Hivi dalili za uchungu kwa mke zinaweza kumhusisha na Mume?

kilamba lamba

JF-Expert Member
May 27, 2020
367
679
Nawasalimu ndugu zangu. Natumai ni wazima.

Ningependa kuuliza jambo kwani najua humu hawakosekani wajuzi wa mambo. Hivi Uchungu kwa mke anayekaribia kujifungua unaweza kumhusisha na mume?

Yaani dalili ambazo anapata mume zipo kwenye kuashiria kwamba na mkewe anakaribia kujifungua?
 
Nilikua siamini mpaka yalivonikuta, wife alizaa kiboss tu ila ni kama nilipatata huo uchungu maana nilihaha hatari.
NB HAKUNA PROOF YA KISAYANSI, HII IMEKAA KIMKAKATI TU (CONSPIRACY)
 
mimi wala huwa sijui chochote kwanza huwa hawasemi kama ni uchungu atakuambia tumbo linauma au kiuno kizito nk dalili sasa na makisio ya dr ndo yatakufanya ujue kuwa huyu yupo na uchungu haraka sana hospital kwangu huwa si hisi kitu chochote.
 
Hakuna kitu kama hicho mkuu,wife alijifungua mm sikuwa nyumbani na sikuhisi chochote maana niliongea nae mchana yake hatukutarajia kama angejifungua siku ile na hata uchungu ulimpomshika kwangu mda huo ilikuwa normal tena nilikuwa kazin...maana walinipigia wakiwa njian kwenda hospitali,nilimuombea basi akajifungua salama...tuwaheshimu wanawake ule uchungu sio poa mzee!
 
Nawasalimu ndugu zangu. Natumai ni wazima.

Ningependa kuuliza jambo kwani najua humu hawakosekani wajuzi wa mambo. Hivi Uchungu kwa mke anayekaribia kujifungua unaweza kumhusisha na mume?

Yaani dalili ambazo anapata mume zipo kwenye kuashiria kwamba na mkewe anakaribia kujifungua?

Hali hii ipo huitwa Cauvade Syndrome. Mwanaume kuweza kupata dalili zimhusuzo mwanamke mjamzito kutokana na ujauzito wa mkewe.

Psychosomatic symptoms of the Couvade syndrome in Finnish and Polish expectant fathers - PubMed
 
Back
Top Bottom