokwa damu puani ni dalili inayoweza kusababishwa na magonjwa au hali mbalimbali zifuatazo :
 • Kuingiza vidole puani
 • Kupiga chafya au kupenga mafua kwa nguvu sana
 • Shinikizo la damu la kupanda
 • Saratani ya damu
 • Matatizo ya damu kushindwa kuganda
 • Kuumia puani kwa kujigonga, au kuvunjika mfupa wa pua
 • Kutumia dawa za kuzuia damu kuganda kama aspirin, clopidogrel na warfarin.
 • Saratani ya pua
 • Magonjwa ya ini au figo
 • Maambukizi ya bakteria au virusi kwenye pua
 • Matumizi ya madawa ya kuvuta puani
 • Kukauka kwa kuta za ndani za pua
Namna Inavyotokea

Kutokwa na damu puani hutokea hasa kwa watoto wa umri wa miaka 2-10 na watu wazima wenye umri wa miaka 50-80.
Hali hii hutokea ghafla damu ikianza kutoka puani polepole. Inaweza ikatoka kwenye tundu moja la pua au yote mawili. Wakati mwingine damu inaweza kutoka baada ya kutembea kwenye jua kali au kufanya mazoezi.
Damu inaweza kutoka wakati wa usiku ukiwa umelala na ukaimeza, kisha ikaonekana kwa kutapika damu au mabonge ya damu, au kupata choo chenye damu damu au cheusi sana.

Nini cha Kufanya

Mara nyingi kutokwa damu puani huacha baada ya muda mfupi bila kuhitaji matibabu. Unapotokwa damu puani fanya yafuatayo;
 • Tulia, usihangaike hangaike.
 • Inua kichwa chako kiwe juu ya usawa wa moyo
 • Inamisha kichwa chako kuelekea mbele kidogo kuzuia kumeza damu
 • Minya sehemu laini ya pua kwa vidole vyako kwa dakika 10 mpaka 15.
Unaweza ukatumia dawa za kupuliza puani ili kusimamisha damu isitoke.
Ikiwa damu inaendelea kutoka licha ya kuibana pua kwa dakika 15 au kupulizia dawa ya kuzuia damu kutoka, unatapika damu au kama hali hii inajirudia mara kwa mara basi onana na daktari haraka iwezekanavyo.
Matibabu ya hospitali hujumuisha;
 • Kuziba mshipa wa damu uliopasuka kwa umeme
 • Kuweka pamba zenye kemikali za kuzuia damu kutoka ndani ya pua. Hizi hukandamiza mishipa ya damu na kuzuia damu kuvuja. Hukaa kwa siku 1 mpaka 3 kabla ya kuondolewa.
 

Abunwasi

JF-Expert Member
Jun 25, 2009
5,488
3,452
Nosebleed is loss of blood from the tissue lining the nose. Bleeding most commonly occurs in one nostril only.

Nosebleeds are very common. Most nosebleeds occur because of minor irritations or colds. They can be frightening for some patients, but are rarely life threatening.

The nose contains many small blood vessels that bleed easily. Air moving through the nose can dry and irritate the membranes lining the inside of the nose, forming crusts. These crusts bleed when irritated by rubbing, picking, or blowing the nose.

The lining of the nose is more likely to become dry and irritated from low humidity, allergies, colds, or sinusitis. Thus, nosebleeds occur more frequently iduring cold season when viruses are common and heated indoor air dries out the nostrils. A deviated septum, foreign object in the nose, or other nasal blockage can also cause a nosebleed.

Most nosebleeds occur on the front of the nasal septum, the tissue that separates the two sides of the nose. The septum contains many fragile, easily damaged blood vessels. This type of nosebleed can be easy for a trained professional to stop.

Less commonly, nosebleeds may occur higher on the septum or deeper in the nose. Such nosebleeds may be harder to control. Occasionally, nosebleeds may indicate other disorders such as bleeding disorders or high blood pressure.

Frequent nosebleeds may also be a sign of hereditary hemorrhagic telangiectasia (also called HHT or Osler-Weber-Rendu syndrome). Blood thinners such as Coumadin or aspirin may cause or worsen nosebleeds.

