Sababu kuu ya ajali za barabarani Tanzania ni hii hapa!!!

Sababu nyingine ambayo inauma sana ni hawa Traffic wanaojificha na tochi, nimeshuhudia ajali moja maeneo ya Kibaha Maili moja na nyingine Korogwe- I think ni kwasunga, eti hawa jamaa wamejificha porini na ukishotkeza na spidi zako nao wanajitokeza ghafla, wanakupiga tochi....ukifunga breki ghafla waweza toka nje ya road
 
Uko juu Mr. Rocky.

Enzi hizo nafanya kazi Iringa weekend naenda kunywa beer Dar. yaani wacha mchezo. Ndio tulikua tunaendesha spidi zote zikiisha tunakopa. ha ha ha ha ha.

Namshukuru Mungu tu nipo salama kwa sasa. ila ujana maji ya moto meeen.

Mkuu Mlachake ujana mzuri sana na shukuru uliutumia ujana vyema mkuu kwa sasa unakula matunda ya kutumika kwako na hukupata kilema kwa kupita barabara kama hizo
Mpaka sasa bado napita baadhi ya barabara mkuu tena za mbali kama ya kwenda lindi mpaka mtwara au ya kwenda serengeti au ya kwenda mwanza kwa kupitia sekenke au kwenda kigoma kupitia kahama- bukombe-runzewe- nyakanazi au kupitia busisi- sengerema-geita- chato- runzewe mpaka nyakanazi na unaunganisha kasulu mpaka kigoma
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli unayosema, kufanya safari ya masafa inatakiwa uwe na uzoefu wa kutosha.Kwanza hata macho kuangalia lami muda wa masaa matatu au manne huwainafikia yanachoka na hatimaye kupelekea usingizi wa ina flani ambao unaweza ukapelekea gari kutoka nje ya barabara.

Mkuu,

Mbaya zaidi ni kwamba ana overtake kwenye kona bila kujua mbele kuna gari au hamna. Halafu ni gari lililobeba abiria!!!!!

Tiba
 
Mkuu ahsante kwa ushauri ila mie kwenye highway hasa nyakati za usiku siendeshi gari zaidi ya 70 ph
 
Duh! na wewe jiografia kabisa, sekeke ukitokea sherui unapandisha, hapo wanashuka sasa itakuwaje sekenke?anayesema kitonga inaweza kuwa sawa, ila hiyo barabara ni ya lami, kitonga siku hizi kuna zege... hi
jamani nikiangalia kwa makini naona kama ni pale daraja mbili maeneo ya iyovi.
 
Ni kweli, madereva wazembe wanachangia ajali barabarani. Pamoja na hayo, akini ningependa kutoa mtazamo tofauti juu ya janga hili linalopelekea maisha ya watz kupotea kila kukicha na huku tukiishia ku-play the blame game. Binafsi nasema wazi kwamba serikali ndio chanzo cha ajali barabarani. Serikali yetu ndio inayoruhusu magari mabovu yatumie barabara zetu. Serikali yetu ndiyo inayoruhusu madereva wazembe waendeshe magari yenye taa moja, kuvutana kwa kamba, nk. Serikali yetu hiyo hiyo ndio imekuwa kinara wa kutujengea barabara nyembamba mithili ya models na kuacha mashimo (drainages) pembezoni mwa barabara! Tizama hata viwango vya barabara zetu ambazo tayari zimeshajengwa, na zinazoendelea kujengwa ni vya chini sana...barabara zimejaa kona kila mahala...istoshe barabara ni nyembamba kiasi kwamba kupishana na gari in opposite direction inakuwa shughuli...mbaya zaidi; kitendo chenyewe cha kupishana na gari ana kwa ana nayo ni kichocheo tosha cha ajali. Nafikiri imefika wakati serikali yetu nayo ijipange katika kusaidia hili eneo hili korofi kama kweli kuna nia ya dhati...mfano hai ni ujenzi wa barabara ya Morogoro eneo la Kimara mwisho. Serikali yetu chini ya Mh. Pombe inajifanya haioni kama kuna ajali inanukia eneo hilo. Ukipita jioni Kimara mwisho is just an accident about to happen.. God forbid, lakini siku ikitokea, watu wengi watapoteza maisha. Darajani Kimara mwisho, utakuta malori mabovu ndio chanzo kikuu cha foleni. Mbaya zaidi hayo malori yanatoka kote huko na yanakuja kuharibikia Kimara mwisho. Jioni hiyo hiyo, hapo darajani hakuna askari wa Usalama barabarani anayesaidi kuratibu msururu wa magari (askari utamkuta kwenye kituo cha daladala!). Istoshe, kandarasi aliyepewa jukumu la kujenga barabara ameshindwa kupitisha greda kwenye barabara mbadala ili kupunguza jam, na uwezekano wa ajali... Tanzania hii, sijui tunaelekea wapi
 
