Sababu hamsini za Lowassa kuwa mgombea wa CCM 2015

Sababu hamsini za Lowassa kuwa mgombea wa CCM 2015

UFISADI WA LOWASSA HUU HAPA:1. Kununua jumba la kifahari London, Uingereza, lenye thamani ya zaidi shilingi bilioni 1 za Tanzania.Metropolitan police wa Uingereza wanachunguza suala hili. Wamewasiliana na anti-money laundering unit ya Tanzania kuchunguza suala hili.2. Ufisadi wa Nyumba ya SanaaLowassa amehisika kufanya uporaji wa ardhi ya Nyumba ya Sanaa iliyopo karibu na Movenpik Hotel (zamani Serena Hotel). Nyaraka zinaonesha yeye ni mmiliki wa kampuni inayojenga gorofa kubwa kwenye eneo hilo la Nyumba ya Sanaa.3. Utajiri usioelezeka (unexplained wealth)Akiwa kama kiongozi wa umma, Lowassa amejilimbikizia mali nyingi sana za thamani ya mabilioni ya shilingi. Mali alizo nazo haziendani na kipato chake kama kiongozi wa umma. Sheria ya kupambana na rushwa Tanzania iko wazi kuwa kiongozi wowote wa umma mwenye utajiri usioendana na mapato yake halali anastahili kufikishwa mahakamani. Kutokana na sera za kulindana na kuogopana, Lowassa, Andrew Chenge, na viongozi wengine wa umma hawajafikishwa mahakamani kwa kosa hili na PCCB. Pia kwenye fomu za kila mwaka za kutaja mali, Lowassa haja declare assets zake zote. Ana miliki Alphatel, Alpha Schools, Alpha House, apartment blocks Dar es Salaam, Arusha na nje ya nchi.4. Land grabbingAlipokuwa Waziri wa Ardhi enzi za utawala wa Mwinyi alihusika na uporaji mkubwa wa ardhi sehemu mbali mbali nchini.5. RichmondLowassa ndiye aliyeagiza TANESCO waporwe madaraka ya kusimamia tenda ya umeme kinyume na sheria ya manunuzi, PPRA. Aliunda kamati ya makatibu wakuu na kusimamia kwa karibu majadiliano ya kamati hii na nRichmond na kuagiza wapewe tenda wakati Tanesco waliikataa Richmond kuwa haifai. Lowassa ndiye mhusika mkuu wa kashfa ya ufisadi ya Richmond ndio maana alilazimika kujiuzulu. 6. Need I say more? Lowassa ni mchafu wa maadili. Anapenda sana mali, amejilimbikizia utajiri kuliko kipato chake halisi. Wafuasi wake wanamfanananisha na Jacob Zuma wa Afrika Kusini. Tofauti ya Zuma na Lowassa ni kuwa Zuma alifikishwa mahakamani na kusafishwa na mahakama. Lowassa apelekwe kortini kujibu shutuma za ufisadi, akishinda kesi ndio atakuwa amesafishwa kweli. Si kwa kutumia vyombo vya habari na waandishi wa habari wenye njaa.

Yes you need to say more! Hivi kuwa tajiri ni ufisadi? We mwenyewe umesema kuwa anamiliki makampuni ya Alfa well and good, ulitaka ashinde akipiga porojo na kucheza bao ndo umeone sio fisadi, Lowassa is a hard working man, ndo maana akawa tajiri, tuambie Richmond serikali ilimlipa Lowassa kiasi gani, au ni fedha kiasi gani lowassa amechota, watanzania tuache wivu wa kike! Wakati sisi tumekaa nyuma ya keyboard tunapiga majungu wenzetu wanatafuta, wakipata tunalia foul! Tuamke!
 
Lowasa hasafishiki hata kwa washing machine,tunamtaka sana sisi wa upande wa pili ccm wampitishe agombee ili tukiangamize chama cha magamba hapo 2015.
 
