Sababu ya kusema neno ‘Hellow’ kwenye simu kabla ya maongezi

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Habari zenu wakuu humu ndani natumai nyie ni wazima wa afya kabisa.

Leo nitashare nanyi hiki:

Hivi ushawahi kujiuliza kwa nini ukiwa unaongea na simu iwe umepiga au kupigiwa, kabla ya maongezi Neno la kwanza kuongea ni Hellow?

Leo nakujuza sababu, wengine watasema Neno hilo humaanisha Habari (Hello). Hapana si hivyo neno hellow lilianza kutumiwa na Mgunduzi wa Simu Alexandra Grahim Bell.

Bell alikuwa na Mapenzi ya dhati sana yaani alikuwa amependa kweli kweli (kama ninavyo penda mimi🤣), hivyo hadi kilifikia kipindi mpenzi wake akamkimbia. Baada ya Bell kuunda simu alifanikiwa kumpigia mkewake huyo aliye mkimbia.

Baada ya mke kupokea, Bell aliamua kumuita kwanza kwa Jina lake huyo mke kwa jina la Hellow ili mke aweze kumsikiliza kwa uzuri.

Mke wa Bell alikuwa akijulikana kwa jina la Mabel Margeret Hellow.

Hiyo ndio sababu ambayo watu wengi wakitaka kuongea na simu huanza kwa kusema Hellow.
 
Kwahiyo alitengeneza simu mbili, moja ya kwake nyingine akampelekea mkewe, alafu ndo akampigia ? Au hio ni baada ya simu kuanza kuenea ?
Baada ya simu kuenea na yeye kupata access ya mawasiliano yake
 
Baada ya simu kuenea na yeye kupata access ya mawasiliano yake
Kwahiyo before ya kupata hiyo access ya mawasiliano, hao watu wengine alikuwa anawasalimiaje, hapa ndipo tunapojua kuwa bongo ni kisiwa cha fix sana

Hellow is a form of greeting used by a hyper-active person in The Netherlands.

Pia unaweza search na kujua maana yake na siyo hiyo wewe unayojaribu kusema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom