Sababu mbili kubwa za Mkutano mkuu kuwarejesha Mbowe na Dr Slaa uchaguzi wa ndani 2014

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Wiki mbili zijazo Chadema itaanza mchakato wa uchaguzi wa ngazi ya kitaifa ambao utahusisha mabaraza na chama chenyewe. Kwenye uchaguzi huu, wengi wetu tunaungana na wazee wa kigoma waliomchukulia fomu Mbowe na tunadhani kuwa Freeman Mbowe na Dr Slaa wanatakiwa warejee kwenye nafasi zao. Kwa maoni yangu, wadau wengi wanawaunga mkono viongozi hao kutokana sababu kubwa mbili. Nitazijadili nikianza na sababu ya kwanza.

Mwaka 2005 Freeman Mbowe alinadi ilani ya Chadema iliyobainisha kuwa Chadema itabadilisha mji wa Dodoma kuwa mji wa Vyuo vikuu. Baada ya kikwete kushinda akachukua fedha kwenye mifuko ya kijamii ya PSPF na NSSF na kuanzisha chap chap chuo kiuu cha UDOM. Matatizo ya kudandia hoja hiyo ni kuwa mpaka leo CAG analalamika kuwa mifuko hiyo ina hali mbaya kifedha pesa za mifuko zilizokowa hazijarejeshwa.

Mmwaka 2010 Dr Slaa alinadi ilani ya Chadema iliyosema Chadema itatoa elimu bure kuanzia kidato cha kwanza hadi sita. Jana Rais Kikwete akiwa mjini Morogoro ametangaza kuwa Serikali inaangalia uwezekano wa kuondoa ada mpaka kidato cha nne. Amesahau kuwa 2010 walimtukana Dr Slaa 2010 kuwa anapiga porojo zisizowezekana.kwa bahati mbaya sana imewachukua ccm miaka 4 kujua kuwa alichonadi Dr Slaa kinafaa.

Mwaka 2005 freeman Mbowe aliasisi matumizi ya helikopta kwenye kampeni za kusaka urais. CCM ilitumia nguvu nyingi sana kushambulia matumizi ya helikopta kwa hoja dhaifu ya gharama. Mwaka 2010 chadema iliendelea kutumia helikopta na CCM wao wakatumia helikopta 2 na wakati mweingine 3. Iliwachukua ccm miaka 5 kugundua kuwa msururu wa magari 20 kwenye kampeni zao ni ghali kuliko helikopta mmoja ya Mbowe. CCM hawajawahi kumshukuru Mbowe na Ubunifu wake bali waliuchukua tu ubunifu huo kimya kimya na kwa aibu 2010.

Mwaka 2010, Dr Slaa alinadi sera ya chadema ya kuwapa watanzania afya ya Bure - yaani matiabu yawe ya bure kama enzi za mwanzo za mwalimu Nyerere kwa watanzania wote. Sasa hivi serikali inasema watoto chini miaka 5 na wazee matibabu yao ni bure. Hata hivyo, hospitalini hali haiko hivyo, kwa wazee na watoto. Matatizo ya kuiga ni kufanya jambo hilo hovyo hovyo.Hata hivyo, tunawashukuru kwa kutambua kuwa sera ya Chadema inatekelezeka na inawezekana.

mwaka 2010 Dr Slaa alisema Chadema wakiingia madarakani gharama ya vifaa vya ujenzi kama sementi, mabati nk vitashuka kwa zaidi ya 50% ya gharama ya sasa (ya wakati huo 2010) kwa kuondoa kodi ili wananchi maskini waweze kujenga nyumba zao.

mpaka sasa serikali iko kimya kuhusu hili pengine hili litawachukua zaidi ya miaka 5 au zaidi ili kuielelewa. Nadhani tunahitaji kuwaombea Mungu awafanulie.

Mwaka 2010 Dr Slaa alinadi ilani ya Chadema kuwa Chadema tukiingia madarakani tutaanzisha mchakato wa katiba mpya ndani ya miezi 3. Baada ya JK kuingia madarakani kiaina alidandia hoja hiyo na kuanzisha mchakato huo bila ridhaa ya ccm na bila kujali kuwa haukuwepo kwenye ilani ya ccm, matokeo yake tunayaona sasa.

Mwaka 2014 Freeman Mbowe alimshirikisha Prof Lipumba na wakakubaliana kuibuka na UKAWA. Leo hii ushirikiano huu wa Chadema, CUF na NCCR (UKAWA) ambao Mbowe ni moja wa mwasisi mkuu ndo mjadala wa kitaifa kiasi kwamba jana Rais kikwete amewaita IKULU baada ya kugundua kuwa bila UKAWA hakuna KATIBA MPYA.