Kaka sababu no.1,3,4,5,6,9,10 zinaweza mfanya awe raisi ila ya 2 ndo inamwalibia kila kitu ukiongeza na ya 13 uwiii
 
Baba wa Taifa alituhusia"mtu mwenye kuitamani Ikulu na hasa akipita huko na huko tena ana honga pesa hatufai! tumuogope kama ukoma! tumuulize izo pesa kapata wapi? atazilipaje? Ikulu kunabihashara gani? Ikulu ni mzigo hapafai kukimbiliwa"
Historia ni jambo zuri sana na inafaa tuwe tunaifuatilia mara kwa mara kwani inatuwezesha kujua tunapotoka, tulipo na tunapokwenda.
Rais tulienae ilimchukua miaka 10 kwenda Ikulu na tena kwa gharama kubwa sana, swali la mimi na wewe kujiuliza, pamoja na nguvu zote alizo/ zilizotumika kumuingiza Ikulu je katenda sawa na matarajio ya watanzania walio wengi? Jibu tunalo wewe na mimi!
Mbinu alizotumia ndo za bwana Lowasa anazozitumia na sababu historia inatulazimisha kujua tulikotoka na tulipo, Mheshimiwa Lowasa will obvious be the same as the current president. Hata awe jasri kiasi gani itabidi awatumikie waliomfadhili. Hasikudanganye mtu kuwa wanasiasa wanatumia pesa zao.Za kwao ni zakuweka bank na kuhonga wanawake ila za wenye kuamini kuwa watafaidika na uwepo wa mwanasiasa huyo ndo huwa wachangiaji wakubwa.
 
22. Anapendwa sana lakini pia anachukiwa sana! anaweza kuwa mgombea aliyepitia tanuru kali hivyo atakuwa ameiva kukabili mgombea wa upinzani.
 
Hata zamani nilikuwa na mtazamo huo.lakini utakunisaidia kwa Rais wetu mstaafu ALLI HASSAN MWINYI alijiuzuru wakati ni waziri wa mambo ya ndani wa jamuhuri ya muungano ya tanzania alikuwa amefanya madudu gani?na madudu yake yalikuwaje yakamfanya awe rais wetu?ebu jaribu kutaja uwezo wake na udhaifu wake Lowasa ambao utatushawishi tuwe upande mmoja wa kukubaliana.na uwe na ushahidi wa kutosha.ok unaenda vizuri kuonyesha taarifa za vyanzo ambavyo vimetufikisha hapa.MIMI LOWASA NIMEMKUBALI.endelea unakwenda vizuri.ahsante

Kuwajibika kwa Mwinyi ni tofauti na Lowasa.Lowassa anahusishwa na mkataba wa kirushwa rushwa,ni aibu kwa mtu katika position yake kulazimisha waru waingie mkataba ambao wataalamu waliona mzabuni hafai.That alone is the very great weakness.
 
Watu wakiwa hawana HOJA wanaleta VIHOJA.

Lowassa alishasema: HAKUNA ALILOFANYA KWENYE RICHMOND AMBALO MWENYEKITI HAKUKIBARIKI AU HAKULIJUA.

Wote mmebaki ooh ana mali sijui kanunua nyumba. Hoja za kuishiwa mbaya sana na akili za kufikiriwa na magazeti sio nzuri kabisa

Mkuu unachotetea hapo ni sawa na mwizi akiulizwa;

Swali: Wewe kwa nini uliiba,na ilihali unajua wizi ni kosa.?

Jibu: Ndio niliiba lakini hata baba yangu alikua anajua kila kitu na alinipa go ahead ya kuiba.

Tafakuri: Je kwa jibu hilo kunamfanya mwizi awe msafi? THINK BIG MKUU,SIO KUMSIFIA SIFIA TU MTU.Lowassa anautafuta urais kwa nguvu mwaka 2011,uchaguzi 2015,kuna nini anataka?/
 
Ndugu umejitahidi sana kutoa sababu nzuri but kitendo cha jamii kumuona mtu fulani ana doa la ufisadi ni sababu tosha ya kumpiga chini katika ngazi yeyote ya uongozi. Ikulu ni mahali patakatifu na haifai shetani kukanyaga mahali hapo.
 
Zipo nyingi zaidi ya hizo. Kikubwa zaidi anaweza kufanya maamuzi magumu, kama ya kujiuzulu ili amwokoe JEI KEI na scandal ya richmond
 
Yes you need to say more! Hivi kuwa tajiri ni ufisadi? We mwenyewe umesema kuwa anamiliki makampuni ya Alfa well and good, ulitaka ashinde akipiga porojo na kucheza bao ndo umeone sio fisadi, Lowassa is a hard working man, ndo maana akawa tajiri, tuambie Richmond serikali ilimlipa Lowassa kiasi gani, au ni fedha kiasi gani lowassa amechota, watanzania tuache wivu wa kike! Wakati sisi tumekaa nyuma ya keyboard tunapiga majungu wenzetu wanatafuta, wakipata tunalia foul! Tuamke!
Usijichanganye wewe, kuwa tajiri kwa njia sahihi zinazo eleweka sio tatizo ila kuwa tajiri kwa kupora rasilimali za nchi ni balaa na hatari kubwa, unapokuwa kiongozi wa umma na mapato yako yanafahamika ikatokea ukajiingiza kwenye biashara huna budi kuujulisha umma ni kwa vipi umeweza kujiingiza kwenye biashara ili kutoa mashaka kwa umma.

