Uchaguzi 2020 Sababu za anguko kubwa la Vyama vya Upinzani 28 Oktoba 2020

Abdalah Abdulrahman

JF-Expert Member
Aug 29, 2019
222
201
1.Kususia uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika 24 Novemba 2019.

Uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika November 2019 ulikua msingi muhimu wa uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 28 Octoba 2020 kwa vyama vya upinzani nchini.Katika uchaguzi huu muhimu, vipo vyama ambavyo vilijitoa katika kinyang'nyiro hiki.Vyama vilivyotangaza kujitoa kushiriki kinyang'nyiro cha uchaguzi huo ni Chadema, UMD, CCK, NCCR-Mageuzi, NLD, ACT-Wazalendo, CUF na Chauma kwa hoja ya kuenguliwa wagombea wa vyama vyao ambao hawakukidhi matakwa ya Tume ya uchaguzi.

Kususia uchaguzi huu kuna athari kuu tatu kwa Vyama vya Upinzani kwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Octoba 2020.

1. Vyama vya upinzani havikupata somo lolote katika uchaguzi wa serikai za mitaa na hivyo kuweza kufanya hayo makosa kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa 28 Octoba 2020

2. Idadi kubwa ya wanachama wa vyama hivi walikata tamaa ya kujiandikisha kwa kuwa na mawazo kuwa yaliyotokea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa (kususia uchaguzi) yatatokea tena kipindi cha uchaguzi mkuu 28 Octoba 2020.

3. Wenyeviti wa serikali za mitaa wanaomchango mkubwa katika kuimarisha vyama na kuweza kuvipatia ushindi kutokana na majukumu yao katika kata.

2. Khofu ya kuwepo mapandikizi ndani ya vyama vya upinzani.
Vyama vya upinzani vimekua vikipokea wanachama wa CCM na kuwapa nyadhifa kubwa za kimaamuzi katika vyama vyao.Viongozi hawa wamekua wakirejea ndani ya CCM wakiwa na siri kubwa za vyama vya upinzani pamoja na kuwaacha mapandikizi ambao hutumika kuvibomoa vyama vya upinzani.Hofu hii inasababisha pia utekelezaji wa majukumu ya vyama kuwa na usiri mkubwa na kutokuaminiana.Jambo ambalo limekuwa likizorotesha shughuli za vyama vya upinzani hasa kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.

3. Aina ya Wafuasi wa vyama vya Upinzani.
Wafuasi wa vyama vya upinzani wamekua wa aina tatu za watu,aina ya kwanza ni ile ya mafisadi na wahujumu uchumi ambao serikali ya awamu ya tano iliwadhibiti,na aina ya pili ya wafuasi ni vijana wahuni wliokuwa wakinufaika na wahalifu wachache ambao serikali ya awamu ya tano imewadhibiti.Aina ya tatu ya wafuasi ni wanaharakati ambao wanatumika na mataifa ya nje kuihujumu Tanzania kwa maslahi yao.

4. Kutokujindikisha kupiga kura.
Ni wazi kuwa vyma vya upinani vilikosa kuwahamasisha wafuasi wao kujiandikisha na kuhakiki taarifa zao kwenye daftari la wapiga kura.Msisitizo mkubwa uliwekwa kwenye suala la Tume huru ya uchaguzi huku viongozi wao wakitamka wazi kutoshiriki uchaguzi bila ya uwepo wa Tume huru ya Uchaguzi.Kwa upande wa CCM wanachama walipewa msisitizo wa kujiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika daftari la waiga kura.

5. Kutokuwa na sera na kuenda na matukio
Vyama vya upinzani vimekua vikiendesha kampeni bila sera maalumu.Hii imepelekea kujikuta wakitaka kuwafurahisha wafuasi wao ambao ni makundi hayo matatu kwa kuwakejeli na kujenga uhasama na vyombo vya ulinzi na usalama-mfano kusema vibaya Polisi,pia wamekuwa wakiwakejeli na kujenga uhasama na vyombo vya habari-mfano TBC waliwaondoa kwenye mkutano wao,kejeli na uhasama kwa wasanii wa kizazi kipya wakiwaita wananjaa.Mambo haya yamekuwa yakikera jamii ya Watanzania ambao wanathamini michango ya vyombo hivi.

