Sababu za Lema kuanguka Arusha hizi hapa!

Sababu za Lema kuanguka Arusha hizi hapa!

Tunahitaji mabadiliko.. hizo propaganda zetu hazina nafasi...Lema ndo mbunge wa Arusha...bora mkae na familia zenu mfanye mambo ingine bro lema hamumuwezi..
Hizo ni facts sio propaganda
 
Lema hana uwezo wa kuchaguliwa tena Arusha mjini, wakazi wa huko wanajitambua sana kwa sasa.

mkuu hao wakazi ni watu wasiokiwa na fikra za mabadiliko za kuleta maendeleo kama wewe na wengine ambao hata jamfikii asilimia 1 hapa Arusha....
 
USA sio Arusha mjini wewe!!
Moshono wamechoshwa na fujo.
Ungalimited ndio kiwanda kinachomilikiwa na Monaban.
Ngarenaro wanadai soko la kilombero liboreshwe.
Mjini kati ndio CCM ina ofisi zake za mkoa.
Sekei na Aicc ndio wasomi wanaomtaka Monaban
Muwekeni Monaban upinzani tuweka jiwe tu.
 
Ungalimited ndio home jingalao kwani kiwanda kuwa ungaltd ndio tumpe kura? Yy aendelee kutupa unga wa ugali lkn kura nikwa Godbless Jonnathan Lema
 
kujitekenya kunaleta raha gani? kila nikijaribu nashindwa kupata raha. nyie wenzangu mnawezaje kujitekenya?
 
Muwekeni Monaban upinzani tuweka jiwe tu.

Hiyo kauli ilitumika sana Arusha kipindi kile cha chadema asilia.

Soma hoja yangu kwa nini ataanguka nimeongelea combinations of issues na sio sababu moja tu.

Tatizo uwezo wenu wa kuchambua na kuelewa mambo ni mdogo sana.
 
Tutakua tunarudia hayohayo kila siku?
Mbona Arusha tulisha sema? Akisimamishwa mgombea wa CCM na upinzani wakalisimamisha jiwe, tutalichagua jiwe pasipo na shaka yoyote.

Aaaaaah mkuu hayo ni matusi ina maana jiwe lina mvuto kuliko ccm?
 
USA sio Arusha mjini wewe!!
Moshono wamechoshwa na fujo.
Ungalimited ndio kiwanda kinachomilikiwa na Monaban.
Ngarenaro wanadai soko la kilombero liboreshwe.
Mjini kati ndio CCM ina ofisi zake za mkoa.
Sekei na Aicc ndio wasomi wanaomtaka Monaban

Wana Arusha tunamtaka lema pigia mstari hao kina escrow washatuibja sana...VIVA LEMAAAAAA
 
Hii propaganda ya kwamba arusha imekosa mapato kutokana na utalii huwa hata nikiiangalia nacheka, na huyo mgombea wa ACT naye namuona anaitumia sana huku akijifanya eti amani ya arusha imepotea. Ukweli ni kwamba sisi tunapata hela zetu kutokana na sekta ya utalii, tunapata hela za kutosha na watalii wanakuja kwa wingi Arusha. Ukitaka kuamini angalia pato la utalii utaona Arusha imechangia kwa kiasi gani. Tuje kwenye mikutano ya hapa Arusha, huenda ni kweli mikutano ya arusha imepungua lakini ni kwa ajili ya fitina za kisiasa ili Lema aonekane hafai. Na hata hivyo sisi wakazi wa Arusha hatutaki mikutano kama hisani, mnaweza kupeleka popote nchi hii kwani ni pato la nchi nzima hata wafanyie Dar, Mwanza nk. Kama ni kweli mnalosema Lema amesababisha uchumi wa Arusha kushuka na mnadhani sisi ni wajinga ngoja nikueleze, hivi leo ni zaidi ya miezi miwili kila siku kuna mgao wa umeme, mgao huu umekuwa na matokeo na hasara ya wazi kuliko hizo propaganda mnazotuletea hapa. Mgao huu umekuwa ukijirudia mara kwa mara katika kipindi chote cha miaka mitano na wananchi wameendelea kupata hasara ya wazi bila serekali ya ccm kufidia hasara hiyo. Sasa tuwaulize huu mgao wa umeme ulioletwa na serekali ya ccm na Lema kuwa mbunge wa Arusha ni kipi kimewapa wananchi wa Arusha hasara ya wazi?

Mnaosema arusha hakuna amani ni nyie mnaokuja na hadhithi za kiccm lakini sisi wakazi wa Arusha tunajua waliokuwa wanavunja amani ni jeshi la polisi kwa kuagizwa na ccm kisa mbunge wa hapa arusha mjini hakubaliani na maslahi yao. Hivyo kama kweli mnauchungu na sisi tunaomba tuwaambie Arusha kuna amani ila kuna mgao wa umeme ulioletwa na serekali ya ccm, na kama ni watalii wapo wa kutosha kwani nchi hii ina amani na wataliii wanalifahamu hilo. Hizo taasisi za serekali zinazogoma kuleta mikutano arusha kwa sababu za kisiasa zinaweza kuendelea hivyohivyo kwani hata ukiangalia mikutano yao mingi haina tija zaidi ya kujiandikia sitting allowance nyingi na kuishia kumbebesha mwananchi mzigo. Na tunampongeza sana Lema kwani ametekeleza majukumu yake matatu vyema ya kibunge kama nitakavyoyataja hapo chini
  1. Kutuwakilisha bungeni
  2. Kutunga sheria bungeni
  3. Kuisimamia na kuishauri serekali.
 
tusubiri tar 25 wananchi waamue wenyewe na si kuwasemea
 
Ni kweli, kuna kipindi wanaarusha waliazimia kumuondoa LEMA, lakini kwa bahati mbaya, huu upepo wa mabadiliko uliopo sasa, hautaruhusu LEMA aondoke, Profesa jingalao mark my words, utaniambia ifikapo oktoba 26.

Hata hivyo LEMA alisharekebisha zile kasoro ndogo ndogo zilizokuwa zinamtia madoa!
 
Last edited by a moderator:
Jamani Watz wenzangu tuwe wa kweli kwaani maeneo yasiyo na maandamano kama songea Rukwa Tabora je huko kumeendelea kuliko Arusha au ni propagada za kulitaka jimbo la Arusha?
 
Hiyo No.6 ukisema Swahiba unakosea SANA Jingalao sema Monabani kaajiriwa na Lowassa kucmamia kiwanda inshort ni Manager wa kiwanda hata cc tunajua na km alimsaidia Batilda jiulize ALISHINDA hata Arumeru c alikua anamsapoti Mkwe wake ALISHINDA? Lawassa mwenyewe alikua km kifaranga kilichonyeshewa na mvua tumestiri halafu alete fitna weeee huo ni Ujinga umeandika.
 
Ni kweli, kuna kipindi wanaarusha waliazimia kumuondoa LEMA, lakini kwa bahati mbaya, huu upepo wa mabadiliko uliopo sasa, hautaruhusu LEMA aondoke, Profesa jingalao mark my words, utaniambia ifikapo oktoba 26.

Hata hivyo LEMA alisharekebisha zile kasoro ndogo ndogo zilizokuwa zinamtia madoa!

Nashukuru kwa kukubali lile ninalolisema japo kwa imani yako unahisi yameisha.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo No.6 ukisema Swahiba unakosea SANA Jingalao sema Monabani kaajiriwa na Lowassa kucmamia kiwanda inshort ni Manager wa kiwanda hata cc tunajua na km alimsaidia Batilda jiulize ALISHINDA hata Arumeru c alikua anamsapoti Mkwe wake ALISHINDA? Lawassa mwenyewe alikua km kifaranga kilichonyeshewa na mvua tumestiri halafu alete fitna weeee huo ni Ujinga umeandika.
Naona mmeanza kuja na majibu ya hoja
 
Ndugu zangu,Tafiti za Twawezwa na Ipsos zisitutoe katika “Mstari” wa kutafakari “AHADI” za CCM za mwaka 2010 na Zile mpya za John Magufuli kama zisizotekelezeka.Ukitaka kujua kama Magufuli atatekeleza ahadi zake ANGALIA kama CCM ya Kikwete ilitekeleza walichowaahidi WATANZANIA wanaowaita “Wapumbavu,Malofa,Mbumbumbu na Kunguni kwa kuwa tu wepesi KUSAHAU!!!Kwa kuwa ninyi mpo sehemu mbalimbali TANZANIA thibitisha kama ahadi hiyo imetekelezwa ama kuna ahadi aliahidi sijaiweka hapa na HAIJATEKELEZWA!!!!
1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora (HAJATEKELEZA)
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini (HAJATEKELEZA)
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria- Igunga (HAJATEKELEZA)
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga (
HAJATEKELEZA)
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
(HAJATEKELEZA)
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
(HAJATEKELEZA)
7. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma (HAJATEKELEZA)
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera (HAJATEKELEZA)
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi- Kagera (HAJATEKELEZA)
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba- Bukoba Mjini (HAJATEKELEZA)
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini (HAJATEKELEZA)
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
(HAJATEKELEZA)
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
(HAJATEKELEZA)
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu- Kagera
(HAINA MENO KABISA NA IMEJAA RUSHWA)
15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya (MAUAJI YANAENDELEA)
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba- Kagera (HAJATEKELEZA NA ZILIZOPO MBOVU HAZIFAI)
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali (HAJATEKELEZA)
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika- Mwanza (HAJATEKELEZA NAVYAMA VILIVYOPO VINA HALI MBAYA NA VINGI VIMEKUFA KABISA)
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
(HAJATEKELEZA)
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita (
21. Kulinda muungano kwa nguvu zote- Pemba
(KERO HAZIJATATULIWA)
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
(HAJATEKELEZA)
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa- Mbeya mjini
(HAJATEKELEZA)
24. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa (HAJATEKELEZA)
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea (HAJATEKELEZA NA WALIMU WAMEPUUZWA WANAULIZA -SHEMEJI UNATUACHAJE?)
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya (HAJATEKELEZA)
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
(HAJATEKELEZA)
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
(HAJATEKELEZA)
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
(HAJATEKELEZA)
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
(HAJATEKELEZA)
31. Kuboresha barabara za Igunga -
Tabora (HAJATEKELEZA)
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu (AMETEKELEZA)
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini (HAJATEKELEZA)
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)- Hydom Manyara (HAJATEKELEZA)
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa-Musoma (HAJATEKELEZA CCM NDIO CHANZO CHA CHOKOCHOKO)
36. Kulinda haki za walemavu- Makete (HAJATEKELEZA,WANATUMIKA KWENYE KAMPENI TU)
37. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini (HAJATEKELEZA)
38. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha (HAJATEKELEZA)
39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini (HAJATEKELEZA)
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni- Kigoma– Kaliua,Tabora (HAJATEKELEZA)
41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi- Arusha Mjini
(ANGALAU JAPO KIWANGO HAKIRIDHISHI)
42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
(HAJATEKELEZA)
43. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido
(HAJATEKELEZA)
44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
(HAJATEKELEZA)
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu 2010 mkoani Arusha – Arusha mjini
(HAJATEKELEZA NCHI IPO GIZANI KWA MGAO AMBAO HAUJATANGAZWA)
46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo- Busekera, Wilaya ya Musoma, .
(HAJATEKELEZA)
47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido (HAJATEKELEZA)
48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti – Ngorongoro (HAJATEKELEZA)
49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
(HAJATEKELEZA)
50. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini (HAJATEKELEZA)
51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
(HAJATEKELEZA NA HALI NI MBAYA SANA)
52. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
53. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania- Iringa
(HAJATEKELEZA)
54. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda (HAJATEKELEZA - CHOKOCHOKO ZA CCM ZINAHATARISHA AMANI)
55. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara (HAJATEKELEZA)
56. Kuwapa wanawake nafasi zaidi- Kilolo ,Iringa (ANGALAU)
57. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
(HAJATEKELEZA)
58. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa- Kabandamaiti mjini Zanzibar (HAJATEKELEZA)
59. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti (HAJATEKELEZA)
60. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
(HAJATEKELEZA)
61. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
(HAJATEKELEZA)
62. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
(HAJATEKELEZA)
61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
(MISAADA YA VYANDARUA NA VYOO KWA MSAADA WA WATU WA MAREKANI)
62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam (HAJATEKELEZA)
63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara (HAJATEKELEZA)
64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
(HAJATEKELEZA)
65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa- Kibaha. (HAJATEKELEZA)
66.Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -
Kibaha (HAJATEKELEZA) N.K
CCM HAIAMINIKI TENA,WAKATI UMEFIKA CCM INAPASWA ITOLEWE KWA NJIA YA KURA MADARAKANI?..KWA NINI WASITEKELEZE AHADI HIZI KABLA YA KUAHIDI ZINGINE?.
...CHAGUA LOWASSA..CHAGUA UKAWA (CHADEMA/CUF/NLD/NCCR MAGEUZI)
 
Back
Top Bottom