Na ili kujua mapato na mali unazomiliki kama ni za kihalali mbona sio kazi ngumu, kinachotakiwa ni kujua ulipaji wako wa kodi ukilinganishwa na mali ulizonazo, kama haviendani pato lako litakuwa la kifisadi. Na rushwa hailipiwi kodi ila huwekezwa (kwenye nchi zetu zisizo na taratibu ya ku-track mapato) na hatimaye huonekana si haramu ila mali inakuwa halali.
 
Watu wakiwa hawana HOJA wanaleta VIHOJA.

Lowassa alishasema: HAKUNA ALILOFANYA KWENYE RICHMOND AMBALO MWENYEKITI HAKUKIBARIKI AU HAKULIJUA.

Wote mmebaki ooh ana mali sijui kanunua nyumba. Hoja za kuishiwa mbaya sana na akili za kufikiriwa na magazeti sio nzuri kabisa

Indirectly alikuwa anaonyesha unafiki wa wana CCM.

Ripoti ya Kamati ya Mukama inasema kwamba mojawapo ya sababu zilizofanya CCM ifanye vibaya uchaguzi wa mwaka jana ni UFISADI. Hawakwenda deep kutaja ni ufisadi gani na watu gani ambao wanatuhumiwa na huo ufisadi. Bali wakaishia kusema kwamba kuna watu walio ndani ya CCM na serikalini ambao wanatajwa na wananchi kwamba ni mafisadi.

Linapokuja swala zima la ufisadi, wana CCM wengi huwa wanatamani kumnasua Mwenyekiti wao ili asiwemo. Jitihada hizo zilianzia kwa wale waliokuwa wakijiita "wapambanaji" kwa kusema JK ni msafi. JK naye huwa anafanya jitihada za kujinasua bila mafanikio. Baada ya kauli ya Lowassa, akina Nape sasa wametulia kimya na akina Mukama wamebaki kubweka tu na hawajui watakachofanya next, maana kama hoja ilikuwa ni ufisadi then na JK nae aondoke kwenye chama, which is impossible.

Sasa wamekuja na idea mpya kwamba iundwe kamati ya nidhamu na maadili ya kushughulikia swala la kuvuana magamba. But Kamati za Maadili zipo kuanzia ngazi ya Tawi mpaka Taifa, iweje leo hii swala la kuvuana magamba liundiwe kamati tofauti? Ngoma imeishakuwa ngumu. Siasa za unafiki za CCM zimefika mahali zinawazamisha wote. Kama ni swala la kutajwa, Dr. Slaa alishataja LIST OF SHAME pale Mwembe Yanga na JK alikuwa ndani ya orodha na vigogo kibao wa CCM.

Kama kigezo ni ufisadi, hakuna ambaye anafaa kuwa Rais kutoka CCM!
 
Ukweli ni kwamba mti wenye matunda ndio hurushiwa mawe
 
Yes you need to say more! Hivi kuwa tajiri ni ufisadi? We mwenyewe umesema kuwa anamiliki makampuni ya Alfa well and good, ulitaka ashinde akipiga porojo na kucheza bao ndo umeone sio fisadi, Lowassa is a hard working man, ndo maana akawa tajiri, tuambie Richmond serikali ilimlipa Lowassa kiasi gani, au ni fedha kiasi gani lowassa amechota, watanzania tuache wivu wa kike! Wakati sisi tumekaa nyuma ya keyboard tunapiga majungu wenzetu wanatafuta, wakipata tunalia foul! Tuamke!

Ndio Lowassa ni hard working kwenye kufanya ufisadi, kwani haiwezekani kiongozi wa umma akajilimbikizia mali nyingi kiasi hiki kama yeye. Huyu Lowassa ni mwizi tu, na Tanzania ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere haihitaji viongozi fisadi. Mamluki wote mnaotumiwa kumsafisha Lowassa humu JF kamwe hamtafanikiwa. Mwambieni master wenu kuwa kachafuka chakari na ajilaumu mwenyewe kwa ufisadi wake. That's what's up, you heard?
 
Namba 14 sio nzuri??? inaeleta element za udini... Plz futa hiyo
 
Indirectly alikuwa anaonyesha unafiki wa wana CCM.

