Sababu za kwa kwanini kuku hushusha utagaji

farmersdesk

Senior Member
May 26, 2012
164
120
Sababu 10 Za Kuku Kupunguza Utagaji Mayai Na Nini Ufanye Kuongeza Uzalishaji Wa Mayai | Mshindo media.

Kupungua kwa mayai yanayo zalishwa kwa siku katika shamba lako la kuku watagao mayai ni dalili moja wapo inayo onesha kwamba kunatatizo katika kundi lako la kuku. Kulingana na utafiti ulio fanywa na shirika la FAO una onesha kwamba kwa kawaida kuku aliye fikia umri wa miezi mitano au sita nakuendelea inatakiwa atage yai moja kila baada ya saa 24 hadi 26, kwa maana hiyo kila siku kuku wako inatakiwa atage yai moja.

Kama vile tunavyo kuwa makini kufuatilia kinyesi cha kuku kugundua kama kuku anaumwa au anatatizo vivyo hivyo tunapaswa kufuatilia uzalishaji wa mayai kwa siku. Mabadiliko katika uzalishaji wa mayai yanaweza kusababishwa na magonjwa, mabadiliko ya tabia, mazingira na stress. Ilikujua sababu haswa inayo badilisha uzalishaji wa mayai katika kundi lako la kuku (flock) ina takiwa urejee na ukague historia ya kundi lako na pia ukague hali ya kuku wote(physical assessment) huku ukijiuliza maswali yafutayo;-

· Je kuna kuku wapya au wageni umewaongeza kwenye kundi lako?, kwasababu kuku wageni huweza kuwa chanzo cha kuleta magonjwa kama sehemu walio toka kuna mlipuko wa ugonjwa.

· Je kuna mabadiliko yoyote katika aina ya chakula unachowalisha, mabadiliko ya makazi (banda) au mpangilio ndani ya banda, mabadiliko ya hali ya hewa, masaa ya mwanga na giza, mabadiliko kwenye kinyesi?.

· Je kunadalili yoyote ya uwepo wa wanyama walao mayai au kuku (predators) au magonjwa ya kuku?. Kunawakati mwingine unaweza dhani kwamba kuku hatagi kumbe sivyo ila kuna wanyama kama paka, mbwa na vicheche wanakula mayai bila wewe kujua.


Baada ya kujiuliza maswali kama hayo mara nyingi kisababishi haswaa cha tatizo hili hujulikana, zifuatazo ni sababu kumi zinazo weza kusababisha uzalishaji wa mayai kushuka katika kundi lako la kuku wa mayai.

1. KUPUNGUA KWA MASAA YA MWANGA (LIGHTING).

Mwanga husisimua “ pituitary gland”kwenye kuku ili kuchochea uzalishaji wa mayai. Mtiririko mzuri wa utagaji wa mayai kwa kuku huhitaji masaa 14 mpaka 16 ya mwanga, kwa mfano kuna baadhi ya majira ya mwaka ambapo jua huwahi kuzama na kuchelewa kuchomoza hivyo husababisha masaa ya mwanga kuwa machache kwa siku, hivyo huathili uzalishaji wa mayai kwa kuku.

Ili kuondoa tatizo hili la upungufu wa masaa ya mwanga unaweza kuweka taa za umeme(artificial light) ndani ya banda lako la kuku wa mayai na uziwashe baada tu ya giza kuingia kwa masaa mawili hadi matatu. Kutokana na utafiti uliofanywa na shirika la FAO una onesha kwamba kuwapa kuku wako mwanga kwa msaa mawili hadi matatu huweza kuimalisha utagaji wa mayai kwa asilimia 20 hadi 30, hii inaonesha ni jinsi gani mwanga ni muhimu sana kwa kuku wa mayai.

2. STRESS NA MABADILIKO MBALIMBALI.


Ni rahisi sana kwa kuku kuathirika na stress na hii hupelekea kupunguza utagaji wa mayai, kwa kawaida kuku hapendi mabadiliko, yanaweza kuwa mabadiliko ya chakula, mpangilio wa vyombo vya chakula na maji ndani ya banda na kuwa hamisha kwenda banda jingine, pia stress inaweza sababishwa mambo kama kusumbuliwa na minyoo, kupe, viroboto, na chawa, joto kari, kelele za wanyama kama mbwa au paka, kelele za machine au magari zisizo isha, yote hayo yanaweza sababisha stress kwa kuku na hatimaye kuathili utagaji wa mayai.

3. MAGONJWA.

Kuku anapo shambuliwa na magonjwa mara nyingi hudhoofu na kukosa nguvu mwilini pia hupoteza hamu ya kula, katika wkati kama huu kuku hupunguza utagaji au kusismisha kabisa utagaji kutegemeana na namna ugonjwa ulivyo muathili. Kuepuka matatizo haya hakikisha kwamnba kuku wanapewa chanzo zote wanazo stahili, watibu kwa wakati pale wanapo ugua na pia jitahidi sana kuzuia vyanzo vya magonjwa ambavyo vipo ndani uwezo wako kama mfugaji.

