Sababu za Lema kuanguka Arusha hizi hapa!

Sababu za Lema kuanguka Arusha hizi hapa!

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
39,412
Reaction score
31,917
Ni wazi lema alikuwa na mvuto wa kipekee katika siasa zilizoijenga chadema kiasi cha kuonekana na Lowassa na Sumaye.

Mapokezi ya lema Arusha baada ya kushinda kesi ya uchaguzi ni mapokezi makubwa kuliko hata ya marais wa marekani waliofika Arusha.

lema alipendwa lakini zipo sababu kadhaa zinazofanya aanguke mwaka huu.


1-Ni kuhusu ahadi zake kwa wananchi.
lema aliahidi mengi lakini makubwa ni kuhusu kufufua na kurejesha kiwanda cha general tyre,Kujenga machinga complex,kujenga hospitali ya manispaa ya Arusha ambapo baadae alibadili na kusema hospitali ya mama na mtoto,kutetea wakazi wa kaloleni wasihamishwe kwenye kota za kaloleni bila fidia,kuboresha miundo mbinu ya soko la kilombero na kuirejesha timu ya AFC.hizi ni baadhi ya ahadi za lema.

kimsingi hakuna alichotekeleza na badala yake anaegemea kwenye mgongo wa kazi na mipango ya ccm Arusha kama vile ujenzi wa barabara za mjini na kupanda kwa mapato.

2-Ni kuhusu kuungwa mkono na wafanyabiashara wadogo ambao wengi sio wapiga kura wa Arusha mjini.

Pia hapa nieleze kuwa baada ya ujio wa lema wafanyabiashara wakubwa wamepoteza sana kutokana na vurugu au kunyimwa fursa.lema hana ushawishi wa kibunge wa kutengeneza fursa za kiuwekezaji au kibiashara.

3-kuzorota kwa biashara ya utalii.Ni wazi kuwa iwe kwa makusudi ya ccm ama kwa vyovyote vile ni wazi kuna upungufu wa dhahiri kwenye biashara ya utalii ambayo vijana wengi wenye elimu za sekondari na vyuo vya ufundi wamejiajiri au kuajiriwa.
Ujio wa lema umefifisha utalii iwe wa kwenda porini au wa mikutano ya kimataifa.
Watu wa Arusha hawataki kuona hilo tena.


4-Kuhusu fedha za kufanya kampeni.
Hili la kutokuwa na fedha za kufanya kampeni limemkuta hata 2010 lakini ilikuwa ni bahati wana wa Arusha waliamua kuiondoa ccm tu na hivyo kampeni ziliendeshwa na wapambe zaidi mwaka huu wapambe wamehamia kwa monaban.
Mpaka anatangazwa kuwa mbunge lema alikuwa hoi kifedha kiasi cha kutaka kuhongwa na lowassa ili aachie jimbo wananchi wakashinikiza asithubutu.

5-Wafuasi aina ya mama ntilie,bodaboda na watoto wa mitaani.
Hawa walikuwa ndio wanajaza mikutano ya lema na kumsindikiza kila anapopita.
Mpinzani wake ndugu Monaban alianza kuwawezesha hili kundi kwa mikopo na misaada ya hapa na pale kwa hiyo sasa wanamuunga mkono.

6-Uswahiba wa Monaban na Lowassa.
Hiĺi ni jambo linalomchanganya lema sana.
Monaban ni zaidi ya swahiba wa lowassa.
lowassa ataendelea kumhujumu lema kama ilivyokuwa 2010 wakati lowassa akimsapoti batilda.isitoshe Monaban alikuwa ndio Team lowassa wa Arusha mjini.

7- Ukabila
Hii ni kete iliyokuwa inaratibiwa kwa muda mrefu na wachaga vs waarusha.
ikatumiwa kama kete na kina lowassa na ole medeye.Ni kete yenye mchango katika siasa za arusha ingawa sio ya kuipigia debe sana.

8-Changamoto ya ACT chini ya estomih malla ambaye ni mwanachadema asili aliyetolewa na lema.

Thread hii nitaiupdate tarehe 26 oktoba 2015.


KWA HISANI YA MACHALII WA ARACHUGA!!


#TheArushaWewant
 
wenye chuki na maendeleo kama wewe ndio huanzisha hizi thread, wapumbavu husambaza huu ujumbe na wajinga wasio na data kuhusu hizi taarifa huamini...wewe ni yupi

ukweli upo wazi Lema ni jembe ...itikadi zenu za kumchafua hazitafika popote
 
wenye chuki na maendeleo kama wewe ndio huanzisha hizi thread, wapumbavu husambaza huu ujumbe na wajinga wasio na data kuhusu hizi taarifa huamini...wewe ni yupi

Lema hana uwezo wa kuchaguliwa tena Arusha mjini, wakazi wa huko wanajitambua sana kwa sasa.
 
wenye chuki na maendeleo kama wewe ndio huanzisha hizi thread, wapumbavu husambaza huu ujumbe na wajinga wasio na data kuhusu hizi taarifa huamini...wewe ni yupi

Utamaduni wa JF toka zamani ni kujibu hoja kwa hoja ...hicho ulichopost nakiona kama tangazo la wadhamini!!
 
mimi ni mkazi wa Arusha-Kaloleni,nakuhakikishia Lema ndo mbunge wetu miaka kumi ijayo...hatuna nafasi ya Mafisiem Arusha...
 
Lema hana uwezo wa kuchaguliwa tena Arusha mjini, wakazi wa huko wanajitambua sana kwa sasa.

nshawajua ninyi no chama flani? hivi ka sio lema achaguliwe nani, kwa lipi, na kina nani? hapa Arusha Lema hana Mpinzani.. nipe jina la huyo mpinzani
 
mimi ni mkazi wa Arusha-Kaloleni,nakuhakikishia Lema ndo mbunge wetu miaka kumi ijayo...hatuna nafasi ya Mafisiem Arusha...

Acha uwongo wewe hata hizo nyumba za kaloleni ambazo zimevunjwa kupisha mwekezaji ambaye ni lowassa huzifahamu.
 
nshawajua ninyi no chama flani? hivi ka sio lema achaguliwe nani, kwa lipi, na kina nani? hapa Arusha Lema hana Mpinzani.. nipe jina la huyo mpinzani
Umesoma thread kweli?
 
mimi ni mkazi wa Arusha-Kaloleni,nakuhakikishia Lema ndo mbunge wetu miaka kumi ijayo...hatuna nafasi ya Mafisiem Arusha...

wanafukuza upepo(lema) , Lema ndio chaguo la watu from lemara, njiro, kijenge, ungalimited, mjini, ngaranero, moshono, usa,e.t.c,,,e.t.c
 
Utamaduni wa JF toka zamani ni kujibu hoja kwa hoja ...hicho ulichopost nakiona kama tangazo la wadhamini!!

Tutakua tunarudia hayohayo kila siku?
Mbona Arusha tulisha sema? Akisimamishwa mgombea wa CCM na upinzani wakalisimamisha jiwe, tutalichagua jiwe pasipo na shaka yoyote.
 
Km Monabani kakuhonga ulete uongo wako hapa mwambie amenoa hata cc tuko Arusha utalii kufifia hausababishwi na Lema kwani ccm ndio walikua wanawalipia wazungu harama kutoka huko kwao na km ulivyosema mwenyewe ccm wanafanya makusudi lutokuleta mikutano Arusha ili tuone kikwazo ni Upinzani ili tusichague lkn haitasaidia ndio inawaharibia kabisa.
 
kwa taarifa yako hawa unaosema wafanya biashara wadogo...ni kama Mimi na tunaenda kumpigia kura mbunge wetu Lema
 
wanafukuza upepo(lema) , Lema ndio chaguo la watu from lemara, njiro, kijenge, ungalimited, mjini, ngaranero, moshono, usa,e.t.c,,,e.t.c
USA sio Arusha mjini wewe!!
Moshono wamechoshwa na fujo.
Ungalimited ndio kiwanda kinachomilikiwa na Monaban.
Ngarenaro wanadai soko la kilombero liboreshwe.
Mjini kati ndio CCM ina ofisi zake za mkoa.
Sekei na Aicc ndio wasomi wanaomtaka Monaban
 
Acha uwongo wewe hata hizo nyumba za kaloleni ambazo zimevunjwa kupisha mwekezaji ambaye ni lowassa huzifahamu.

Tunahitaji mabadiliko.. hizo propaganda zetu hazina nafasi...Lema ndo mbunge wa Arusha...bora mkae na familia zenu mfanye mambo ingine bro lema hamumuwezi..
 
Km Monabani kakuhonga ulete uongo wako hapa mwambie amenoa hata cc tuko Arusha utalii kufifia hausababishwi na Lema kwani ccm ndio walikua wanawalipia wazungu harama kutoka huko kwao na km ulivyosema mwenyewe ccm wanafanya makusudi lutokuleta mikutano Arusha ili tuone kikwazo ni Upinzani ili tusichague lkn haitasaidia ndio inawaharibia kabisa.

Unadhani wazungu wanakuja kuangalia maandamano?
 
USA sio Arusha mjini wewe!!
Moshono wamechoshwa na fujo.
Ungalimited ndio kiwanda kinachomilikiwa na Monaban.
Ngarenaro wanadai soko la kilombero liboreshwe.
Mjini kati ndio CCM ina ofisi zake za mkoa.
Sekei na Aicc ndio wasomi wanaomtaka Monaban
Wew kweli Jinga lao...mwambie aliekutuma asubiri tarehe 25 muuone kama wanaArusha tunanunulika...
 
Back
Top Bottom