Ripoti ya Kamati ya Mukama inasema kwamba mojawapo ya sababu zilizofanya CCM ifanye vibaya uchaguzi wa mwaka jana ni UFISADI. Hawakwenda deep kutaja ni ufisadi gani na watu gani ambao wanatuhumiwa na huo ufisadi. Bali wakaishia kusema kwamba kuna watu walio ndani ya CCM na serikalini ambao wanatajwa na wananchi kwamba ni mafisadi.

Linapokuja swala zima la ufisadi, wana CCM wengi huwa wanatamani kumnasua Mwenyekiti wao ili asiwemo. Jitihada hizo zilianzia kwa wale waliokuwa wakijiita "wapambanaji" kwa kusema JK ni msafi. JK naye huwa anafanya jitihada za kujinasua bila mafanikio. Baada ya kauli ya Lowassa, akina Nape sasa wametulia kimya na akina Mukama wamebaki kubweka tu na hawajui watakachofanya next, maana kama hoja ilikuwa ni ufisadi then na JK nae aondoke kwenye chama, which is impossible.

Sasa wamekuja na idea mpya kwamba iundwe kamati ya nidhamu na maadili ya kushughulikia swala la kuvuana magamba. But Kamati za Maadili zipo kuanzia ngazi ya Tawi mpaka Taifa, iweje leo hii swala la kuvuana magamba liundiwe kamati tofauti? Ngoma imeishakuwa ngumu. Siasa za unafiki za CCM zimefika mahali zinawazamisha wote. Kama ni swala la kutajwa, Dr. Slaa alishataja LIST OF SHAME pale Mwembe Yanga na JK alikuwa ndani ya orodha na vigogo kibao wa CCM.

Kama kigezo ni ufisadi, hakuna ambaye anafaa kuwa Rais kutoka CCM!

Lakini kuna anayefaa kuwa mgombea urais kupitia CCM!!! hata kama atashindwa. Zipo sababu Hamsini za Lowasa kupewa tiketi ya kugombea urais ingawa atashindwa. Wote tuendelee kutafakari kujadili hadi zifike 50 bila kumpendelea wala kumuonea!
 
Namba 14 sio nzuri??? inaeleta element za udini... Plz futa hiyo

CCM ni chama cha udini kwa hiyo mgombea wake mwaka 2015 ni lazima awe mkristo!!!!! wenyewe wanajuana kwa udini wao na ndiyo maana hujasikia Muislam yeyote ambaye yuko kwenye mbio za kugombea tiketi hiyo! Ngoja nikukumbushe walioko kwenye mbio hizo. Fredrick Sumaye, Samuel Sitta, Edward Lowasa, Prof. Mwandosya, Membe, Pombe Magufuli nk. Wakina Dr. Bilal, Salim, Mwinyi, Mkullo, Meghji nk wanajua kuwa siyo zamu yao!!!!!!
 
23. Atakuwa ni mtu muhimu mwenye turufu ya CCM ku neutralise vuguvugu kubwa la CHADEMA lililoko kanda ya kaskazini hasa mkoani Arusha.
 
Yes you need to say more! Hivi kuwa tajiri ni ufisadi? We mwenyewe umesema kuwa anamiliki makampuni ya Alfa well and good, ulitaka ashinde akipiga porojo na kucheza bao ndo umeone sio fisadi, Lowassa is a hard working man, ndo maana akawa tajiri, tuambie Richmond serikali ilimlipa Lowassa kiasi gani, au ni fedha kiasi gani lowassa amechota, watanzania tuache wivu wa kike! Wakati sisi tumekaa nyuma ya keyboard tunapiga majungu wenzetu wanatafuta, wakipata tunalia foul! Tuamke!

unajua mkuu wakat mwingine utumiage hata akili ya kuzaliwa kujibu kitu kwa kuangalia uhalisia wa mambo. Hatujawahi kusikia EL ana mashamba kwao analima, ameanza kwa kufanya biashara flan, alikuwa mbeba zege mahali flan au hata kusikia kuwa ukwasi wake ulitokana na wazazi wake kuwa nazo hivyo akafanya kazi kwa bidii na kufikia hapo alipo. R A inasemekana ukwasi wake umetokana na biashara zake ambazo zimetokana na wazazi wake, sasa je, chanzo cha ukwasi wake ni nini? Au alizaliwa nao? Kama ndivyo, kwa nini asieleze aliko utoa wakati sheria inamtaka kama kiongozi kueleza vyanzo vya ukwasi wake?
 
Back
Top Bottom