4. UMRI WA KUKU

Kwa kawaida kuku anapo fikisha umri wa miaka miwili uzalishaji wake wa mayai hupungua, jinsi anavyo zidi kuwa na umri mkubwa uzalishaji wa mayai hupungua lakini huwa wanataga mayai makubwa kiumbo kuliko kuku wadogo. Ili kuongeza faida na ufanishi katika mradi wako hakikisha kwamba unaondoa kuku walio zeka na kuwaleta wengine ambao hawajazeka, kwasababu hao kuku wazee wanaweza wakawa wanakula chakula kingi lakini hawatagi hivyo husababisha hasara ndani ya shamba.

5. UKOSEFU WA MAJI

Upatikanaji wa maji safi na salama ni wa muhimu sana katika mfumo wa kutengeneza mayai kwa kuku. Uzalisha wa mayai huathirika endapo kuku wako hawatakunywa maji ya kutosha pengine kwa sababu ni machafu, hayajawekwa mahala ambapo panafikika vizuri hivyo kuku wanashindwa kunywa kiurahisi au hayana radha halisi ya maji kutokana uchafu au vitu ambavyo vimechanganywa ndani yake. Hakikisha kwamba maji safi na salma yanapatikana ndani ya banda muda wote na yaweke mahali ambapo panafikika na pia hakikisha kwamba idadi ya vyombo vya maji ina kidhi mahitaji kulingana na idadi ya kuku wako.

6. JOTO (TEMPERATURE).

Mtiririko wa utagaji wa mayai kwa kuku waweza athiriwa na joto katika mazingira husika. Kwa kawaida ili kuku aendele kutaga katika mtiririko wake wa kawaida yani yai moja kila siku anahitaji joto lisiwe chini ya 11 oC na lisiwe zaidi 28 oc .

&t;div dir="ltr">Jedwali apo chini lina onesha matokea ya viwango tofauti tofauti vya joto kwa kuku wako katika uzalishaji.

7. MATATIZO KATIKA MFUMO WA UZAZI

Magojwa au kasoro za kimaumbile katika mfumo wa uzazi pia zaweza sababisha kushuka kwa utagaji wa mayai, kwahiyo hakikisha kwamba kuku wako wa mayai hana matatizo ya kimaumbile. Tafuta msaada wa dakitari wa mifugo kama kuku ata onekana kuwa amevimba au ametuna kama mfano wa puto lenye maji upande wa chini wa tumbo au unaweza ona kama kuna dalili ya yai kukwama .

8. UPUNGUFU WA VIRUTUBISHO.

Upungufu wa virutubisho muhimu katika chakula cha kuku wa mayai husababish kupungua kwa uzalishaji wa mayai. Hakikisha kwamba kuku wako wanapewa chakula ambacho kina virutubisho vyote ambavyo ni vya muhimu kwake. Ili kuondoa tatizo hili unaweza kununua chakula kutoka madukani ambacho kimeshafanyiwa mchanganyiko maalumu wa virutubisho vinavyo faa kwa kuku wa mayai au ilikupunguza ghalama unaweza kujifunza fomula mbalimbali za mchanganyiko wa chakula na ukatengeneza chakula chako mwenyewe kwajili ya kuku wako. Katika chakula hicho cha kukuk wa mayai hakikisha kwamba kuna kiwango cha kutosha cha protini, madini kashiamu na wanga.

9. KUPUKUTISHA MANYOYA (MOLTING).

Hii ni tabia ya asili ambayo hutokea kwa kuku katika hatua mbailimbali ya ukuaji, baadhi ya kuku wanawza kupukutisha manyoya mengi kwa wakati mmoja na akabaki wazi baadhi ya sehemu za mwili wake kama mgongo na shingo au akapukutisha manyoya yake kidokidogo huku mengine yakiota, ambapo haitakuwa rahisi kwa wewe kugundua kama yupo katika hatua hii ya kupukutisha manyoya.

Katika kipindi hiki kuku hupunguza au kusimamisha kabisa utagaji, hii hutokana na ukweli kwamba kipindi hiki kuku hutumia protini nyingi na nguvu nyingi kuotesha manyoya mapya mwilini mwake kuliko kuzalisha mayai. Hali hii ni ya asili na haizuiliki kinacho takiwa katika kipindi hiki ni kujitahidi kumpa chakula ambacho ni bora(balanced diet).

10. HALI YA KUATAMIA.

Hi ni hali ya kuku kulalia mayai yake ili kuyapa joto na kuruhusu ukuaji wa kiini tete (embryo) ndani ya yai. Hali hii ni kawaida kwa kuku wetu wa asili. Kuku anapo anza kuatamia huacha kutaga mayai, pia kama kuku huyu anaye atamia yupo ndani ya banda ambalo kuku wengine bado wanaendelea kutaga, hupelekea kuku wengine kupatwa na hali hii pale tu wanapo muona ka atamia. Kwahiyo ni vyema kuku wanao atamia wasikae kweny banda moja na wale wanao endelea
instagram farmersdesk -Tanzania
 
Back
Top Bottom