Ni kweli sehemu kubwa ya lawama za ajali barabarani inabebwa na serikali. Kwa mtazamo wangu serikali haijaweka dhamira na due deligence katika janga hili. Pamoja na kelele nyingi za lawama latika majukwaa yote unayoyafahamu, bado hajaweka mkakati kazi wa kuliondoa tatizo. Askari wa usalama barabarani, kama chombo husika, wanabeba lawama hii kwa niaba ya serikali. Vitendea kazi vya kisasa wanavyo, nguvu kazi ipo ila commitment haipo. Kimekuwa chombo cha kutengeneza mazingira ya ulaji tu. Hebu tuangalie mfano mdogo:
barabara ya Morogoro - kuanzia Ubungo hadi Chalinze haihitaji zaidi askari 9 kuli-monitor. Sehemu korofi zinajulikana na wakijipanga kisayansi na kusimamia sheria ipasavyo, ajali zitabakia kuwa ajali na siyo uzembe wa dereva wala ubovu wa gari.
Kwa Tanzania yetu ya leo, hayo ni maamuzi magumu, ikizingatiwa kwamba hakuna political will, kuogopana na wakati mwingine kwa watendaji "on the ground" wanapofanya kazi zao ipasavyo, wakubwa wanawaangusha kwa kuwapuuza. This particular topic is so far reaching in that we require a very strong willed government to at least try.
 
View attachment 72660
Duh huyu dereva ana hatari sana,una overtake mlimani afu na nissan diesel kwa scania
this is more than danger

Mkuu, hii Picha Me Imenisisimua Sana, i Met Similar Situation Ruaha Mbuyuni Nikiwa Naenda Kwenye Mahafari Ya Mdogo Wangu Pale Tumaini Iringa. its frighten For The Incomin car. Nililazimika Kutoka Nje Ya Barabara Miguu Yote. Namshukuru Mungu Tulienda Na Kurudi Salama. Natakiwa kwenda Mbeya this Christmas. Naomba Mungu Anitangulie Maana Hii Trend Sio Nzuri Kbs.
 
Mkuu, hii Picha Me Imenisisimua Sana, i Met Similar Situation Ruaha Mbuyuni Nikiwa Naenda Kwenye Mahafari Ya Mdogo Wangu Pale Tumaini Iringa. its frighten For The Incomin car. Nililazimika Kutoka Nje Ya Barabara Miguu Yote. Namshukuru Mungu Tulienda Na Kurudi Salama. Natakiwa kwenda Mbeya this Christmas. Naomba Mungu Anitangulie Maana Hii Trend Sio Nzuri Kbs.

Hawa madereva wa mabasi ya mikoani pia ni chanzo kikubwa sana cha ajari,kitendo cha magari madogo kuwaogopa inawapa advantage ya kuvunja sheria barabarani,huwa sitamani kabisa kukaa seat za mbele kwenye mabus ya mikoani maana utakavyovishudia mpaka unafika ni kumshukuru Mungu.They are very rough and speed,wanaovertake kiholela without even taking a good look mbele kuna nini,Mkuu ukienda Mbeya inabidi uwe an extra careful maana madereva wa huko pia bangi tupu.
 
Sababu kubwa ni hii mi trafiki mi juzi mida ya să kumi jioni hapo kibaha aliniată wamejificha nikashtukiA huyo na jitumbo lake na kamera nikamkosa kumgonga mana nilishtuka sana nilizani ni mnyama anavuka nilivyosimama nikamchezeshea mbata kadhaa then nikasepa zangu arusha....
Sababu nyingine ambayo inauma sana ni hawa Traffic wanaojificha na tochi, nimeshuhudia ajali moja maeneo ya Kibaha Maili moja na nyingine Korogwe- I think ni kwasunga, eti hawa jamaa wamejificha porini na ukishotkeza na spidi zako nao wanajitokeza ghafla, wanakupiga tochi....ukifunga breki ghafla waweza toka nje ya road
 
pamoja na uzembe wa madereva kuchangia katika asilimia kubwa sana ya ajali za magari barabarani,na kusababisha vifo vya maelfu ya raia wasio na hatia yoyote sasa tunakuletea sababu moja wapo ya msingi ya kukithiri kwa ajali siku za hivi karibuni:
View attachment 72655
madereva wengi sana wanaojifunza gari mijini(dar-arusha-tanga)wakishapata lessen tu,huwa na mzuka wa kukata masafa marefu na gari zao au za kuazima,kimatembezi,au kwa shida nyengine yoyote ile!!bila kuweka katika akili zao kuwa barabara zote zinazokwenda mikoani huwa zinamisukosuko ya aina mbali mbali!!
1:inahitaji uwe mzoefu wa hali ya juu katika ku overtake
2:inatakiwa ujuwe sehemu za ku overtake au kuto overtake ili kujiepusha na ajali
3:uwe na uvumilivu wa kukwepa makosa ya madereva wengine,ili kujiepushia ajali
4:masafa ya km200-1200km si sawa na 20km au 15 km,safari ndefu zinataka angalau ukae kushoto hata mara mbili
View attachment 72658
barabara zetu za mikoani zina changamoto mbali mbali unapoendesha gari majira ya usiku huwezi kuyaepuka kama wewe si dereva mzoefu wa njia hizo!!!
1:kuna gari nyingi usiku huwa zinatembea na taa moja tu,unaweza ukadhani pikipiki ukiibana imekula kwako!
2:kuna matreckta yanavuta matela nyakati za usiku bila kuwa na ishara yoyote,na ajali nyingi hutokea hapo!!
3:kuna madereva wanaowasha taa zenye mwanga mkali bila kuzizima,hivyo kukusababishia kupata ajali!
View attachment 72660
ninachopenda kuwaeleza madereva wa mjini muliokuwa hamuna idea na barabara za mikoani,kabla ya kuchukua maamuzi ya kuhatarisha maisha yako au ya familia yako,unapotaka kukata masafa marefu ya mikoani hali ya kuwa huna idea ya marabara za huku,ajiri dereva akuendeshe angalau tripu mbili au tatu,upate uzoefu,na muchangie katika kutupunguzia ajali,ambazo sisi wakazi wa mikoani tunaona madereva wengi wanaotusababishia ajali nyingi hutokana na kutokuwa wazoefu wa njia zetu!!!!!!

sababu uliyotoa ni udereva ule ule
 
Mkuu, hii Picha Me Imenisisimua Sana, i Met Similar Situation Ruaha Mbuyuni Nikiwa Naenda Kwenye Mahafari Ya Mdogo Wangu Pale Tumaini Iringa. its frighten For The Incomin car. Nililazimika Kutoka Nje Ya Barabara Miguu Yote. Namshukuru Mungu Tulienda Na Kurudi Salama. Natakiwa kwenda Mbeya this Christmas. Naomba Mungu Anitangulie Maana Hii Trend Sio Nzuri Kbs.

kaka hata ukiwa right kwenye side(saiti) yako. kwenye hii njia Just drive as if you are on the wrong side of the road. meaning that at any time kuna gari itakuja mbele yako wewe upande huo unaondeshea. Iyovi sio mchezo
 
Kwakuchangia na mimi nikua nawashauri madereva wenzangu pia hakuna ulazima wa kuendesha gari usiku na mvua inanyesha halafu unasafiri safari ndefu! Kwakweli sintakaa nisahau yaliyonikuta niliendesha gari tokea Holili kuja Arusha milango ya saa 4 za usiku na mvua inanyesha tena kubwa nilichojionea ni Mungu na siri yangu mwenyewe! ni bora ukapaki gari uchukue Guest au kama huna hela ya chumba lala kwenye gari.
 
Kuna baadhi ya michezo huwa inafanyika barabarani hatari tupu
Hapa ajari zitaisha kweli...
images
 
Halafu naomba kuuliza swali! Ni kwanini inapotokea ajali kubwa unapomkuta marehemu ndani ya gari akiwa nyang'anyang'a mara nyingi unamkuta hana nguo yuko na boxsa tu?
 
Na saa nyingine usiku mtu anakuwa nyuma yako amepiga full light na wa mbele mnayepishana the same!Huwa ni shida tupu!Na pia mtu unatakiwa ujue kukadiria spidi ya gari unaloovertake na hata ukubwa wake na mazingira ya barabara.Kuna siku nilishuhudia basi sa superfeo na lori la mafuta maeneo ya Iyovi kuelekea Iringa kwani jamaa wa basi aliamua kuover take ktk kona wakati lori lilikuwa spidi na dereva wa lori hakupunguza mwendo kumpisha yule wa basi,nilikuwa nyuma yao na gari dogo nilichokifanya ni kupunguza mwendo ili hata wa basi akirudi ghafla asiniue na familia.Ila nilijiuliza sana kama kule mbele pangetokea gari jingine ktk hiyo kona yule wa superfeo si angechinja watu wengi tu au hata kuacha wengi wao vilema!
Na unatakiwa pia kwenda speed unayoweza kouna incase of anything utamudu gari lako.
 
Sheria legelege za barabarani zinachangia pia

Vitendea kazi duni kwa wanausalama wa barabarani

Madereva hawapati nafasi za kupumzika hasa wale wa masafa marefu. Dereva wa lori anakesha kulinda mali isivunjwe na kuibiwa alafu asubuhi ananza safari tena ya maili 250 au zaidi alafu hapo tutaepusha ajari kweli

Utumiaji wa madawa ya kulevya na pombe nyakati za safari. Hili hufanywa na madereva wengi wa gari ndogo,malori,na hata mabasi. Mtu anaendesha gari ya familia kwasababu mama au baba hayupo anawasha bangi na masela wake siti ya nyuma wanafungua mzinga wa KUNYWA ONGEZA NGUVU YAKO MWILINI ANGALIA GONGO INAUA(KONYAGI) wakati huo wanaenda MBEYA na ndiyo kwanza wako CHALINZE. KITAKACHO FUATA HAPO WADAU MNAJUA

MOTHER NATURE NAYO IPO KATIKA KUTUMALIZA. Hali ya hewa pia kwa wasio wazoefu wa mahali fulani. Hasa nyanda za juu kusini nyakati za ukungu ni hatari pia wana. Mfano kuna sehemu pale Wilaya ya Rungwe ilipewa jina UWANJA WA NDEGE karibu sana na maeneo ya IGOGWE miaka ya themanini hadi tisini palikua pabaya sana kulikua na mabaki ya magari tu yako bondeni futi kama 120 kwa makadilio.

UFINYU WA BARABARA ZETU PIA UNATUMALIZA
 
Back
Top Bottom