6. Tofauti za kimtizamo kati ya Viongozi
Kumekuwepo tofauti za wazi katika vyama viwili vikubwa vya siasa nchini,tofauti hizi ni kati ya Tindu Lissu ambaye ni mgombea Uraisi kupitia Chadema na Freeman Mboe ambae ni mwenyekiti wa Chadema.Msimamo wa Tindu Lissu kutokana na zuio la kufanya kampeni ulikua ni kuendelea na kampeni,lakini Freeman Mboe ambaye ndiye mwenyekiti wa chama akakataa kuendelea na kampeni.Jambo hili limekigawa chama katika makundi mawili,kundi linaloungamkono uamuzi wa Tindu Lissu na lile linalomuunga mkono Freeman Mboe.

Mtafaruku mwingine ni ndani ya ACT-Wazalendo ambao umeibuliwa na Maalim Seif Sharif Hamad mgombea wa AcT-Wazalendo ambapo bila kupitia vikao rasmi alitangaza kumuunga mkono Tindu Lissu kama mgombea Uraisi tofauti na mgombea wa chama chake Bernard Membe.Tofauti hii inatengeneza ufa ndani ya ACT-Wazalendo kwa pande zote mbili za muungano,Zanzibar na Tanzania bara.Hivyo kumpunguzia idadi ya wafuasi Maalim Seif kutokana na usaliti ndani ya Chama.

Kutokana na mambo yaliyoainishwa hapo juu,ni wazi kuwa vyama vya upinzani vinaweza nufaika kwa njia moja tu katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Tarehe 28 Octoba 2020 mbayo ni kujifunza na kufanya maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2025.
 
Sababu kuu ni huyo braza aliyezungushiwa duara.
Screenshot_2020-09-28-13-03-17-1.jpg
 
Sababu zako karibu zote hazina mashiko, kwa mfano kwenye majiji la Dar msitegemee hali ya 2015 na Mbeya ni 50/50 na huku kaskazini labda Kilimanjaro lakini Arusha na Manyara ngoma bichi kwa CHADEMA. Na huko kusini ndio kabisa Wala msijipe matumaini.
 
Kura mpya za JPM zimeongezeka.ACT waliohama Chadema kwa zengwe alafu Zito anawashawishi tena waipe kura Chadema wamegoma kabisa kumtii Zito, hivyo wameamua kumpa kura JPM.
#JPM mitano tena,ushindi ni 95%
 
Kweli Ujinga unazidi kuongezeka kwa kasi kubwa sana.

Mleta andiko Karibu sana Jamii Forum
 
Hahaha uvcc a.k.a JESHI LA AKIBA mliambiwa na Bashiru mjibu hoja, mkija hivi mtakuwa hamlipwi.

October 28, ondoa Pombe, ondoa Makufuli.

Nakumbuka filamu ya SARAFINA aliimba "FREEDOM IS COMING "
 
Hivi NEC wamewapa ccm ushindi wa bure wa mezani wabunge na madiwani tuanzie hapo.
 
1.Kususia uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika 24 Novemba 2019.

Uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika November 2019 ulikua msingi muhimu wa uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 28 Octoba 2020 kwa vyama vya upinzani nchini.Katika uchaguzi huu muhimu, vipo vyama ambavyo vilijitoa katika kinyang'nyiro hiki.Vyama vilivyotangaza kujitoa kushiriki kinyang'nyiro cha uchaguzi huo ni Chadema, UMD, CCK, NCCR-Mageuzi, NLD, ACT-Wazalendo, CUF na Chauma kwa hoja ya kuenguliwa wagombea wa vyama vyao ambao hawakukidhi matakwa ya Tume ya uchaguzi.

Kususia uchaguzi huu kuna athari kuu tatu kwa Vyama vya Upinzani kwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Octoba 2020.

1. Vyama vya upinzani havikupata somo lolote katika uchaguzi wa serikai za mitaa na hivyo kuweza kufanya hayo makosa kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa 28 Octoba 2020

2. Idadi kubwa ya wanachama wa vyama hivi walikata tamaa ya kujiandikisha kwa kuwa na mawazo kuwa yaliyotokea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa (kususia uchaguzi) yatatokea tena kipindi cha uchaguzi mkuu 28 Octoba 2020.

3. Wenyeviti wa serikali za mitaa wanaomchango mkubwa katika kuimarisha vyama na kuweza kuvipatia ushindi kutokana na majukumu yao katika kata.

2. Khofu ya kuwepo mapandikizi ndani ya vyama vya upinzani.
Vyama vya upinzani vimekua vikipokea wanachama wa CCM na kuwapa nyadhifa kubwa za kimaamuzi katika vyama vyao.Viongozi hawa wamekua wakirejea ndani ya CCM wakiwa na siri kubwa za vyama vya upinzani pamoja na kuwaacha mapandikizi ambao hutumika kuvibomoa vyama vya upinzani.Hofu hii inasababisha pia utekelezaji wa majukumu ya vyama kuwa na usiri mkubwa na kutokuaminiana.Jambo ambalo limekuwa likizorotesha shughuli za vyama vya upinzani hasa kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.

3. Aina ya Wafuasi wa vyama vya Upinzani.
Wafuasi wa vyama vya upinzani wamekua wa aina tatu za watu,aina ya kwanza ni ile ya mafisadi na wahujumu uchumi ambao serikali ya awamu ya tano iliwadhibiti,na aina ya pili ya wafuasi ni vijana wahuni wliokuwa wakinufaika na wahalifu wachache ambao serikali ya awamu ya tano imewadhibiti.Aina ya tatu ya wafuasi ni wanaharakati ambao wanatumika na mataifa ya nje kuihujumu Tanzania kwa maslahi yao.

4. Kutokujindikisha kupiga kura.
Ni wazi kuwa vyma vya upinani vilikosa kuwahamasisha wafuasi wao kujiandikisha na kuhakiki taarifa zao kwenye daftari la wapiga kura.Msisitizo mkubwa uliwekwa kwenye suala la Tume huru ya uchaguzi huku viongozi wao wakitamka wazi kutoshiriki uchaguzi bila ya uwepo wa Tume huru ya Uchaguzi.Kwa upande wa CCM wanachama walipewa msisitizo wa kujiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika daftari la waiga kura.

5. Kutokuwa na sera na kuenda na matukio
Vyama vya upinzani vimekua vikiendesha kampeni bila sera maalumu.Hii imepelekea kujikuta wakitaka kuwafurahisha wafuasi wao ambao ni makundi hayo matatu kwa kuwakejeli na kujenga uhasama na vyombo vya ulinzi na usalama-mfano kusema vibaya Polisi,pia wamekuwa wakiwakejeli na kujenga uhasama na vyombo vya habari-mfano TBC waliwaondoa kwenye mkutano wao,kejeli na uhasama kwa wasanii wa kizazi kipya wakiwaita wananjaa.Mambo haya yamekuwa yakikera jamii ya Watanzania ambao wanathamini michango ya vyombo hivi.

6. Tofauti za kimtizamo kati ya Viongozi
Kumekuwepo tofauti za wazi katika vyama viwili vikubwa vya siasa nchini,tofauti hizi ni kati ya Tindu Lissu ambaye ni mgombea Uraisi kupitia Chadema na Freeman Mboe ambae ni mwenyekiti wa Chadema.Msimamo wa Tindu Lissu kutokana na zuio la kufanya kampeni ulikua ni kuendelea na kampeni,lakini Freeman Mboe ambaye ndiye mwenyekiti wa chama akakataa kuendelea na kampeni.Jambo hili limekigawa chama katika makundi mawili,kundi linaloungamkono uamuzi wa Tindu Lissu na lile linalomuunga mkono Freeman Mboe.

Mtafaruku mwingine ni ndani ya ACT-Wazalendo ambao umeibuliwa na Maalim Seif Sharif Hamad mgombea wa AcT-Wazalendo ambapo bila kupitia vikao rasmi alitangaza kumuunga mkono Tindu Lissu kama mgombea Uraisi tofauti na mgombea wa chama chake Bernard Membe.Tofauti hii inatengeneza ufa ndani ya ACT-Wazalendo kwa pande zote mbili za muungano,Zanzibar na Tanzania bara.Hivyo kumpunguzia idadi ya wafuasi Maalim Seif kutokana na usaliti ndani ya Chama.

Kutokana na mambo yaliyoainishwa hapo juu,ni wazi kuwa vyama vya upinzani vinaweza nufaika kwa njia moja tu katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Tarehe 28 Octoba 2020 mbayo ni kujifunza na kufanya maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2025.
Rudi ufanye utafiti tena, wapinzani hawakufanya siasa miaka 5, baadhi yao wameshughurikiwa na dola, kukosekana uwanja sawa kwenye zoezi la uchaguzi nk
 
Back
Top Bottom