Sababu za kuoa au kuolewa

Sababu za kuoa au kuolewa

Kupata life partner ambae moyo na mwili unakubali unamuhitaji,kuzaa watoto (they bring more hapiness and trouble perhaps,but inakuongezea bidii cz unajua una mtoto wa kumtunza),heshima kwenye jamii (u may be taken more seriously than zamani,uhuni basi tena,japo mhhh sio wote),kutake responsibility (km umempa binti ujauzito) flaws and all naona life is a lot better when u enjoy and face it with ur family or loved ones,na badae ukizeeka walau u got people to take u for a walk or drive u to the hospital and u can look back and be proud u got a family...ndo maisha yenyewe hayo...
 
Kwa sababu amempata wa kumuoa/kuolewa naye....
 
wengine hawaamui,

wanaamuliwa na wazazi wao ama kufungishwa ndoa za mkeka kabisa!

sijui niko nje ya mada ama vipi? lols!

Natafuta huyo mwanamke wa kufungishwa nae ndoa ya mkeka, maana ni very cost effective. Hakuna mahari, sijui mkaja wa bibi, mara msuli wa baba... Aah, raha sana. Nampata wapi huyo, tena aliyebomba?
 
hivi kwann mtu anaamua kuoa au kuolewa?
Hili swali liwafikie wanandoa wanaochepuka

Wanaopiga wake zao

wasio wasaidizi kwa wenzi wao

Wasio tayari ku sacrifice kwa ajili ya mwenza

Wanaoenda kinyume na kiapo cha ndoa na promises baina yao
 
Wanaamua kuoa na kuolewa kutimiza wajbu na kutoa gundu,ingekua ni kwaajil ya kugegedana tu wangetulia na ndoa zao na michepuko isingekuepo!
 
Natafuta huyo mwanamke wa kufungishwa nae ndoa ya mkeka, maana ni very cost effective. Hakuna mahari, sijui mkaja wa bibi, mara msuli wa baba... Aah, raha sana. Nampata wapi huyo, tena aliyebomba?

Nenda katembee na mtoto wa shehe utapata ndoa isiyokuwa na gharama
 
To make it official in the eyes of the lord, government or community, inategemea na imani ya mtu, ukizingatia huyo unayembeba ni mtoto wa mtu kwahio ndoa ndio itakupa baraka zote kutoka kwa wazazi, ndugu na jamii
 
Kuoa/kuolewa ni makubaliano/maridhiano ya watu wawili kuhitaji kuishi pamoja kama mke na mume kwenye shida na raha,japo kwenye shida sikuhizi watu hawazingatii....Sababu za kuoa
/kuolewa zipo kibaaaooo kila mtu na janga lake litakalomkuta na kuamua koa/kuolew
1.Kuchoka kukaa peke yako
2.kupata mtu wa kufua /kuchek hali ya nyumba
3.Mimba zisizotaraji/ za kutegesheana.
4.Mapenzi ya dhat kwa wahusika
5.Uchumi..Dada/kaka anajiweza sasa asaidie kukutoa kwenye umaskini.
6.Wazazi kulazimisha
7.Mila za kabila flani ili kuonekana mkubwa lazima uoe.
8.Baby,honey kulazimisha ndoa....
 
1 Basi kwa habari ya mambo yale
mliyoandika, ni heri mwanamume
asimguse mwanamke.
2 Lakini kwa sababu ya zinaa kila
mwanamume na awe na mke
wake mwenyewe, na kila
mwanamke na awe na mume
wake mwenyewe.
3 Mume na ampe mkewe haki
yake, na vivyo hivyo mke na ampe
mumewe haki yake.
4 Mke hana amri juu ya mwili
wake, bali mumewe; vivyo hivyo
mume hana amri juu ya mwili
wake, bali mkewe.
5 Msinyimane isipokuwa
mmepatana kwa muda, ili mpate
faragha kwa kusali; mkajiane
tena, Shetani asije akawajaribu
kwa kutokuwa na kiasi kwenu.
6 Lakini nasema hayo, kwa kutoa
idhini yangu, si kwa amri.
7 Ila nipendalo ni kwamba watu
wote wawe kama mimi nilivyo;
walakini kila mtu ana karama
yake mwenyewe itokayo kwa
Mungu, huyu hivi, na huyu hivi.
8 Lakini nawaambia wale wasiooa
bado, na wajane, Ni heri wakae
kama mimi nilivyo.
9 Lakini ikiwa hawawezi kujizuia,
na waoe; maana ni afadhali kuoa
kuliko kuwaka tamaa.
10 Lakini wale waliokwisha
kuoana nawaagiza; wala hapo si
mimi, ila Bwana; mke asiachane
na mumewe;
11 lakini, ikiwa ameachana naye,
na akae asiolewe, au apatane na
mumewe; tena mume asimwache
mkewe.
12 Lakini watu wengine
nawaambia mimi, wala si Bwana,
ya kwamba iwapo ndugu mmoja
ana mke asiyeamini, na mke huyo
anakubali kukaa naye asimwache.
13 Na mwanamke, ambaye ana
mume asiyeamini, na mume huyo
anakubali kukaa naye, asimwache
mumewe.
 
Back
Top Bottom