Repeated nosebleeds may be a symptom of another disease such as high blood pressure, allergies, a bleeding disorder, or a tumor of the nose or sinuses.
 

Iza

JF-Expert Member
Jan 8, 2009
2,001
588
thanks for the tip! atleast nimepata ka mwanga, Mola Akuzidishie
 

Change_it

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
279
83
kuna kiumbe mmoja kama nungunungu tafuta mishale yake choma afu uvute ule kama vile unanusa, itaisha kabisa.
 

Daffi Jr

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
3,830
905
kuna kiumbe mmoja kama nungunungu tafuta mishale yake choma afu uvute ule kama vile unanusa, itaisha kabisa.
<br />
<br />
Duh!kiumbe gani huyo na anapatikana wapi!imethibitishwa au iko kiimani zaidi kama dawa ya babu wa loliondo?
 

Mwanaweja

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
3,575
521
tafuta limau na majani ya mifangio inayonuka (Malumba) kama unatoka village unanipata kuna mifangio siijui jina ila inanuka na wakati mwingine inatumika kufukuzia nyuki kwa sababu ya harufu yake ponda ponda weka puani kwa muda
 

Mau

Senior Member
Apr 8, 2009
176
10
Mwenyewe nilikuwa na tatizo kama lako na zilikuwa zikinitoka kila siku asubuhi nikiamka nikapata rafiki ambaye baba yake ni doctor akaniletea vidonge flani kutoka kwa babake toka nilipomeza wee ndo umenikumbusha tena leo manake nishasahau hilo tatizo. La msingi niPM nikuunganishe na baba yake jamaa
 

Riwa

JF-Expert Member
Oct 11, 2007
2,597
3,018
Wakuu nisaidieni nina tatizo la kutokwa na damu ni la mda mrefu dawa yake nini?

NAWASILISHA

Ndugu yangu Capitalist...kutoka damu puani (Epistaxis) si tatizo dogo la kubeza, kwani inaweza ukawa unapata attacks ndogo ndogo kisha zinastop ukadharau, kuna siku zitatoka tuu non-stop na huwa kucontrol hiyo bleeding..Nimeona cases kama hizo kadhaa!

Tafadhali nenda haraka kamuone daktari specialist ENT (Ear, Nose and Throat) akufanyie evaluation ya kutosha na kukushauri tiba na nini cha kufanya unapopata attack.
 

God bell

JF-Expert Member
May 13, 2011
591
208
Ndugu, poleni kwa majukumu. Mtoto wangu wa miaka 7 ana tatizo la kutokwa damu puani. Inatoka mda wowote, haijalishi ni kipindi cha baridi au joto, kwani anaweza akaamka asubuhi damu ikaanza kutiririka. Naombeni ushauri madoctor.
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,858
30,255
Dawa ya kutibu Maradhi ya kutoka Damu Puani. Chukuwa maziwa uyachemshe hadi yamechemke vizuri na uyatie katika gilasi, kisha chukuwa yai bichi ulipasue na kulimimina ndani ya hayo maziwa. Koroga mchanganyiko huo wa maziwa na mayai na kuacha hadi yapoe. Kunywa yakishapoa. Tumia hivyo Asubuhi kabla ya kula kitu na usiku kila siku mpaka apone hayo maradhi inshallah atapona kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu .

Au tumia dawa hii pata siki kwa kiingereza inaitwa (Vinegar) kijiko kidogo changanya na maji ya wa mawaridi kwa kiingereza inaitwa (rose water) kijijko kidogo, mtilie matone matone kwenye tundu za pua yake hukatisha kutoka hiyo Damu.

Au tumia dawa hii jaribu kumnusisha huyo mgonjwa hiyo siki kwa kiingereza inaitwa (Vinegar) hiyo damu itakatika.

Au tumia dawa hii chukuwa mavi ya njiwa uyaponde, kisha uchanganye na siki kwa kiingereza inaitwa (Vinegar) ya zamani ,kisha mgonjwa awe ananusa kila mara damu ya kutoka puani itakatika inshallah jaribu Mwenyeezi Mungu atajaalia mwanao atapona inshallah.

MHINA.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom