Sababu za kwa nini huwa tunachepuka

Sababu za kwa nini huwa tunachepuka

There you are. Kuna watu wengi wameacha kujisimamia kisa eti waliokuwa wakiwaangalia kama kioo chao nao wanacheat. Hii kitu ni swala binafsi... halitegemeani na mtu mwingine yeyote ili wewe uwe utakavyo.

Kuna kaupepo kanapita sasa hivi best... ''SI KILA MTU ANAFANYA?'' unakaa na vijana unawasikiliza unashangaa kwa kweli... hawajifikirii wao kama wao tena, wanaangalia wangapi wanafanya na wangapi hawafanyi... Kama wengi wanafanya HIO NI HALALI. uhalali wa kinachofanywa hakiwahusu. Huu ndio mtazamo wa jamii kwa sasa.
(Iwe ni wizi wa maofisini, mali ya uma, kuingiliana kinyume na maumbile, ku-cheat, wake za watu, kamari... you name them)

There we go.........
It begins with you.
mimi nataka nini? nafanya nini? haijalishi mwenzio anataka/anafanya nini. I like this
 
There you are. Kuna watu wengi wameacha kujisimamia kisa eti waliokuwa wakiwaangalia kama kioo chao nao wanacheat. Hii kitu ni swala binafsi... halitegemeani na mtu mwingine yeyote ili wewe uwe utakavyo.

Kuna kaupepo kanapita sasa hivi best... ''SI KILA MTU ANAFANYA?'' unakaa na vijana unawasikiliza unashangaa kwa kweli... hawajifikirii wao kama wao tena, wanaangalia wangapi wanafanya na wangapi hawafanyi... Kama wengi wanafanya HIO NI HALALI. uhalali wa kinachofanywa hakiwahusu. Huu ndio mtazamo wa jamii kwa sasa.
(Iwe ni wizi wa maofisini, mali ya uma, kuingiliana kinyume na maumbile, ku-cheat, wake za watu, kamari... you name them)
Umejitahidi kwenda mbali best, I like that.
Nakubaliana nawe kabisa hili la kujiingiza kwenye jambo sababu tu ya kuamini kila mtu anafanya.....
 
Thank you my friend and I hope your week is off to an awesome start!

Thanx for a useful thread...now mke wangu Kaunga akisikia mimi na wewe tuna chepuka ajue tu ni natural...nampenda na simuachi..na wewe unampenda mumeo na humuachi.. just a to try new taste..
 
Last edited by a moderator:
There you are. Kuna watu wengi wameacha kujisimamia kisa eti waliokuwa wakiwaangalia kama kioo chao nao wanacheat. Hii kitu ni swala binafsi... halitegemeani na mtu mwingine yeyote ili wewe uwe utakavyo.

Kuna kaupepo kanapita sasa hivi best... ''SI KILA MTU ANAFANYA?'' unakaa na vijana unawasikiliza unashangaa kwa kweli... hawajifikirii wao kama wao tena, wanaangalia wangapi wanafanya na wangapi hawafanyi... Kama wengi wanafanya HIO NI HALALI. uhalali wa kinachofanywa hakiwahusu. Huu ndio mtazamo wa jamii kwa sasa.
(Iwe ni wizi wa maofisini, mali ya uma, kuingiliana kinyume na maumbile, ku-cheat, wake za watu, kamari... you name them)
but ukiwasoma vizuri hawa wanachosema best, siyo kwamba ni kujustfy kinachofanywa na wengi but kusema kuwa ku-cheat haimaanishi hamna happy relationship. hata wale ambao wapo happy wanafanya hivyo, kwa nini? Nyani Ngabu kajitahidi sana kuelezea......
hatutetei kuwepo kwa huo udanganyifu, but tunaangalia kwa nini huo udanganyifu unakuwepo....
 
Last edited by a moderator:
Kabisa dada yangu.... nimelifanyia uchunguzi saa hili swala.... we ukiona mtu anafanya kitu cha kiajabu jaribu tu kumtafutia pozi siku umuulize kwa nini anafanya hiko anakofanya, then utaniambia.

Lakini pia kwa upande wa pili, Wale watu tuliowategemea kuwa mfano haswa viongozi wa dini wana mchango mkubwa sana kumumonyoka kwa maadili siku hizi maana kama waumini wanasikia viongozi wao wamefumaniwa, wana kesi za ulawiti hadi mahakamani, wamechukua wake za watu, wamebaka, wametembea na waumini wao, madawa ya kulevya... unafikiri wanachi wa kawaida watakuwaje?

Maana hata maandiko yanasema ''MCHUNGAJI WA KONDOO AKIPIGWA, KONDOO HUTAWANYIKA'' nawalaumu wale wachache wanaofanya vitendo hivi, kwa kweli wana sehemu kuubwa sana kwenye haya tunayoyaona kwa sasa.
Umejitahidi kwenda mbali best, I like that.
Nakubaliana nawe kabisa hili la kujiingiza kwenye jambo sababu tu ya kuamini kila mtu anafanya.....
 
Thanx for a useful thread...now mke wangu Kaunga akisikia mimi na wewe tuna chepuka ajue tu ni natural...nampenda na simuachi..na wewe unampenda mumeo na humuachi.. just a to try new taste..
ha haaaa, wataka my dearest Kaunga anipotezee for no reason?
una bahati wakezo wote wanalijua hili na wameamua kuishi na hili.
Just having fun, lol!
 
Last edited by a moderator:
Thanx for a useful thread...now mke wangu Kaunga akisikia mimi na wewe tuna chepuka ajue tu ni natural...nampenda na simuachi..na wewe unampenda mumeo na humuachi.. just a to try new taste..

Wow wow wow...Bossman, mbona ni kama ulikuwa unamjibu FP lakini ukaninukuu mimi.....

Boy you're about to start a contagion of rumors now...hahahaaaa
 
Kabisa dada yangu.... nimelifanyia uchunguzi saa hili swala.... we ukiona mtu anafanya kitu cha kiajabu jaribu tu kumtafutia pozi siku umuulize kwa nini anafanya hiko anakofanya, then utaniambia.

Lakini pia kwa upande wa pili, Wale watu tuliowategemea kuwa mfano haswa viongozi wa dini wana mchango mkubwa sana kumumonyoka kwa maadili siku hizi maana kama waumini wanasikia viongozi wao wamefumaniwa, wana kesi za ulawiti hadi mahakamani, wamechukua wake za watu, wamebaka, wametembea na waumini wao, madawa ya kulevya... unafikiri wanachi wa kawaida watakuwaje?

Maana hata maandiko yanasema ''MCHUNGAJI WA KONDOO AKIPIGWA, KONDOO HUTAWANYIKA'' nawalaumu wale wachache wanaofanya vitendo hivi, kwa kweli wana sehemu kuubwa sana kwenye haya tunayoyaona kwa sasa.
wanasema tusifwate matendo yao but maneno yao, I believe this.
They are just human as we are.
 
kwa misingi hio Fixed Point, Cheating inakuwa ni tabia ya mmoja wapo.... kwake huo awe na happy relatioship au vinginevyo yeye kutoka nje ni kawaida, either ni mazoea yake au tamaa zake tu. nakubaliana na hilo.

Personal commitment inahusika sana japo kuna wengine wanacheat kutokana na kuwa na mahusiano yasiyo na furaha... kwa hio mtu huyu anatka nje kwa gia ya kutafuta furaha ... lakini baadae anakuta hali imeendelea kua mbaya kwa sasababu anahangaika na matokeo tu bila kuangalia kiini cha tatizo.
but ukiwasoma vizuri hawa wanachosema best, siyo kwamba ni kujustfy kinachofanywa na wengi but kusema kuwa ku-cheat haimaanishi hamna happy relationship. hata wale ambao wapo happy wanafanya hivyo, kwa nini? Nyani Ngabu kajitahidi sana kuelezea......
hatutetei kuwepo kwa huo udanganyifu, but tunaangalia kwa nini huo udanganyifu unakuwepo....
 
Last edited by a moderator:
Nyaningabu kingereza chako huwa kinanikosha ,yaani i wish ...:A S 11::A S 11::A S 11::A S 11: huyu mkoloni angenikoma ,najua cha kwangu

Oh ahsante sana FL1.

Pongezi nyingi sana ziwaendee walimu wangu Philip Pullman enzi za Bishop Kirk Middle School na Ms. Godinho pale SRSS.
 
Wow wow wow...Bossman, mbona ni kama ulikuwa unamjibu FP lakini ukaninukuu mimi.....

Boy you're about to start a contagion of rumors now...hahahaaaa
ha haaaa, mi simooooooo.......
sijui ndo uliberali? mi sijui. nililiona hili nikachuna, ngoja wakeze waje waone.
 
Rafiki Fixed Point sababu za waliomo ndani ya ndoa ni nyingi na zinaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu. Kwa mfano mwingine anaweza kukwambia nimempenda sana tu huyu kaka/dada yaani ameiteka akili kiasi ambacho siwezi kabisa kuukwepa ukweli wa hili.

Mwingine atasema mke/mume hanijali/hanithamini kabisa mama mkewe/mumewe hana muda na mkewe/mumewe kabisa akirudi nyumbani kila siku kanuna na saa zote ni mtu wa kufoka.

Mume anaweza kudai nyumbani mke hamshugulikii kwa lolote lile kila kitu kinafanywa na HG yeye yuko busy mitandaoni, kwenye simu au akifuatilia vipindi mbali mbali kwenye TV. Mke naye anaweza kudai mume akitoka kazini ni kwenda kula nyama choma na moja moto moja baridi akirudi hapa ni saa tano/sita za usiku kuja kuweka mbavu tu na kila siku iendayo kwa mungu maisha yetu ndiyo hivyo. Hatujawahi kukaa mezani na mume kula chakula chochote cha siku kuanzia kifungua kinywa, chakula cha mchana au cha usiku (for those who afford 3 meals per day) atajibaraguza baraguza hapa siku za sikukuu labda ndio tutapata kifungua kinywa pamoja na chakula cha mchana baada ya hapo huyoo anaishia anakokujua yeye kurudi ndio mpaka usiku wa manane. Mume hajawahi kuniambia "I love you" hatujawahi kutoka kwenda popote pale iwe ni movie, club au kwenda kula nje au hata kwenye nyama choma pamoja. Mume/Mke akiwa na marafiki anakuwa na furaha kubwa sana vicheko na muongeaji kama yeye hakuna tena lakini akiwa nyumbani na mkewe/mumewe ni visirani na kununa saa zote.

Sababu kama hizi zinaweza kabisa kuwa chanzo kwa mume/mke kuamua kuwa na mchepuko na kama mchepuko ukiweza kuteka akili ya mume/mke husika basi wakati mwingine hata ndoa huvunjika unasikia fulani anaachana na mkewe/mumewe kasha baada ya muda unasikia fulani siku hizi yuko na aliyekuwa mke/mume wa fulani au wanaweza kuendeleza mchepuko wa hali ya juu mpaka watu wakadani hao ni mke na mume kumbe ni mchepuko tu.

Zamani kabla ya kuwepo kwa mtandao hili la kucheat kwa wanandoa lilikuwa gumu kutokana na mawasiliano kutokuwa rahisi. Pamoja na kuwa kucheat kulikuwepo lakini si katika kiwango kikubwa kama ilivyo sasa baada ya mawasiliano kurahisishwa mno na mtandao. watu wanaweza kuwasiliana kupitia text messages, emails, twitter, FB, whatsapp n.k. bila wenzi wao kushtuka kuhusu nini kinachoendelea ndani ya ndoa zao. Na siku hizi hata baadhi ya wanawake na wanaume wanadai ni adhabu kubwa kuwemo kwenye ndoa na mtu yule yule kwa miaka 20/30/40 na kuendelea wanataka ndoa za mikataba au ndoa za wazi (open marriages) kila mtu anachepuka kwa raha zake na ndoa inaendelea...Hmmmm!!!. Mnapiga mkataba wenu wa miaka mitatu, miaka mitatu ikikatika kama bado hamjazinguana mnakaa chini kama kuna umuhimu wa kuongeza tena miaka mitatu/miwili/mmoja au kila mtu achukue 50 zake. Taasisi ya ndoa kwa maoni yangu inakufa taratibu miaka 50 ijayo si ajabu hizi ndoa kama tunavyozifahamu leo hii zitakuwa hazipo labda kutakuwa na hizo ndoa za mikataba au sijui kutakuwa na mfumo upi wa maisha kati ya mwanamke na mwanaume waliopendana. Katika nchi za wenzetu takwimu zinaonyesha idadi ya ndoa katika miaka ya karibuni imepungua sana na zitazidi kupungua. Haya mchango wangu huo wa senti 50. Uwe na jioni njema.

Wapendwa wangu habari za siku nyingi.
Nimekutana na hili andiko sehemu nikaona tushirikishane.
Nadhani itakuwa vizuri sana kama kila mtu atajisomea mwenyewe na kujielewesha kwa kadiri atakavyojaliwa kupitia huu ukurasa.

Kwa kifupi tu wanaeleza kuwa hata wenzi ambao wapo kwenye mahusiano yenye furaha wanatoka nje ya mahusiano (spouses in happy marriages [I can add; relationships] have affairs).
Kwa nini tunafanya hivyo?
Tunatafuta nini?
Tunakubaliana na sababu ambazo hawa wenzetu wamezitoa (kwa wale watakaojaliwa kusoma)?
Huko ni Amerika (By the way, waliohojiwa na mhojiji ni mzungu wala siyo wabongo/afrika; so zile arguments za kwamba mzungu akikupenda ha-cheat zisiwepo hapa), vipi huku kwetu?
Nini kifanyike?
Nawasilisha kwa mjadala

Source:
slate

Esther Perel on affairs: Spouses in happy marriages cheat and Americans don’t understand infidelity.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom