Mathethamathetha
Senior Member
- Jul 11, 2015
- 152
- 148
Umeshachelewa, Lema ndio mbunge wetu hata kama hajafanya chochote.
Jamani Watz wenzangu tuwe wa kweli kwaani maeneo yasiyo na maandamano kama songea Rukwa Tabora je huko kumeendelea kuliko Arusha au ni propagada za kulitaka jimbo la Arusha?
Hiyo kauli ilitumika sana Arusha kipindi kile cha chadema asilia.
Soma hoja yangu kwa nini ataanguka nimeongelea combinations of issues na sio sababu moja tu.
Tatizo uwezo wenu wa kuchambua na kuelewa mambo ni mdogo sana.
Mkuu tatizo la umeme lilikuwepo kwa mda mrefu lakini Arusha iliendelea.Hii propaganda ya kwamba arusha imekosa mapato kutokana na utalii huwa hata nikiiangalia nacheka, na huyo mgombea wa ACT naye namuona anaitumia sana huku akijifanya eti amani ya arusha imepotea. Ukweli ni kwamba sisi tunapata hela zetu kutokana na sekta ya utalii, tunapata hela za kutosha na watalii wanakuja kwa wingi Arusha. Ukitaka kuamini angalia pato la utalii utaona Arusha imechangia kwa kiasi gani. Tuje kwenye mikutano ya hapa Arusha, huenda ni kweli mikutano ya arusha imepungua lakini ni kwa ajili ya fitina za kisiasa ili Lema aonekane hafai. Na hata hivyo sisi wakazi wa Arusha hatutaki mikutano kama hisani, mnaweza kupeleka popote nchi hii kwani ni pato la nchi nzima hata wafanyie Dar, Mwanza nk. Kama ni kweli mnalosema Lema amesababisha uchumi wa Arusha kushuka na mnadhani sisi ni wajinga ngoja nikueleze, hivi leo ni zaidi ya miezi miwili kila siku kuna mgao wa umeme, mgao huu umekuwa na matokeo na hasara ya wazi kuliko hizo propaganda mnazotuletea hapa. Mgao huu umekuwa ukijirudia mara kwa mara katika kipindi chote cha miaka mitano na wananchi wameendelea kupata hasara ya wazi bila serekali ya ccm kufidia hasara hiyo. Sasa tuwaulize huu mgao wa umeme ulioletwa na serekali ya ccm na Lema kuwa mbunge wa Arusha ni kipi kimewapa wananchi wa Arusha hasara ya wazi?
Mnaosema arusha hakuna amani ni nyie mnaokuja na hadhithi za kiccm lakini sisi wakazi wa Arusha tunajua waliokuwa wanavunja amani ni jeshi la polisi kwa kuagizwa na ccm kisa mbunge wa hapa arusha mjini hakubaliani na maslahi yao. Hivyo kama kweli mnauchungu na sisi tunaomba tuwaambie Arusha kuna amani ila kuna mgao wa umeme ulioletwa na serekali ya ccm, na kama ni watalii wapo wa kutosha kwani nchi hii ina amani na wataliii wanalifahamu hilo. Hizo taasisi za serekali zinazogoma kuleta mikutano arusha kwa sababu za kisiasa zinaweza kuendelea hivyohivyo kwani hata ukiangalia mikutano yao mingi haina tija zaidi ya kujiandikia sitting allowance nyingi na kuishia kumbebesha mwananchi mzigo. Na tunampongeza sana Lema kwani ametekeleza majukumu yake matatu vyema ya kibunge kama nitakavyoyataja hapo chini
- Kutuwakilisha bungeni
- Kutunga sheria bungeni
- Kuisimamia na kuishauri serekali.
Mkuu tatizo la umeme lilikuwepo kwa mda mrefu lakini Arusha iliendelea.
Ukosefu wa mikutano ni vurugu za kila kukicha zilizohamasishwa na lema.
Hivi ahadi nilitoa mimi au lema?iweje ukatae hata issue ya ahadi alizoshindwa kutekeleza?
Leo hii manispaa haina hospitali na hakuna juhudi yoyote ya kujenga.
leo hii Arusha haina stand ya kueleweka ya mkoa baada ya vurugu za lema kuzuia utekelezaji wa master plan ya jiji la Arusha.
Katafute watoto wadogo ndio uwaambie huu upuuzi unaousema hapa. Kujenga hospital ama miundo mbinu yoyote ni wajibu wa mmbunge? Mmbunge akijenga miundo mbinu ni kupitia uhamisishaji wake na wafadhili wake kwani kipato cha mmbunge hakimudu kutengeneza miundo mbinu kama hospital nk. Kama unataka tuamini Lema ndio alizuia stand kujengwa mbona alimgomea meya kwamba hajapatikana kihalali na bado hamkutekeleza. Unasema umeme ulikuwa haupo lakini Arusha iliendelea, are you serious au umeamua kujitutumua na propaganda za kizee? Kwa hiyo Lema aliwazuia watu kwenda kwenye kazi zao? Unaweza kunitajia siku Lema aliyowazuia watu kwenda kwenye kazi zao? Mimi naweza kukutajia vipindi vyote vya migao ya umeme na jinsi vilivyoathiri makundi yafuatayo
Hayo ni makundi ambayo leo ukiwafuata watakuambia kati ya Lema na Serekali ya ccm ni nani aliyewaletea umaskini watakuambia bila kusita na ndio maana watu wanataka mabadiliko.
- Wachomeleaji
- Vinyozi
- Wauza vyakula barafu
- Viwanda kwa kuongeza gharama ya mafuta ili kutumia generator
- Ofisi za uchapishaji
- Achia mbali watu kushindwa kuweka vitu kwenye majokofu
- Mahoteli kujikuta yanaingia gharama kubwa za uendeshaji kutokana na kukosekana kwa umeme
Naomba pia nisaidie, hayo majimbo yote yanaongoza kwa umaskini hapa nchini nayo yamesababishwa na Lema kuwa mbunge wao? Hizi propaganda zinakuacha uchi kuliko unavyodhani. Mfano nipe taarifa ya maendeleo ya 2010-2015 katika majimbo ya yafuatayo yanaongozwa na wabunge wa ccm
- Simanjiro v/s Arusha mjini
- Kilindi v/s arusha mjini
- Handeni v/s arusha mjini
- mtama v/s arusha mjini
Mkuu jingalao hebu pita na hapa
https://www.jamiiforums.com/uchaguz...zwa-kupiga-kampeni-arusha-mjini-new-post.html
Nashukuru kwa kukubali lile ninalolisema japo kwa imani yako unahisi yameisha.
Omba picha za jiji la Arusha leo ujionee
Wewe endelea kuchambua mambo ambayo hayachambuki Ccm Arusha ilishafutika kitambo sana.Hiyo kauli ilitumika sana Arusha kipindi kile cha chadema asilia.
Soma hoja yangu kwa nini ataanguka nimeongelea combinations of issues na sio sababu moja tu.
Tatizo uwezo wenu wa kuchambua na kuelewa mambo ni mdogo sana.
Kwa hiyo bendera na mabango ndio ccm mbona mnashindwa at a kutumia viwanja vyenu kufanyia kampeni kama bado mpo mjaze watu we we kaa hapo masaki it center ya huku nje wanajua wanayoyaona ccm huu ndio mwisho wenu