Lazima tukubaliane kuwa bila ubunifu huu wa Mbowe leo hii katiba ingeandikwa na wangerejesha serikali mbili Kinyume na maoni ya wananchi yalikusanywa na tume ya Warioba bila kash kashi yo yote.

Kwa hiyo, basi, sababu ya kwanza ni kuiendesha serikali kutoka nje na ndo maana sishawishiki kuwabadilisha viongozi hawa wanaoiendesha serikali kutoka nje. Kwa maoni yangu, viongozi wote wawili Dr Slaa na Mbowe wabaki kwenye nafasi zao.

Haya ni maoni yangu na ninaamini ndo msimamo wa wanachadema walio wengi. Hapa sijagusia sababu ya pili ambayo ni mafanikio yao kwenye kuijenga Chadema mpaka ikasambaa nchi nzima kwenye ngazi ya mabalozi wa nyumba kumi /nyumba tano. Hiyo ni makala mengine na ni sababu ya pili ya kwa nini ninawaunga mkona viongozi hawa wabakie kwenye nafasi zao.

Nawasilisha.
MIKAEL AWEDA.
 
Utawaondoa wamiliki wa saccos uweke wapangaji? Mbowe ndio chadema chumbani nyie wengine wa sebuleni endeleeni kumpigia makofi
 
Acheni demokrasia ichukue mkondo wake,msiwatishe wanaCHADEMA watakaotaka kuziwania nafasi za Uenyekiti na Ukatibu Mkuu,Kama viongozi wa sasa wanakubalika na wanaCHADEMA wengi watarudishwa tu madarakani.
 
Wewe utakuwa mwanaCHADEMA lakini huifahamu CHADEMA katika mazingira ya jana na leo!.

Hao unaodai warudishwe lazima ufahamu kuwa hawahitaji kurudishwa kwa sasa kama fikra zako zinavyodhani kwa sababu wameishajirudisha wenyewe.

Mh. Mbowe na Dkt. Slaa kwa sasa wameishajenga mazingira ambayo hayahitaji hata kupigiwa kura ili kurudi katika nafasi zao za uongozi.

Mh. Mbowe na Dkt. Slaa wameishawafukuza na wanaendelea kuwafukuza wanachama wale ambao andiko lako ndiyo lilitakiwa liwaombe wawarudishe kina Mbowe na Dkt. Slaa katika nafasi zao.

Kwani hufahamu sababu iliyopelekea uchaguzi wa ndani wa CHADEMA Taifa kupigwa tarehe mara tatu ili waendelee kujenga mazingira ya kujirudisha wenyewe katika uongozi.

Kama unafahamu sababu zake, basi wewe utakuwa umetumwa pia kujenga mazingira ili ionekane kama kuna uwanja ulio sawa katika chaguzi za nafasi ya kitaifa ndani ya CHADEMA.

Kila siku ninasema, CHADEMA kimejengwa katika misingi ya kilaghai.
 
Pia uzingatie na vichwa vya habari vilivyotawala baada ya kufukuza Zitto.
-Ngumizapigwa chadema mbeya
-Katibu wa Chadema Tanga ahoji
-Katibu wa Chadema Dar mbaroni
-Chadema Ruvuma kimenuka
-Chadema vyuo vikuu watoa angalizo wakemea ubabe wa
viongozi
-Chadema kigoma wachoma bendera
-Said Arfi ajiuzulu
-Profesa Beregu siungi mkono maamuzi ya juu ya Zitto
kuvuliwa uongozi
-Chadema Geita watoa tamko
-Dr. Slaa marufuku kukanyaga kigoma
-Mwenyeki wa Chadema mkoa wa Lindi ajiuzuru
-Vijana wa vyuo vikuu Morogoro 60 waikacha Chadema
-Zitto akatisha ziara ya Dr.Slaa kigoma
-Mwenekiti wa Chadema mkoa Singida ajiuzuru
-Ofisi ya Chadema mkoa Arusha yachomwa moto
-Chadema kina ubinafsi na Zitto kaonewa
-Chadema mkoa wa mwanza sababu za kuvua uongozi Zitto
hazikubaliki.
-Chadema Arusha wasusia kikao cha upatanishi
-POLISI:Chadema inahusika na moto Arusha
-Wana chadema UDOM warudisha kadi za chama
-Mkutano wa chedema Kasulu vurugu
-Mabomu yapigwa mkutano wa chadema
-Polisi yatahadharisha Dr. akatishe ziara kigoma
-Mikutano ya Dr. Slaa yadoda kigoma
 
Wewe kama kibaraka wao mkuu lazima uandike haya uliyoandika

Uteuzi wa kibaraka mkuu wa Mbowe na Dr Slaa unafanywa kamati ipi wapi na lini? Hata hivyo, ni heshima kuwa kibaraka wa Mbowe na Dr Slaa kuliko kuwa kibaraka wa ccm wanaofilishi nchi yetu kwa ufisadi. Bado hujanitukana mkuu.
 
Uteuzi wa kibaraka mkuu wa Mbowe na Dr Slaa unafanywa kamati ipi wapi na lini? Hata hivyo, ni heshima kuwa kibaraka wa Mbowe na Dr Slaa kuliko kuwa kibaraka wa ccm wanaofilishi nchi yetu kwa ufisadi. Bado hujanitukana mkuu.
Mkuu, umesahau kuwa hata mwenyekiti wako huwa anaenda kufanya uzinifu huko Dubai na fedha za walipa kodi. Huo si ufisadi?
 
pia uzingatie na vichwa vya habari vilivyotawala baada ya kufukuza zitto.
-ngumizapigwa chadema mbeya
-katibu wa chadema tanga ahoji
-katibu wa chadema dar mbaroni
-chadema ruvuma kimenuka
-chadema vyuo vikuu watoa angalizo wakemea ubabe wa
viongozi
-chadema kigoma wachoma bendera
-said arfi ajiuzulu
-profesa beregu siungi mkono maamuzi ya juu ya zitto
kuvuliwa uongozi
-chadema geita watoa tamko
-dr. Slaa marufuku kukanyaga kigoma
-mwenyeki wa chadema mkoa wa lindi ajiuzuru
-vijana wa vyuo vikuu morogoro 60 waikacha chadema
-zitto akatisha ziara ya dr.slaa kigoma
-mwenekiti wa chadema mkoa singida ajiuzuru
-ofisi ya chadema mkoa arusha yachomwa moto
-chadema kina ubinafsi na zitto kaonewa
-chadema mkoa wa mwanza sababu za kuvua uongozi zitto
hazikubaliki.
-chadema arusha wasusia kikao cha upatanishi
-polisi:chadema inahusika na moto arusha
-wana chadema udom warudisha kadi za chama
-mkutano wa chedema kasulu vurugu
-mabomu yapigwa mkutano wa chadema
-polisi yatahadharisha dr. Akatishe ziara kigoma
-mikutano ya dr. Slaa yadoda kigoma

bila kujua umejikuta ukiandika jinsi cdm ilivyosambaa nchi nzima , kwa taarifa yako mbowe na dr slaa ndio wamefanya kazi hiyo .
 
Viongozi wa CDM watachaguliwa na wanaCDM, wengine ni ushabiki wa mechi isiyowahusu na wanatakiwa kutambua mipaka ya majukumu yao. Pia hawazuiliwi kama wametambua kuwa CDM ndio itatoa mwanaMAGOGONI na hivyo wanajaribu kuangalia ni nani anawafaa kwa upande wao, ila hii haiwalazimu wanaCDM kuwasililiza walitakalo kwani bado ni wafurukutwa na washabiki ndani ya CDM. Wakereketwa songeni mbele
 
Pia uzingatie na vichwa vya habari vilivyotawala baada ya kufukuza Zitto.
-Ngumizapigwa chadema mbeya
-Katibu wa Chadema Tanga ahoji
-Katibu wa Chadema Dar mbaroni
-Chadema Ruvuma kimenuka
-Chadema vyuo vikuu watoa angalizo wakemea ubabe wa
viongozi
-Chadema kigoma wachoma bendera
-Said Arfi ajiuzulu
-Profesa Beregu siungi mkono maamuzi ya juu ya Zitto
kuvuliwa uongozi
-Chadema Geita watoa tamko
-Dr. Slaa marufuku kukanyaga kigoma
-Mwenyeki wa Chadema mkoa wa Lindi ajiuzuru
-Vijana wa vyuo vikuu Morogoro 60 waikacha Chadema
-Zitto akatisha ziara ya Dr.Slaa kigoma
-Mwenekiti wa Chadema mkoa Singida ajiuzuru
-Ofisi ya Chadema mkoa Arusha yachomwa moto
-Chadema kina ubinafsi na Zitto kaonewa
-Chadema mkoa wa mwanza sababu za kuvua uongozi Zitto
hazikubaliki.
-Chadema Arusha wasusia kikao cha upatanishi
-POLISI:Chadema inahusika na moto Arusha
-Wana chadema UDOM warudisha kadi za chama
-Mkutano wa chedema Kasulu vurugu
-Mabomu yapigwa mkutano wa chadema
-Polisi yatahadharisha Dr. akatishe ziara kigoma
-Mikutano ya Dr. Slaa yadoda kigoma

kwa kila kichwa cha habari naomba utuandike jina la gazeti na mmiliki wake. Na tuambie kama ni gazeti la ccm au la mwanaccm. Ukishamaliza nitakujibu.
 
Back
Top Bottom